1 Wafalme 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 5 (Swahili) 1st Kings 5 (English)

Ndipo Hiramu, mfalme wa Tiro, akawatuma watumishi wake kwa Sulemani; kwani alikuwa amesikia ya kwamba wamemtia mafuta awe mfalme mahali pa baba yake. Kwa maana Hiramu alikuwa akimpenda Daudi siku zote. 1 Wafalme 5:1

Hiram king of Tyre sent his servants to Solomon; for he had heard that they had anointed him king in the room of his father: for Hiram was ever a lover of David.

Basi Sulemani akatuma watu kwa Hiramu, akasema, 1 Wafalme 5:2

Solomon sent to Hiram, saying,

Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata Bwana alipowatia watu chini ya nyayo zake. 1 Wafalme 5:3

You know how that David my father could not build a house for the name of Yahweh his God for the wars which were about him on every side, until Yahweh put them under the soles of his feet.

Ila leo Bwana, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya. 1 Wafalme 5:4

But now Yahweh my God has given me rest on every side; there is neither adversary, nor evil occurrence.

Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wangu, kama Bwana alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 1 Wafalme 5:5

Behold, I purpose to build a house for the name of Yahweh my God, as Yahweh spoke to David my father, saying, Your son, whom I will set on your throne in your room, he shall build the house for my name.

Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni. 1 Wafalme 5:6

Now therefore command you that they cut me cedar trees out of Lebanon; and my servants shall be with your servants; and I will give you hire for your servants according to all that you shall say: for you know that there is not among us any who knows how to cut timber like the Sidonians.

Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe Bwana leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi. 1 Wafalme 5:7

It happened, when Hiram heard the words of Solomon, that he rejoiced greatly, and said, Blessed be Yahweh this day, who has given to David a wise son over this great people.

Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi. 1 Wafalme 5:8

Hiram sent to Solomon, saying, I have heard [the message] which you have sent to me: I will do all your desire concerning timber of cedar, and concerning timber of fir.

Watumishi wangu wataishusha toka Lebanoni mpaka baharini; nami nitaiendesha baharini, ikifungwa pamoja, mpaka mahali utakaponiagiza, huko nitaifungua ili wewe uichukue; ndivyo utakavyoitimiza haja yangu, ukiwapa chakula watu wa nyumbani mwangu. 1 Wafalme 5:9

My servants shall bring them down from Lebanon to the sea; and I will make them into rafts to go by sea to the place that you shall appoint me, and will cause them to be broken up there, and you shall receive them; and you shall accomplish my desire, in giving food for my household.

Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka. 1 Wafalme 5:10

So Hiram gave Solomon timber of cedar and timber of fir according to all his desire.

Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano, chakula cha watu wake, na kori ishirini za mafuta safi. Ndizo Sulemani alizompa Hiramu mwaka kwa mwaka. 1 Wafalme 5:11

Solomon gave Hiram twenty thousand measures of wheat for food to his household, and twenty measures of pure oil: thus gave Solomon to Hiram year by year.

Bwana akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanyana maagano pamoja hao wawili. 1 Wafalme 5:12

Yahweh gave Solomon wisdom, as he promised him; and there was peace between Hiram and Solomon; and they two made a league together.

Mfalme Sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote; nayo shokoa hiyo ilikuwa ya watu thelathini elfu. 1 Wafalme 5:13

King Solomon raised a levy out of all Israel; and the levy was thirty thousand men.

Akawatuma Lebanoni kwa mwezi, elfu kumi kwa zamu. Mwezi mmoja walikuwako huko Lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. Na Adoramu alikuwa juu ya shokoa. 1 Wafalme 5:14

He sent them to Lebanon, ten thousand a month by courses; a month they were in Lebanon, and two months at home; and Adoniram was over the men subject to forced labor.

Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatao miti themanini elfu milimani; 1 Wafalme 5:15

Solomon had seventy thousand who bore burdens, and eighty thousand who were stone cutters in the mountains;

mbali na maakida yake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na mia tatu, wasimamizi wa watu waliotenda kazi. 1 Wafalme 5:16

besides Solomon's chief officers who were over the work, three thousand and three hundred, who bore rule over the people who labored in the work.

Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa. 1 Wafalme 5:17

The king commanded, and they hewed out great stones, costly stones, to lay the foundation of the house with worked stone.

Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.

1 Wafalme 5:18

Solomon's builders and Hiram's builders and the Gebalites did fashion them, and prepared the timber and the stones to build the house.