1 Wafalme 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 8 (Swahili) 1st Kings 8 (English)

Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni. 1 Wafalme 8:1

Then Solomon assembled the elders of Israel, and all the heads of the tribes, the princes of the fathers' [houses] of the children of Israel, to king Solomon in Jerusalem, to bring up the ark of the covenant of Yahweh out of the city of David, which is Zion.

Wakakutana mbele ya mfalme Sulemani watu wote wa Israeli wakati wa sikukuu, katika mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba. 1 Wafalme 8:2

All the men of Israel assembled themselves to king Solomon at the feast, in the month Ethanim, which is the seventh month.

Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku. 1 Wafalme 8:3

All the elders of Israel came, and the priests took up the ark.

Wakalipandisha sanduku la Bwana, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa katika ile Hema; vitu hivyo makuhani na Walawi wakavipandisha. 1 Wafalme 8:4

They brought up the ark of Yahweh, and the tent of meeting, and all the holy vessels that were in the Tent; even these did the priests and the Levites bring up.

Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli waliokutanika kwake, walikuwako pamoja naye mbele ya sanduku, wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe, wasioweza kuhesabiwa wala kufahamiwa idadi yao kwa kuwa wengi. 1 Wafalme 8:5

King Solomon and all the congregation of Israel, who were assembled to him, were with him before the ark, sacrificing sheep and oxen, that could not be counted nor numbered for multitude.

Makuhani wakalileta sanduku la agano la Bwana hata mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi. 1 Wafalme 8:6

The priests brought in the ark of the covenant of Yahweh to its place, into the oracle of the house, to the most holy place, even under the wings of the cherubim.

Kwa maana makerubi yalinyosha mbawa zao, juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu. 1 Wafalme 8:7

For the cherubim spread forth their wings over the place of the ark, and the cherubim covered the ark and the poles of it above.

Na ile miti kwa kuwa mirefu, ncha za miti zilionekana katika mahali patakatifu, mbele ya chumba cha ndani; lakini hazikuonekana nje; nayo iko kuko huko hata leo. 1 Wafalme 8:8

The poles were so long that the ends of the poles were seen from the holy place before the oracle; but they were not seen outside: and there they are to this day.

Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri. 1 Wafalme 8:9

There was nothing in the ark save the two tables of stone which Moses put there at Horeb, when Yahweh made a covenant with the children of Israel, when they came out of the land of Egypt.

Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya Bwana ikajaa wingu; 1 Wafalme 8:10

It came to pass, when the priests were come out of the holy place, that the cloud filled the house of Yahweh,

hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya Bwana ilikuwa imejaa utukufu wa Bwana. 1 Wafalme 8:11

so that the priests could not stand to minister by reason of the cloud; for the glory of Yahweh filled the house of Yahweh.

Ndipo Sulemani akanena, Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. 1 Wafalme 8:12

Then spoke Solomon, Yahweh has said that he would dwell in the thick darkness.

Hakika nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. 1 Wafalme 8:13

I have surely built you a house of habitation, a place for you to dwell in forever.

Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama. 1 Wafalme 8:14

The king turned his face about, and blessed all the assembly of Israel: and all the assembly of Israel stood.

Akasema, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena na Daudi baba yangu kwa kinywa chake akalitimiza kwa mkono wake, akasema, 1 Wafalme 8:15

He said, Blessed be Yahweh, the God of Israel, who spoke with his mouth to David your father, and has with his hand fulfilled it, saying,

Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wo wote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nalimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli. 1 Wafalme 8:16

Since the day that I brought forth my people Israel out of Egypt, I chose no city out of all the tribes of Israel to build a house, that my name might be there; but I chose David to be over my people Israel.

Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 1 Wafalme 8:17

Now it was in the heart of David my father to build a house for the name of Yahweh, the God of Israel.

Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako. 1 Wafalme 8:18

But Yahweh said to David my father, Whereas it was in your heart to build a house for my name, you did well that it was in your heart:

Lakini wewe hutanijengea nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako, yeye ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. 1 Wafalme 8:19

nevertheless you shall not build the house; but your son who shall come forth out of your loins, he shall build the house for my name.

Basi Bwana amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama Bwana alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 1 Wafalme 8:20

Yahweh has established his word that he spoke; for I am risen up in the room of David my father, and sit on the throne of Israel, as Yahweh promised, and have built the house for the name of Yahweh, the God of Israel.

Na humo sanduku hili nimelifanyizia mahali, ambalo ndani yake mna maagano ya Bwana, aliyoyafanya na baba zetu, hapo alipowatoa katika nchi ya Misri. 1 Wafalme 8:21

There have I set a place for the ark, in which is the covenant of Yahweh, which he made with our fathers, when he brought them out of the land of Egypt.

Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake mbinguni. 1 Wafalme 8:22

Solomon stood before the altar of Yahweh in the presence of all the assembly of Israel, and spread forth his hands toward heaven;

Akasema Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote. 1 Wafalme 8:23

and he said, Yahweh, the God of Israel, there is no God like you, in heaven above, or on earth beneath; who keep covenant and loving kindness with your servants, who walk before you with all their heart;

Umemtimizia mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 1 Wafalme 8:24

who have kept with your servant David my father that which you did promise him: yes, you spoke with your mouth, and have fulfilled it with your hand, as it is this day.

Na sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, umfikilizie mtumishi wako, Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli machoni pangu, kama watoto wako wakiangalia njia zao, ili kuenenda mbele zangu kama wewe ulivyoenenda. 1 Wafalme 8:25

Now therefore, Yahweh, the God of Israel, keep with your servant David my father that which you have promised him, saying, There shall not fail you a man in my sight to sit on the throne of Israel, if only your children take heed to their way, to walk before me as you have walked before me.

Sasa, Ee Mungu wa Israeli, nakusihi, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako, Daudi, baba yangu. 1 Wafalme 8:26

Now therefore, God of Israel, Please let your word be verified, which you spoke to your servant David my father.

Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga! 1 Wafalme 8:27

But will God in very deed dwell on the earth? behold, heaven and the heaven of heavens can't contain you; how much less this house that I have built!

Walakini uyaelekee maombi ya mtumwa wako, na dua yake, Ee Bwana, Mungu wangu, uisikilize sauti na maombi ya mtumwa wako, aombayo mbele zako leo. 1 Wafalme 8:28

Yet have respect for the prayer of your servant, and for his supplication, Yahweh my God, to listen to the cry and to the prayer which your servant prays before you this day;

Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa. 1 Wafalme 8:29

that your eyes may be open toward this house night and day, even toward the place of which you have said, My name shall be there; to listen to the prayer which your servant shall pray toward this place.

Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe. 1 Wafalme 8:30

Listen you to the supplication of your servant, and of your people Israel, when they shall pray toward this place: yes, hear in heaven, your dwelling-place; and when you hear, forgive.

Ikiwa mtu amemkosa mwenzake, na kupewa sharti ya kiapo aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako, katika nyumba hii; 1 Wafalme 8:31

If a man sin against his neighbor, and an oath be laid on him to cause him to swear, and he come [and] swear before your altar in this house;

basi, usikie huko mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumwa wako; ukimpatiliza mtu mbaya, kwa kuleta njia yake juu ya kichwa chake; na kumpa mwenye haki haki yake, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake. 1 Wafalme 8:32

then hear you in heaven, and do, and judge your servants, condemning the wicked, to bring his way on his own head, and justifying the righteous, to give him according to his righteousness.

Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii; 1 Wafalme 8:33

When your people Israel are struck down before the enemy, because they have sinned against you; if they turn again to you, and confess your name, and pray and make supplication to you in this house:

basi, usikie huko mbinguni, ukawaachilie watu wako Israeli dhambi yao, ukawarejeze tena katika nchi uliyowapa baba zao. 1 Wafalme 8:34

then hear you in heaven, and forgive the sin of your people Israel, and bring them again to the land which you gave to their fathers.

Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa; 1 Wafalme 8:35

When the sky is shut up, and there is no rain, because they have sinned against you; if they pray toward this place, and confess your name, and turn from their sin, when you do afflict them:

basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao. 1 Wafalme 8:36

then hear in heaven, and forgive the sin of your servants, and of your people Israel, when you teach them the good way in which they should walk; and send rain on your land, which you have given to your people for an inheritance.

Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; 1 Wafalme 8:37

If there be in the land famine, if there be pestilence, if there be blasting [or] mildew, locust [or] caterpillar; if their enemy besiege them in the land of their cities; whatever plague, whatever sickness there be;

maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii; 1 Wafalme 8:38

whatever prayer and supplication be made by any man, [or] by all your people Israel, who shall know every man the plague of his own heart, and spread forth his hands toward this house:

basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote); 1 Wafalme 8:39

then hear in heaven, your dwelling-place, and forgive, and do, and render to every man according to all his ways, whose heart you know; (for you, even you only, know the hearts of all the children of men;)

ili wakuche wewe siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu. 1 Wafalme 8:40

that they may fear you all the days that they live in the land which you gave to our fathers.

Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako; 1 Wafalme 8:41

Moreover concerning the foreigner, who is not of your people Israel, when he shall come out of a far country for your name's sake

(maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii; 1 Wafalme 8:42

(for they shall hear of your great name, and of your mighty hand, and of your outstretched arm); when he shall come and pray toward this house;

basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako. 1 Wafalme 8:43

hear in heaven, your dwelling-place, and do according to all that the foreigner calls to you for; that all the peoples of the earth may know your name, to fear you, as does your people Israel, and that they may know that this house which I have built is called by my name.

Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yo yote utakayowapeleka, wakikuomba, Bwana, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 1 Wafalme 8:44

If your people go out to battle against their enemy, by whatever way you shall send them, and they pray to Yahweh toward the city which you have chosen, and toward the house which I have built for your name;

basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao. 1 Wafalme 8:45

then hear in heaven their prayer and their supplication, and maintain their cause.

Ikiwa wamekutenda dhambi, (maana hakuna mtu asiyetenda dhambi), hata ukawaghadhibikia, ukawatia katika mikono ya adui zao, wawachukue mateka mpaka nchi ya adui zao, iliyo mbali au iliyo karibu; 1 Wafalme 8:46

If they sin against you (for there is no man who doesn't sin), and you are angry with them, and deliver them to the enemy, so that they carry them away captive to the land of the enemy, far off or near;

basi, wakijirudia nafsi zao katika nchi ile watakayochukuliwa mateka, wakitubu, na kukusihi katika nchi ya hao waliowachukua mateka, wakisema, Tumekosa, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu; 1 Wafalme 8:47

yet if they shall repent themselves in the land where they are carried captive, and turn again, and make supplication to you in the land of those who carried them captive, saying, We have sinned, and have done perversely, we have dealt wickedly;

watakaporejea kwako kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya adui zao, waliowachukua mateka, wakikuomba, kwa kuikabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 1 Wafalme 8:48

if they return to you with all their heart and with all their soul in the land of their enemies, who carried them captive, and pray to you toward their land, which you gave to their fathers, the city which you have chosen, and the house which I have built for your name:

basi, uyasikie maombi yao na dua yao, huko mbinguni, makao yako, ukaitetee haki yao; 1 Wafalme 8:49

then hear you their prayer and their supplication in heaven, your dwelling-place, and maintain their cause;

ukawasamehe watu wako waliokutenda dhambi, na makosa yao yote waliyokukosa; ukawape kuonewa huruma mbele yao waliowachukua mateka, ili wapate kuwahurumia. 1 Wafalme 8:50

and forgive your people who have sinned against you, and all their transgressions in which they have transgressed against you; and give them compassion before those who carried them captive, that they may have compassion on them

Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuu ya chuma. 1 Wafalme 8:51

(for they are your people, and your inheritance, which you brought forth out of Egypt, from the midst of the furnace of iron);

Macho yako na yafumbuke, na kuielekea dua ya mtumwa wako, na dua za watu wako Israeli, ukawasikilize kila wakati watakapokulilia. 1 Wafalme 8:52

that your eyes may be open to the supplication of your servant, and to the supplication of your people Israel, to listen to them whenever they cry to you.

Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU. 1 Wafalme 8:53

For you did separate them from among all the peoples of the earth, to be your inheritance, as you spoke by Moses your servant, when you brought our fathers out of Egypt, Lord Yahweh.

Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni. 1 Wafalme 8:54

It was so, that when Solomon had made an end of praying all this prayer and supplication to Yahweh, he arose from before the altar of Yahweh, from kneeling on his knees with his hands spread forth toward heaven.

Akasimama, na kuwabariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, akasema, 1 Wafalme 8:55

He stood, and blessed all the assembly of Israel with a loud voice, saying,

Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lo lote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. 1 Wafalme 8:56

Blessed be Yahweh, who has given rest to his people Israel, according to all that he promised: there has not failed one word of all his good promise, which he promised by Moses his servant.

Bwana, Mungu wetu, na akae nasi, kama alivyokaa na baba zetu; asituache, wala asitutupe; 1 Wafalme 8:57

Yahweh our God be with us, as he was with our fathers: let him not leave us, nor forsake us;

aielekeze mioyo yetu kwake, ili tuende katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na sheria zake, na hukumu zake, alizowaamuru baba zetu. 1 Wafalme 8:58

that he may incline our hearts to him, to walk in all his ways, and to keep his commandments, and his statutes, and his ordinances, which he commanded our fathers.

Na maneno yangu haya, niliyoyaomba mbele za Bwana, na yawe karibu na Bwana, Mungu wetu, mchana na usiku, ili aitetee haki ya mtumishi wake, na haki ya watu wake Israeli, kwa kadiri ya haja zao za kila siku. 1 Wafalme 8:59

Let these my words, with which I have made supplication before Yahweh, be near to Yahweh our God day and night, that he maintain the cause of his servant, and the cause of his people Israel, as every day shall require;

Watu wote wa ulimwengu wajue ya kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine. 1 Wafalme 8:60

that all the peoples of the earth may know that Yahweh, he is God; there is none else.

Mioyo yenu na iwe kamili kwa Bwana, Mungu wetu, kuenenda katika sheria zake, na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo. 1 Wafalme 8:61

Let your heart therefore be perfect with Yahweh our God, to walk in his statutes, and to keep his commandments, as at this day.

Ndipo mfalme, na Israeli wote pamoja naye, wakatoa sadaka mbele za Bwana. 1 Wafalme 8:62

The king, and all Israel with him, offered sacrifice before Yahweh.

Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea Bwana, ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Bwana. 1 Wafalme 8:63

Solomon offered for the sacrifice of peace-offerings, which he offered to Yahweh, two and twenty thousand oxen, and one hundred twenty thousand sheep. So the king and all the children of Israel dedicated the house of Yahweh.

Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani. 1 Wafalme 8:64

The same day did the king make the middle of the court holy that was before the house of Yahweh; for there he offered the burnt offering, and the meal-offering, and the fat of the peace-offerings, because the brazen altar that was before Yahweh was too little to receive the burnt offering, and the meal-offering, and the fat of the peace-offerings.

Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za Bwana, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne. 1 Wafalme 8:65

So Solomon held the feast at that time, and all Israel with him, a great assembly, from the entrance of Hamath to the brook of Egypt, before Yahweh our God, seven days and seven days, even fourteen days.

Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake. 1 Wafalme 8:66

On the eighth day he sent the people away; and they blessed the king, and went to their tents joyful and glad of heart for all the goodness that Yahweh had shown to David his servant, and to Israel his people.