1 Wafalme 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 3 (Swahili) 1st Kings 3 (English)

Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya Bwana, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu. 1 Wafalme 3:1

Solomon made affinity with Pharaoh king of Egypt, and took Pharaoh's daughter, and brought her into the city of David, until he had made an end of building his own house, and the house of Yahweh, and the wall of Jerusalem round about.

Ila watu walikuwa wakichinja dhabihu katika mahali pa juu, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la Bwana, hata siku zile. 1 Wafalme 3:2

Only the people sacrificed in the high places, because there was no house built for the name of Yahweh until those days.

Sulemani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. 1 Wafalme 3:3

Solomon loved Yahweh, walking in the statutes of David his father: only he sacrificed and burnt incense in the high places.

Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile. 1 Wafalme 3:4

The king went to Gibeon to sacrifice there; for that was the great high place: a thousand burnt offerings did Solomon offer on that altar.

Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. 1 Wafalme 3:5

In Gibeon Yahweh appeared to Solomon in a dream by night; and God said, Ask what I shall give you.

Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. 1 Wafalme 3:6

Solomon said, You have shown to your servant David my father great loving kindness, according as he walked before you in truth, and in righteousness, and in uprightness of heart with you; and you have kept for him this great loving kindness, that you have given him a son to sit on his throne, as it is this day.

Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 1 Wafalme 3:7

Now, Yahweh my God, you have made your servant king instead of David my father: and I am but a little child; I don't know how to go out or come in.

Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 1 Wafalme 3:8

Your servant is in the midst of your people which you have chosen, a great people, that can't be numbered nor counted for multitude.

Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? 1 Wafalme 3:9

Give your servant therefore an understanding heart to judge your people, that I may discern between good and evil; for who is able to judge this your great people?

Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 1 Wafalme 3:10

The speech pleased the Lord, that Solomon had asked this thing.

Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 1 Wafalme 3:11

God said to him, Because you have asked this thing, and have not asked for yourself long life, neither have asked riches for yourself, nor have asked the life of your enemies, but have asked for yourself understanding to discern justice;

basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. 1 Wafalme 3:12

behold, I have done according to your word: behold, I have given you a wise and an understanding heart; so that there has been none like you before you, neither after you shall any arise like you.

Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote. 1 Wafalme 3:13

I have also given you that which you have not asked, both riches and honor, so that there shall not be any among the kings like you, all your days.

Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi. 1 Wafalme 3:14

If you will walk in my ways, to keep my statutes and my commandments, as your father David did walk, then I will lengthen your days.

Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Bwana, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote. 1 Wafalme 3:15

Solomon awoke; and, behold, it was a dream: and he came to Jerusalem, and stood before the ark of the covenant of Yahweh, and offered up burnt offerings, and offered peace-offerings, and made a feast to all his servants.

Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. 1 Wafalme 3:16

Then there came two women who were prostitutes, to the king, and stood before him.

Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. 1 Wafalme 3:17

The one woman said, Oh, my lord, I and this woman dwell in one house; and I was delivered of a child with her in the house.

Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. 1 Wafalme 3:18

It happened the third day after I was delivered, that this woman was delivered also; and we were together; there was no stranger with us in the house, save we two in the house.

Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. 1 Wafalme 3:19

This woman's child died in the night, because she lay on it.

Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. 1 Wafalme 3:20

She arose at midnight, and took my son from beside me, while your handmaid slept, and laid it in her bosom, and laid her dead child in my bosom.

Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. 1 Wafalme 3:21

When I rose in the morning to give my child suck, behold, it was dead; but when I had looked at it in the morning, behold, it was not my son, whom I bore.

Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme. 1 Wafalme 3:22

The other woman said, No; but the living is my son, and the dead is your son. This said, No; but the dead is your son, and the living is my son. Thus they spoke before the king.

Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. 1 Wafalme 3:23

Then said the king, The one says, This is my son who lives, and your son is the dead: and the other says, No; but your son is the dead, and my son is the living.

Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. 1 Wafalme 3:24

The king said, Get me a sword. They brought a sword before the king.

Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. 1 Wafalme 3:25

The king said, Divide the living child in two, and give half to the one, and half to the other.

Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. 1 Wafalme 3:26

Then spoke the woman whose the living child was to the king, for her heart yearned over her son, and she said, Oh, my lord, give her the living child, and in no way kill it. But the other said, It shall be neither mine nor yours; divide it.

Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake. 1 Wafalme 3:27

Then the king answered, Give her the living child, and in no way kill it: she is the mother of it.

Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu. 1 Wafalme 3:28

All Israel heard of the judgment which the king had judged; and they feared the king: for they saw that the wisdom of God was in him, to do justice.