1 Wakorintho 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 12 (Swahili) 1st Corinthians 12 (English)

Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu. 1 Wakorintho 12:1

Now concerning spiritual things, brothers, I don't want you to be ignorant.

Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa. 1 Wakorintho 12:2

You know that when you were heathen{or Gentiles}, you were led away to those mute idols, however you might be led.

Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. 1 Wakorintho 12:3

Therefore I make known to you that no man speaking by God's Spirit says, "Jesus is accursed." No one can say, "Jesus is Lord," but by the Holy Spirit.

Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 1 Wakorintho 12:4

Now there are various kinds of gifts, but the same Spirit.

Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 1 Wakorintho 12:5

There are various kinds of service, and the same Lord.

Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. 1 Wakorintho 12:6

There are various kinds of workings, but the same God, who works all things in all.

Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 1 Wakorintho 12:7

But to each one is given the manifestation of the Spirit for the profit of all.

Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 1 Wakorintho 12:8

For to one is given through the Spirit the word of wisdom, and to another the word of knowledge, according to the same Spirit;

mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 1 Wakorintho 12:9

to another faith, by the same Spirit; and to another gifts of healings, by the same Spirit;

na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; 1 Wakorintho 12:10

and to another workings of miracles; and to another prophecy; and to another discerning of spirits; to another different kinds of languages; and to another the interpretation of languages.

lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 1 Wakorintho 12:11

But the one and the same Spirit works all of these, distributing to each one separately as he desires.

Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 1 Wakorintho 12:12

For as the body is one, and has many members, and all the members of the body, being many, are one body; so also is Christ.

Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 1 Wakorintho 12:13

For in one Spirit we were all baptized into one body, whether Jews or Greeks, whether bond or free; and were all given to drink into one Spirit.

Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 1 Wakorintho 12:14

For the body is not one member, but many.

Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? 1 Wakorintho 12:15

If the foot would say, "Because I'm not the hand, I'm not part of the body," it is not therefore not part of the body.

Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 1 Wakorintho 12:16

If the ear would say, "Because I'm not the eye, I'm not part of the body," it's not therefore not part of the body.

Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 1 Wakorintho 12:17

If the whole body were an eye, where would the hearing be? If the whole were hearing, where would the smelling be?

Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 1 Wakorintho 12:18

But now God has set the members, each one of them, in the body, just as he desired.

Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 1 Wakorintho 12:19

If they were all one member, where would the body be?

Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 1 Wakorintho 12:20

But now they are many members, but one body.

Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 1 Wakorintho 12:21

The eye can't tell the hand, "I have no need for you," or again the head to the feet, "I have no need for you."

Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 1 Wakorintho 12:22

No, much rather, those members of the body which seem to be weaker are necessary.

Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 1 Wakorintho 12:23

Those parts of the body which we think to be less honorable, on those we bestow more abundant honor; and our unpresentable parts have more abundant propriety;

Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; 1 Wakorintho 12:24

whereas our presentable parts have no such need. But God composed the body together, giving more abundant honor to the inferior part,

ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 1 Wakorintho 12:25

that there should be no division in the body, but that the members should have the same care for one another.

Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. 1 Wakorintho 12:26

When one member suffers, all the members suffer with it. Or when one member is honored, all the members rejoice with it.

Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 1 Wakorintho 12:27

Now you are the body of Christ, and members individually.

Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. 1 Wakorintho 12:28

God has set some in the assembly: first apostles, second prophets, third teachers, then miracle workers, then gifts of healings, helps, governments, and various kinds of languages.

Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? 1 Wakorintho 12:29

Are all apostles? Are all prophets? Are all teachers? Are all miracle workers?

Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? 1 Wakorintho 12:30

Do all have gifts of healings? Do all speak with various languages? Do all interpret?

Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora. 1 Wakorintho 12:31

But earnestly desire the best gifts. Moreover, I show a most excellent way to you.