1 Wafalme 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 15 (Swahili) 1st Kings 15 (English)

Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu ya Yuda. 1 Wafalme 15:1

Now in the eighteenth year of king Jeroboam the son of Nebat began Abijam to reign over Judah.

Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu. 1 Wafalme 15:2

Three years reigned he in Jerusalem: and his mother's name was Maacah the daughter of Abishalom.

Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye. 1 Wafalme 15:3

He walked in all the sins of his father, which he had done before him; and his heart was not perfect with Yahweh his God, as the heart of David his father.

Walakini kwa ajili ya Daudi, Bwana, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu; 1 Wafalme 15:4

Nevertheless for David's sake did Yahweh his God give him a lamp in Jerusalem, to set up his son after him, and to establish Jerusalem;

kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti. 1 Wafalme 15:5

because David did that which was right in the eyes of Yahweh, and didn't turn aside from anything that he commanded him all the days of his life, except only in the matter of Uriah the Hittite.

Basi kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote za maisha yake. 1 Wafalme 15:6

Now there was war between Rehoboam and Jeroboam all the days of his life.

Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 1 Wafalme 15:7

The rest of the acts of Abijam, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah? There was war between Abijam and Jeroboam.

Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake. 1 Wafalme 15:8

Abijam slept with his fathers; and they buried him in the city of David: and Asa his son reigned in his place.

Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa alianza kutawala juu ya Yuda. 1 Wafalme 15:9

In the twentieth year of Jeroboam king of Israel began Asa to reign over Judah.

Akatawala miaka arobaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu. 1 Wafalme 15:10

Forty-one years reigned he in Jerusalem: and his mother's name was Maacah the daughter of Abishalom.

Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi. 1 Wafalme 15:11

Asa did that which was right in the eyes of Yahweh, as did David his father.

Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake. 1 Wafalme 15:12

He put away the sodomites out of the land, and removed all the idols that his fathers had made.

Hata na Maaka, mamaye, akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake akaiteketeza penye kijito cha Kidroni. 1 Wafalme 15:13

Also Maacah his mother he removed from being queen, because she had made an abominable image for an Asherah; and Asa cut down her image, and burnt it at the brook Kidron.

Lakini mahali pa juu hapakuondoshwa; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu kwa Bwana siku zake zote. 1 Wafalme 15:14

But the high places were not taken away: nevertheless the heart of Asa was perfect with Yahweh all his days.

Akavileta vile vitu alivyovitakasa baba yake, na vile alivyovitakasa yeye mwenyewe, katika nyumba ya Bwana, fedha; na dhahabu, na vyombo. 1 Wafalme 15:15

He brought into the house of Yahweh the things that his father had dedicated, and the things that himself had dedicated, silver, and gold, and vessels.

Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote. 1 Wafalme 15:16

There was war between Asa and Baasha king of Israel all their days.

Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akaondoka juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda. 1 Wafalme 15:17

Baasha king of Israel went up against Judah, and built Ramah, that he might not allow anyone to go out or come in to Asa king of Judah.

Ndipo Asa akazitwaa fedha zote na dhahabu zilizosalia katika hazina za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme, akazitia mikononi mwa watumishi wake; mfalme Asa akawatuma kwa Ben-hadadi, mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema, 1 Wafalme 15:18

Then Asa took all the silver and the gold that were left in the treasures of the house of Yahweh, and the treasures of the king's house, and delivered them into the hand of his servants; and king Asa sent them to Ben Hadad, the son of Tabrimmon, the son of Hezion, king of Syria, who lived at Damascus, saying,

Tumepatana mimi nawe, na baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea zawadi, fedha na dhahabu; basi nenda, uyavunje mapatano yako na Baasha mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi. 1 Wafalme 15:19

[There is] a league between me and you, between my father and your father: behold, I have sent to you a present of silver and gold; go, break your league with Baasha king of Israel, that he may depart from me.

Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali. 1 Wafalme 15:20

Ben Hadad listened to king Asa, and sent the captains of his armies against the cities of Israel, and struck Ijon, and Dan, and Abel Beth Maacah, and all Chinneroth, with all the land of Naphtali.

Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo akaacha kuujenga Rama, akaenda akakaa Tirza. 1 Wafalme 15:21

It happened, when Baasha heard of it, that he left off building Ramah, and lived in Tirzah.

Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa. 1 Wafalme 15:22

Then king Asa made a proclamation to all Judah; none was exempted: and they carried away the stones of Ramah, and the timber of it, with which Baasha had built; and king Asa built therewith Geba of Benjamin, and Mizpah.

Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu. 1 Wafalme 15:23

Now the rest of all the acts of Asa, and all his might, and all that he did, and the cities which he built, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah? But in the time of his old age he was diseased in his feet.

Asa akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake. Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake. 1 Wafalme 15:24

Asa slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David his father; and Jehoshaphat his son reigned in his place.

Nadabu mwana wa Yeroboamu alianza kutawala juu ya Israeli, mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala juu ya Israeli miaka miwili. 1 Wafalme 15:25

Nadab the son of Jeroboam began to reign over Israel in the second year of Asa king of Judah; and he reigned over Israel two years.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli. 1 Wafalme 15:26

He did that which was evil in the sight of Yahweh, and walked in the way of his father, and in his sin with which he made Israel to sin.

Basi Baasha wa Ahiya, wa mbari ya Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni. 1 Wafalme 15:27

Baasha the son of Ahijah, of the house of Issachar, conspired against him; and Baasha struck him at Gibbethon, which belonged to the Philistines; for Nadab and all Israel were laying siege to Gibbethon.

Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake. 1 Wafalme 15:28

Even in the third year of Asa king of Judah did Baasha kill him, and reigned in his place.

Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi ye yote, hata alipomharibu sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni; 1 Wafalme 15:29

It happened that, as soon as he was king, he struck all the house of Jeroboam: he didn't leave to Jeroboam any who breathed, until he had destroyed him; according to the saying of Yahweh, which he spoke by his servant Ahijah the Shilonite;

kwa sababu ya makosa yake Yeroboamu aliyoyakosa, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; kwa sababu ya chukizo lake alilomchukiza Bwana, Mungu wa Israeli, hata kumghadhibisha. 1 Wafalme 15:30

for the sins of Jeroboam which he sinned, and with which he made Israel to sin, because of his provocation with which he provoked Yahweh, the God of Israel, to anger.

Basi mambo yote ya Nadabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 1 Wafalme 15:31

Now the rest of the acts of Nadab, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Israel?

Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote. 1 Wafalme 15:32

There was war between Asa and Baasha king of Israel all their days.

Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kutawala juu ya Israeli wote huko Tirza, akatawala miaka ishirini na minne. 1 Wafalme 15:33

In the third year of Asa king of Judah began Baasha the son of Ahijah to reign over all Israel in Tirzah, [and reigned] twenty-four years.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli. 1 Wafalme 15:34

He did that which was evil in the sight of Yahweh, and walked in the way of Jeroboam, and in his sin with which he made Israel to sin.