1 Wafalme 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 21 (Swahili) 1st Kings 21 (English)

Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. 1 Wafalme 21:1

It happened after these things, that Naboth the Jezreelite had a vineyard, which was in Jezreel, hard by the palace of Ahab king of Samaria.

Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. 1 Wafalme 21:2

Ahab spoke to Naboth, saying, Give me your vineyard, that I may have it for a garden of herbs, because it is near to my house; and I will give you for it a better vineyard than it: or, if it seem good to you, I will give you the worth of it in money.

Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. 1 Wafalme 21:3

Naboth said to Ahab, Yahweh forbid it me, that I should give the inheritance of my fathers to you.

Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula. 1 Wafalme 21:4

Ahab came into his house sullen and angry because of the word which Naboth the Jezreelite had spoken to him; for he had said, I will not give you the inheritance of my fathers. He laid him down on his bed, and turned away his face, and would eat no bread.

Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? 1 Wafalme 21:5

But Jezebel his wife came to him, and said to him, Why is your spirit so sad, that you eat no bread?

Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. 1 Wafalme 21:6

He said to her, Because I spoke to Naboth the Jezreelite, and said to him, Give me your vineyard for money; or else, if it please you, I will give you [another] vineyard for it: and he answered, I will not give you my vineyard.

Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. 1 Wafalme 21:7

Jezebel his wife said to him, Do you now govern the kingdom of Israel? arise, and eat bread, and let your heart be merry: I will give you the vineyard of Naboth the Jezreelite.

Basi, akaandika nyaraka kwa jina la Ahabu, akazitia muhuri yake, akazipeleka zile nyaraka kwa wazee, na kwa watu wenye nguvu waliokuwa katika mji wake, waliokaa pamoja na Nabothi. 1 Wafalme 21:8

So she wrote letters in Ahab's name, and sealed them with his seal, and sent the letters to the elders and to the nobles who were in his city, [and] who lived with Naboth.

Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu, 1 Wafalme 21:9

She wrote in the letters, saying, Proclaim a fast, and set Naboth on high among the people:

mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe. 1 Wafalme 21:10

and set two men, base fellows, before him, and let them testify against him, saying, You did curse God and the king. Then carry him out, and stone him to death.

Wale wazee wa mji wake, na walio wenye nguvu waliokaa mjini mwake, wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea. 1 Wafalme 21:11

The men of his city, even the elders and the nobles who lived in his city, did as Jezebel had sent to them, according as it was written in the letters which she had sent to them.

Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu. 1 Wafalme 21:12

They proclaimed a fast, and set Naboth on high among the people.

Na hao watu wawili, watu wasiofaa, wakaingia, wakaketi mbele yake; wale watu wasiofaa wakamshuhudia Nabothi mbele ya watu, wakasema, Nabothi amemtukana Mungu na mfalme. Ndipo wakamchukua nje ya mji, wakampiga kwa mawe hata akafa. 1 Wafalme 21:13

The two men, the base fellows, came in and sat before him: and the base fellows bore witness against him, even against Naboth, in the presence of the people, saying, Naboth did curse God and the king. Then they carried him forth out of the city, and stoned him to death with stones.

Wakampelekea Yezebeli habari, wakasema, Nabothi amepigwa kwa mawe, amekufa. 1 Wafalme 21:14

Then they sent to Jezebel, saying, Naboth is stoned, and is dead.

Ikawa Yezebeli aliposikia ya kwamba Nabothi amepigwa kwa mawe na kufa, Yezebeli akamwambia Ahabu, Inuka, ulitamalaki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, alilokataa kukupa kwa fedha, maana Nabothi hako hai, lakini amekufa. 1 Wafalme 21:15

It happened, when Jezebel heard that Naboth was stoned, and was dead, that Jezebel said to Ahab, Arise, take possession of the vineyard of Naboth the Jezreelite, which he refused to give you for money; for Naboth is not alive, but dead.

Ikawa Ahabu aliposikia ya kwamba Nabothi amekufa, akaondoka, alitelemkie shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ili alitamalaki. 1 Wafalme 21:16

It happened, when Ahab heard that Naboth was dead, that Ahab rose up to go down to the vineyard of Naboth the Jezreelite, to take possession of it.

Neno la Bwana likamjia Eliya Mtishbi, kusema, 1 Wafalme 21:17

The word of Yahweh came to Elijah the Tishbite, saying,

Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. 1 Wafalme 21:18

Arise, go down to meet Ahab king of Israel, who dwells in Samaria: behold, he is in the vineyard of Naboth, where he is gone down to take possession of it.

Ukamwambie, ukisema, Bwana asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, Bwana asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako. 1 Wafalme 21:19

You shall speak to him, saying, Thus says Yahweh, Have you killed and also taken possession? You shall speak to him, saying, Thus says Yahweh, In the place where dogs licked the blood of Naboth shall dogs lick your blood, even yours.

Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa Bwana. 1 Wafalme 21:20

Ahab said to Elijah, Have you found me, my enemy? He answered, I have found you, because you have sold yourself to do that which is evil in the sight of Yahweh.

Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli. 1 Wafalme 21:21

Behold, I will bring evil on you, and will utterly sweep you away and will cut off from Ahab every man-child, and him who is shut up and him who is left at large in Israel:

Kisha nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha Israeli. 1 Wafalme 21:22

and I will make your house like the house of Jeroboam the son of Nebat, and like the house of Baasha the son of Ahijah for the provocation with which you have provoked me to anger, and have made Israel to sin.

Tena Bwana alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli. 1 Wafalme 21:23

Of Jezebel also spoke Yahweh, saying, The dogs shall eat Jezebel by the rampart of Jezreel.

Mtu wa nyumba ya Ahabu afaye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashambani ndege wa angani watamla. 1 Wafalme 21:24

Him who dies of Ahab in the city the dogs shall eat; and him who dies in the field shall the birds of the sky eat.

(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. 1 Wafalme 21:25

(But there was none like Ahab, who did sell himself to do that which was evil in the sight of Yahweh, whom Jezebel his wife stirred up.

Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.) 1 Wafalme 21:26

He did very abominably in following idols, according to all that the Amorites did, whom Yahweh cast out before the children of Israel.)

Ikawa, Ahabu alipoyasikia maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. 1 Wafalme 21:27

It happened, when Ahab heard those words, that he tore his clothes, and put sackcloth on his flesh, and fasted, and lay in sackcloth, and went softly.

Neno la Bwana likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema, 1 Wafalme 21:28

The word of Yahweh came to Elijah the Tishbite, saying,

Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake. 1 Wafalme 21:29

See you how Ahab humbles himself before me? because he humbles himself before me, I will not bring the evil in his days; but in his son's days will I bring the evil on his house.