1 Wakorintho 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 5 (Swahili) 1st Corinthians 5 (English)

Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 1 Wakorintho 5:1

It is actually reported that there is sexual immorality among you, and such sexual immorality as is not even named among the Gentiles, that one has his father's wife.

Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 1 Wakorintho 5:2

You are puffed up, and didn't rather mourn, that he who had done this deed might be removed from among you.

Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 1 Wakorintho 5:3

For I most assuredly, as being absent in body but present in spirit, have already, as though I were present, judged him who has done this thing.

Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 1 Wakorintho 5:4

In the name of our Lord Jesus Christ, you being gathered together, and my spirit, with the power of our Lord Jesus Christ,

kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. 1 Wakorintho 5:5

are to deliver such a one to Satan for the destruction of the flesh, that the spirit may be saved in the day of the Lord Jesus.

Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? 1 Wakorintho 5:6

Your boasting is not good. Don't you know that a little yeast leavens the whole lump?

Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; 1 Wakorintho 5:7

Purge out the old yeast, that you may be a new lump, even as you are unleavened. For indeed Christ, our Passover, has been sacrificed in our place.

basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli. 1 Wakorintho 5:8

Therefore let us keep the feast, not with old yeast, neither with the yeast of malice and wickedness, but with the unleavened bread of sincerity and truth.

Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 1 Wakorintho 5:9

I wrote to you in my letter to have no company with sexual sinners;

Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 1 Wakorintho 5:10

yet not at all meaning with the sexual sinners of this world, or with the covetous and extortioners, or with idolaters; for then you would have to leave the world.

Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 1 Wakorintho 5:11

But as it is, I wrote to you not to associate with anyone who is called a brother who is a sexual sinner, or covetous, or an idolater, or a slanderer, or a drunkard, or an extortioner. Don't even eat with such a person.

Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? 1 Wakorintho 5:12

For what have I to do with also judging those who are outside? Don't you judge those who are within?

Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

1 Wakorintho 5:13

But those who are outside, God judges. "Put away the wicked man from among yourselves."