1 Wakorintho 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 9 (Swahili) 1st Corinthians 9 (English)

Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana? 1 Wakorintho 9:1

Am I not free? Am I not an apostle? Haven't I seen Jesus Christ, our Lord? Aren't you my work in the Lord?

Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana. 1 Wakorintho 9:2

If to others I am not an apostle, yet at least I am to you; for you are the seal of my apostleship in the Lord.

Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza. 1 Wakorintho 9:3

My defense to those who examine me is this.

Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa? 1 Wakorintho 9:4

Have we no right to eat and to drink?

Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa? 1 Wakorintho 9:5

Have we no right to take along a wife who is a believer, even as the rest of the apostles, and the brothers of the Lord, and Cephas?

Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi? 1 Wakorintho 9:6

Or have only Barnabas and I no right to not work?

Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? 1 Wakorintho 9:7

What soldier ever serves at his own expense? Who plants a vineyard, and doesn't eat of its fruit? Or who feeds a flock, and doesn't drink from the flock's milk?

Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo? 1 Wakorintho 9:8

Do I speak these things according to the ways of men? Or doesn't the law also say the same thing?

Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe? 1 Wakorintho 9:9

For it is written in the law of Moses, "You shall not muzzle an ox while it treads out the grain." Is it for the oxen that God cares,

Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. 1 Wakorintho 9:10

or does he say it assuredly for our sake? Yes, it was written for our sake, because he who plows ought to plow in hope, and he who threshes in hope should partake of his hope.

Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 1 Wakorintho 9:11

If we sowed to you spiritual things, is it a great thing if we reap your fleshly things?

Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 1 Wakorintho 9:12

If others partake of this right over you, don't we yet more? Nevertheless we did not use this right, but we bear all things, that we may cause no hindrance to the Gospel of Christ.

Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 1 Wakorintho 9:13

Don't you know that those who serve around sacred things eat from the things of the temple, and those who wait on the altar have their portion with the altar?

Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili. 1 Wakorintho 9:14

Even so the Lord ordained that those who proclaim the Gospel should live from the Gospel.

Lakini mimi sikutumia mambo hayo hata moja. Wala siyaandiki hayo ili iwe hivyo kwangu mimi; maana ni heri nife kuliko mtu awaye yote abatilishe huku kujisifu kwangu. 1 Wakorintho 9:15

But I have used none of these things, and I don't write these things that it may be done so in my case; for I would rather die, than that anyone should make my boasting void.

Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! 1 Wakorintho 9:16

For if I preach the Gospel, I have nothing to boast about; for necessity is laid on me; but woe is to me, if I don't preach the Gospel.

Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili. 1 Wakorintho 9:17

For if I do this of my own will, I have a reward. But if not of my own will, I have a stewardship entrusted to me.

Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. 1 Wakorintho 9:18

What then is my reward? That, when I preach the Gospel, I may present the Gospel of Christ without charge, so as not to abuse my authority in the Gospel.

Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. 1 Wakorintho 9:19

For though I was free from all, I brought myself under bondage to all, that I might gain the more.

Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. 1 Wakorintho 9:20

To the Jews I became as a Jew, that I might gain Jews; to those who are under the law, as under the law, that I might gain those who are under the law;

Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. 1 Wakorintho 9:21

to those who are without law, as without law (not being without law toward God, but under law toward Christ), that I might win those who are without law.

Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. 1 Wakorintho 9:22

To the weak I became as weak, that I might gain the weak. I have become all things to all men, that I may by all means save some.

Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine. 1 Wakorintho 9:23

Now I do this for the Gospel's sake, that I may be a joint partaker of it.

Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. 1 Wakorintho 9:24

Don't you know that those who run in a race all run, but one receives the prize? Run like that, that you may win.

Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. 1 Wakorintho 9:25

Every man who strives in the games exercises self-control in all things. Now they do it to receive a corruptible crown, but we an incorruptible.

Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 1 Wakorintho 9:26

I therefore run like that, as not uncertainly. I fight like that, as not beating the air,

bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. 1 Wakorintho 9:27

but I beat my body and bring it into submission, lest by any means, after I have preached to others, I myself should be rejected.