1 Wafalme 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 13 (Swahili) 1st Kings 13 (English)

Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. 1 Wafalme 13:1

Behold, there came a man of God out of Judah by the word of Yahweh to Beth El: and Jeroboam was standing by the altar to burn incense.

Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. 1 Wafalme 13:2

He cried against the altar by the word of Yahweh, and said, altar, altar, thus says Yahweh: Behold, a son shall be born to the house of David, Josiah by name; and on you shall he sacrifice the priests of the high places who burn incense on you, and men's bones shall they burn on you.

Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika. 1 Wafalme 13:3

He gave a sign the same day, saying, This is the sign which Yahweh has spoken: Behold, the altar shall be torn, and the ashes that are on it shall be poured out.

Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. 1 Wafalme 13:4

It happened, when the king heard the saying of the man of God, which he cried against the altar in Bethel, that Jeroboam put forth his hand from the altar, saying, Lay hold on him. His hand, which he put forth against him, dried up, so that he could not draw it back again to him.

Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana. 1 Wafalme 13:5

The altar also was torn, and the ashes poured out from the altar, according to the sign which the man of God had given by the word of Yahweh.

Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza. 1 Wafalme 13:6

The king answered the man of God, Entreat now the favor of Yahweh your God, and pray for me, that my hand may be restored me again. The man of God entreated Yahweh, and the king's hand was restored him again, and became as it was before.

Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu. 1 Wafalme 13:7

The king said to the man of God, Come home with me, and refresh yourself, and I will give you a reward.

Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa; 1 Wafalme 13:8

The man of God said to the king, If you will give me half your house, I will not go in with you, neither will I eat bread nor drink water in this place;

maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia. 1 Wafalme 13:9

for so was it charged me by the word of Yahweh, saying, You shall eat no bread, nor drink water, neither return by the way that you came.

Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli. 1 Wafalme 13:10

So he went another way, and didn't return by the way that he came to Bethel.

Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao. 1 Wafalme 13:11

Now there lived an old prophet in Bethel; and one of his sons came and told him all the works that the man of God had done that day in Bethel: the words which he had spoken to the king, them also they told to their father.

Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda. 1 Wafalme 13:12

Their father said to them, Which way did he go? Now his sons had seen which way the man of God went, who came from Judah.

Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda. 1 Wafalme 13:13

He said to his sons, Saddle me the donkey. So they saddled him the donkey; and he rode thereon.

Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye. 1 Wafalme 13:14

He went after the man of God, and found him sitting under an oak; and he said to him, Are you the man of God who came from Judah? He said, I am.

Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula. 1 Wafalme 13:15

Then he said to him, Come home with me, and eat bread.

Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa; 1 Wafalme 13:16

He said, I may not return with you, nor go in with you; neither will I eat bread nor drink water with you in this place:

kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia. 1 Wafalme 13:17

for it was said to me by the word of Yahweh, You shall eat no bread nor drink water there, nor turn again to go by the way that you came.

Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo. 1 Wafalme 13:18

He said to him, I also am a prophet as you are; and an angel spoke to me by the word of Yahweh, saying, Bring him back with you into your house, that he may eat bread and drink water. [But] he lied to him.

Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake. 1 Wafalme 13:19

So he went back with him, and ate bread in his house, and drank water.

Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha; 1 Wafalme 13:20

It happened, as they sat at the table, that the word of Yahweh came to the prophet who brought him back;

akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, 1 Wafalme 13:21

and he cried to the man of God who came from Judah, saying, Thus says Yahweh, Because you have been disobedient to the mouth of Yahweh, and have not kept the commandment which Yahweh your God commanded you,

bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako. 1 Wafalme 13:22

but came back, and have eaten bread and drunk water in the place of which he said to you, Eat no bread, and drink no water; your body shall not come to the tomb of your fathers.

Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda. 1 Wafalme 13:23

It happened, after he had eaten bread, and after he had drunk, that he saddled for him the donkey, [to wit], for the prophet whom he had brought back.

Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti. 1 Wafalme 13:24

When he was gone, a lion met him by the way, and killed him: and his body was cast in the way, and the donkey stood by it; the lion also stood by the body.

Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee. 1 Wafalme 13:25

Behold, men passed by, and saw the body cast in the way, and the lion standing by the body; and they came and told it in the city where the old prophet lived.

Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya Bwana; kwa hiyo Bwana amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia. 1 Wafalme 13:26

When the prophet who brought him back from the way heard of it, he said, It is the man of God, who was disobedient to the mouth of Yahweh: therefore Yahweh has delivered him to the lion, which has torn him, and slain him, according to the word of Yahweh, which he spoke to him.

Akawaambia wanawe, akasema, Nitandikieni punda. Wakamtandikia. 1 Wafalme 13:27

He spoke to his sons, saying, Saddle me the donkey. They saddled it.

Akaenda, akamwona yule maiti ametupwa njiani, na punda na simba wamesimama karibu na maiti; yule simba alikuwa hakumla maiti, wala hakumrarua punda. 1 Wafalme 13:28

He went and found his body cast in the way, and the donkey and the lion standing by the body: the lion had not eaten the body, nor torn the donkey.

Nabii yule akamtwaa maiti wa yule mtu wa Mungu, akamweka juu ya punda wake, akamrudisha; yule nabii mzee akaenda mjini mwake, kukaa matanga, na kumzika. 1 Wafalme 13:29

The prophet took up the body of the man of God, and laid it on the donkey, and brought it back; and he came to the city of the old prophet, to mourn, and to bury him.

Akamweka maiti katika kaburi lake mwenyewe; wakamlilia, wakisema, Aa! Ndugu yangu! 1 Wafalme 13:30

He laid his body in his own grave; and they mourned over him, [saying], Alas, my brother!

Hata ikawa, alipokwisha kumzika, akawaambia wanawe, akasema, Nikifa mimi, nizikeni katika kaburi hili alimozikwa yule mtu wa Mungu; iwekeni mifupa yangu kando ya mifupa yake. 1 Wafalme 13:31

It happened, after he had buried him, that he spoke to his sons, saying, When I am dead, then bury me in the tomb in which the man of God is buried; lay my bones beside his bones.

Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la Bwana, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa. 1 Wafalme 13:32

For the saying which he cried by the word of Yahweh against the altar in Bethel, and against all the houses of the high places which are in the cities of Samaria, shall surely happen.

Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote. 1 Wafalme 13:33

After this thing Jeroboam didn't return from his evil way, but made again from among all the people priests of the high places: whoever would, he consecrated him, that there might be priests of the high places.

Kila aliyetaka akamfanya wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu. Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi. 1 Wafalme 13:34

This thing became sin to the house of Jeroboam, even to cut it off, and to destroy it from off the surface of the earth.