1 Wafalme 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 6 (Swahili) 1st Kings 6 (English)

Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana. 1 Wafalme 6:1

It happened in the four hundred and eightieth year after the children of Israel were come out of the land of Egypt, in the fourth year of Solomon's reign over Israel, in the month Ziv, which is the second month, that he began to build the house of Yahweh.

Nayo nyumba hiyo mfalme Sulemani aliyomjengea Bwana, urefu wake ulikuwa mikono sitini, na upana wake ishirini, na kwenda juu kwake mikono thelathini. 1 Wafalme 6:2

The house which king Solomon built for Yahweh, the length of it was sixty cubits, and the breadth of it twenty [cubits], and the height of it thirty cubits.

Na ukumbi mbele ya hekalu la nyumba, urefu wake ulikuwa mikono ishirini, kadiri ya upana wa nyumba; na upana wake mikono kumi mbele ya nyumba. 1 Wafalme 6:3

The porch before the temple of the house, twenty cubits was the length of it, according to the breadth of the house; [and] ten cubits was the breadth of it before the house.

Akaifanyia nyumba madirisha ya miangaza yenye kimia. 1 Wafalme 6:4

For the house he made windows of fixed lattice-work.

Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kote kote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote. 1 Wafalme 6:5

Against the wall of the house he built stories round about, against the walls of the house round about, both of the temple and of the oracle; and he made side-chambers round about.

Chumba cha chini kilikuwa mikono mitano upana wake, na chumba cha katikati kilikuwa mikono sita upana wake, na chumba cha tatu kilikuwa mikono saba upana wake; kwa kuwa upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane kutani mwa nyumba. 1 Wafalme 6:6

The nethermost story was five cubits broad, and the middle was six cubits broad, and the third was seven cubits broad; for on the outside he made offsets [in the wall] of the house round about, that [the beams] should not have hold in the walls of the house.

Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba. 1 Wafalme 6:7

The house, when it was in building, was built of stone made ready at the quarry; and there was neither hammer nor axe nor any tool of iron heard in the house, while it was in building.

Mlango wa vyumba vya chini ulikuwapo upande wa kuume wa nyumba; mtu hupanda madaraja ya kuzunguka mpaka vyumba vya katikati, na kutoka vile vya katikati mpaka vile vya tatu. 1 Wafalme 6:8

The door for the middle side-chambers was in the right side of the house: and they went up by winding stairs into the middle [story], and out of the middle into the third.

Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi. 1 Wafalme 6:9

So he built the house, and finished it; and he covered the house with beams and planks of cedar.

Akavijenga vyumba mbavuni mwa nyumba yote, kwenda juu kwake kila kimoja kilikuwa mikono mitano; vikaitegemea nyumba kwa boriti za mwerezi. 1 Wafalme 6:10

He built the stories against all the house, each five cubits high: and they rested on the house with timber of cedar.

Neno la Bwana likamjia Sulemani, kusema, 1 Wafalme 6:11

The word of Yahweh came to Solomon, saying,

Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako. 1 Wafalme 6:12

Concerning this house which you are building, if you will walk in my statutes, and execute my ordinances, and keep all my commandments to walk in them; then will I establish my word with you, which I spoke to David your father.

Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli. 1 Wafalme 6:13

I will dwell among the children of Israel, and will not forsake my people Israel.

Basi Sulemani akaijenga hiyo nyumba akaimaliza. 1 Wafalme 6:14

So Solomon built the house, and finished it.

Akazijenga kuta za nyumba ndani kwa mbao za mwerezi; toka sakafu ya nyumba hata boriti za juu, akazifunika ndani kwa mti; akafunika sakafu ya nyumba kwa mbao za mberoshi. 1 Wafalme 6:15

He built the walls of the house within with boards of cedar: from the floor of the house to the walls of the ceiling, he covered them on the inside with wood; and he covered the floor of the house with boards of fir.

Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu. 1 Wafalme 6:16

He built twenty cubits on the hinder part of the house with boards of cedar from the floor to the walls [of the ceiling]: he built [them] for it within, for an oracle, even for the most holy place.

Nayo nyumba, ndiyo hekalu la mbele, ilikuwa mikono arobaini. 1 Wafalme 6:17

The house, that is, the temple before [the oracle], was forty cubits [long].

Na ndani ya nyumba, mlikuwa na mwerezi ulionakishiwa maboga na maua yaliyofunuka wazi; mlikuwa na mwerezi mahali pote; wala mawe hayakuonekana. 1 Wafalme 6:18

There was cedar on the house within, carved with buds and open flowers: all was cedar; there was no stone seen.

