1 Wakorintho 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 11 (Swahili) 1st Corinthians 11 (English)

Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo. 1 Wakorintho 11:1

Be imitators of me, even as I also am of Christ.

Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea. 1 Wakorintho 11:2

Now I praise you, brothers, that you remember me in all things, and hold firm the traditions, even as I delivered them to you.

Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. 1 Wakorintho 11:3

But I would have you know that the head of every man is Christ, and the head of the woman is the man, and the head of Christ is God.

Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake. 1 Wakorintho 11:4

Every man praying or prophesying, having his head covered, dishonors his head.

Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. 1 Wakorintho 11:5

But every woman praying or prophesying with her head unveiled dishonors her head. For it is one and the same thing as if she were shaved.

Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe. 1 Wakorintho 11:6

For if a woman is not covered, let her also be shorn. But if it is shameful for a woman to be shorn or shaved, let her be covered.

Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 1 Wakorintho 11:7

For a man indeed ought not to have his head covered, because he is the image and glory of God, but the woman is the glory of the man.

Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. 1 Wakorintho 11:8

For man is not from woman, but woman from man;

Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. 1 Wakorintho 11:9

for neither was man created for the woman, but woman for the man.

Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika. 1 Wakorintho 11:10

For this cause the woman ought to have authority on her head, because of the angels.

Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana. 1 Wakorintho 11:11

Nevertheless, neither is the woman independent of the man, nor the man independent of the woman, in the Lord.

Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. 1 Wakorintho 11:12

For as woman came from man, so a man also comes through a woman; but all things are from God.

Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa? 1 Wakorintho 11:13

Judge for yourselves. Is it appropriate that a woman pray to God unveiled?

Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake? 1 Wakorintho 11:14

Doesn't even nature itself teach you that if a man has long hair, it is a dishonor to him?

Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi. 1 Wakorintho 11:15

But if a woman has long hair, it is a glory to her, for her hair is given to her for a covering.

Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu. 1 Wakorintho 11:16

But if any man seems to be contentious, we have no such custom, neither do God's assemblies.

Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara. 1 Wakorintho 11:17

But in giving you this command, I don't praise you, that you come together not for the better but for the worse.

Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki; 1 Wakorintho 11:18

For first of all, when you come together in the assembly, I hear that divisions exist among you, and I partly believe it.

kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu. 1 Wakorintho 11:19

For there also must be factions among you, that those who are approved may be revealed among you.

Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; 1 Wakorintho 11:20

When therefore you assemble yourselves together, it is not possible to eat the Lord's supper.

kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 1 Wakorintho 11:21

For in your eating each one takes his own supper before others. One is hungry, and another is drunken.

Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo. 1 Wakorintho 11:22

What, don't you have houses to eat and to drink in? Or do you despise God's assembly, and put them to shame who don't have? What shall I tell you? Shall I praise you? In this I don't praise you.

Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, 1 Wakorintho 11:23

For I received from the Lord that which also I delivered to you, that the Lord Jesus on the night in which he was betrayed took bread.

naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 1 Wakorintho 11:24

When he had given thanks, he broke it, and said, "Take, eat. This is my body, which is broken for you. Do this in memory of me."

Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. 1 Wakorintho 11:25

In the same way he also took the cup, after supper, saying, "This cup is the new covenant in my blood. Do this, as often as you drink, in memory of me."

Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. 1 Wakorintho 11:26

For as often as you eat this bread and drink this cup, you proclaim the Lord's death until he comes.

Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 1 Wakorintho 11:27

Therefore whoever eats this bread or drinks the Lord's cup in a manner unworthy of the Lord will be guilty of the body and the blood of the Lord.

Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. 1 Wakorintho 11:28

But let a man examine himself, and so let him eat of the bread, and drink of the cup.

Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. 1 Wakorintho 11:29

For he who eats and drinks in an unworthy manner eats and drinks judgment to himself, if he doesn't discern the Lord's body.

Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. 1 Wakorintho 11:30

For this cause many among you are weak and sickly, and not a few sleep.

Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. 1 Wakorintho 11:31

For if we discerned ourselves, we wouldn't be judged.

Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia. 1 Wakorintho 11:32

But when we are judged, we are punished by the Lord, that we may not be condemned with the world.

Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojaneni; 1 Wakorintho 11:33

Therefore, my brothers, when you come together to eat, wait one for another.

mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza. 1 Wakorintho 11:34

But if anyone is hungry, let him eat at home, lest your coming together be for judgment. The rest I will set in order whenever I come.