1 Wakorintho 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 8 (Swahili) 1st Corinthians 8 (English)

Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. 1 Wakorintho 8:1

Now concerning things sacrificed to idols: We know that we all have knowledge. Knowledge puffs up, but love builds up.

Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua. 1 Wakorintho 8:2

But if anyone thinks that he knows anything, he doesn't yet know as he ought to know.

Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye. 1 Wakorintho 8:3

But if anyone loves God, the same is known by him.

Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu. 1 Wakorintho 8:4

Therefore concerning the eating of things sacrificed to idols, we know that no idol is anything in the world, and that there is no other God but one.

Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; 1 Wakorintho 8:5

For though there are things that are called "gods," whether in the heavens or on earth; as there are many "gods" and many "lords;"

lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. 1 Wakorintho 8:6

yet to us there is one God, the Father, of whom are all things, and we for him; and one Lord, Jesus Christ, through whom are all things, and we live through him.

Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika. 1 Wakorintho 8:7

However, that knowledge isn't in all men. But some, with consciousness of the idol until now, eat as of a thing sacrificed to an idol, and their conscience, being weak, is defiled.

Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu. 1 Wakorintho 8:8

But food will not commend us to God. For neither, if we don't eat, are we the worse; nor, if we eat, are we the better.

Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu. 1 Wakorintho 8:9

But be careful that by no means does this liberty of yours become a stumbling block to the weak.

Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu? 1 Wakorintho 8:10

For if a man sees you who have knowledge sitting in an idol's temple, won't his conscience, if he is weak, be emboldened to eat things sacrificed to idols?

Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 1 Wakorintho 8:11

And through your knowledge, he who is weak perishes, the brother for whose sake Christ died.

Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo. 1 Wakorintho 8:12

Thus, sinning against the brothers, and wounding their conscience when it is weak, you sin against Christ.

Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu. 1 Wakorintho 8:13

Therefore, if food causes my brother to stumble, I will eat no meat forevermore, that I don't cause my brother to stumble.