Akaweka tayari chumba cha ndani katikati ya nyumba ndani, ili atie humo sanduku la agano la Bwana. 1 Wafalme 6:19

He prepared an oracle in the midst of the house within, to set there the ark of the covenant of Yahweh.

Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na dhahabu safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi. 1 Wafalme 6:20

Within the oracle was [a space of] twenty cubits in length, and twenty cubits in breadth, and twenty cubits in the height of it; and he overlaid it with pure gold: and he covered the altar with cedar.

Hivyo Sulemani akaifunika nyumba ndani kwa dhahabu safi. Akaitenga kwa mikufu ya dhahabu mbele ya chumba cha ndani; akapafunika na dhahabu. 1 Wafalme 6:21

So Solomon overlaid the house within with pure gold: and he drew chains of gold across before the oracle; and he overlaid it with gold.

Akaifunika nyumba yote kwa dhahabu, hata ilipokwisha nyumba yote; tena madhabahu yote iliyokuwa ya chumba cha ndani akaifunika kwa dhahabu. 1 Wafalme 6:22

The whole house he overlaid with gold, until all the house was finished: also the whole altar that belonged to the oracle he overlaid with gold.

Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono kumi. 1 Wafalme 6:23

In the oracle he made two cherubim of olive-wood, each ten cubits high.

Na bawa moja la kerubi lilikuwa mikono mitano urefu wake, na bawa la pili la kerubi mikono mitano; mikono kumi toka mwisho wa bawa moja hata mwisho wa bawa la pili. 1 Wafalme 6:24

Five cubits was the one wing of the cherub, and five cubits the other wing of the cherub: from the uttermost part of the one wing to the uttermost part of the other were ten cubits.

Na kerubi la pili lilikuwa mikono kumi; makerubi yote mawili walikuwa ya cheo kimoja na namna moja. 1 Wafalme 6:25

The other cherub was ten cubits: both the cherubim were of one measure and one form.

Kwenda juu kwake kerubi moja kulikuwa mikono kumi, na kerubi la pili vivyo. 1 Wafalme 6:26

The height of the one cherub was ten cubits, and so was it of the other cherub.

Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba. 1 Wafalme 6:27

He set the cherubim within the inner house; and the wings of the cherubim were stretched forth, so that the wing of the one touched the one wall, and the wing of the other cherub touched the other wall; and their wings touched one another in the midst of the house.

Akayafunika makerubi kwa dhahabu. 1 Wafalme 6:28

He overlaid the cherubim with gold.

Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje. 1 Wafalme 6:29

He carved all the walls of the house round about with carved figures of cherubim and palm trees and open flowers, inside and outside.

Na sakafu ya nyumba akaifunika na dhahabu ndani na nje. 1 Wafalme 6:30

The floor of the house he overlaid with gold, inside and outside.

Akayafanyia maingilio ya chumba cha ndani milango ya mzeituni; kizingiti na miimo ilikuwa ya pande tano. 1 Wafalme 6:31

For the entrance of the oracle he made doors of olive-wood: the lintel [and] door-posts were a fifth part [of the wall].

Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende. 1 Wafalme 6:32

So [he made] two doors of olive-wood; and he carved on them carvings of cherubim and palm trees and open flowers, and overlaid them with gold; and he spread the gold on the cherubim, and on the palm trees.

Ndivyo alivyoyafanyia maingilio ya hekalu miimo ya mzeituni, yenye pande nne; 1 Wafalme 6:33

So also made he for the entrance of the temple door-posts of olive-wood, out of a fourth part [of the wall];

na milango miwili ya mberoshi; mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa za kukunjana, na mbao mbili za mlango wa pili za kukunjana. 1 Wafalme 6:34

and two doors of fir-wood: the two leaves of the one door were folding, and the two leaves of the other door were folding.

Akanakshi juu yake makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi; akazifunika kwa dhahabu iliyonyoshwa juu ya machoro. 1 Wafalme 6:35

He carved [thereon] cherubim and palm trees and open flowers; and he overlaid them with gold fitted on the engraved work.

Akaijengea behewa ya ndani safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi. 1 Wafalme 6:36

He built the inner court with three courses of hewn stone, and a course of cedar beams.

Katika mwaka wa nne nyumba ya Bwana ilitiwa msingi, katika mwezi wa Zivu. 1 Wafalme 6:37

In the fourth year was the foundation of the house of Yahweh laid, in the month Ziv.

Hata katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, na sharti zake zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.

1 Wafalme 6:38

In the eleventh year, in the month Bul, which is the eighth month, was the house finished throughout all the parts of it, and according to all the fashion of it. So was he seven years in building it.