1 Wakorintho 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wakorintho 15 (Swahili) 1st Corinthians 15 (English)

Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 1 Wakorintho 15:1

Now I declare to you, brothers, the Gospel which I preached to you, which also you received, in which you also stand,

na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 1 Wakorintho 15:2

by which also you are saved, if you hold firmly the word which I preached to you--unless you believed in vain.

Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 1 Wakorintho 15:3

For I delivered to you first of all that which I also received: that Christ died for our sins according to the Scriptures,

na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 1 Wakorintho 15:4

that he was buried, that he was raised on the third day according to the Scriptures,

na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 1 Wakorintho 15:5

and that he appeared to Cephas, then to the twelve.

baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 1 Wakorintho 15:6

Then he appeared to over five hundred brothers at once, most of whom remain until now, but some have also fallen asleep.

baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 1 Wakorintho 15:7

Then he appeared to James, then to all the apostles,

na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 1 Wakorintho 15:8

and last of all, as to the child born at the wrong time, he appeared to me also.

Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 1 Wakorintho 15:9

For I am the least of the apostles, who is not worthy to be called an apostle, because I persecuted the assembly of God.

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 1 Wakorintho 15:10

But by the grace of God I am what I am. His grace which was bestowed on me was not futile, but I worked more than all of them; yet not I, but the grace of God which was with me.

Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. 1 Wakorintho 15:11

Whether then it is I or they, so we preach, and so you believed.

Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 1 Wakorintho 15:12

Now if Christ is preached, that he has been raised from the dead, how do some among you say that there is no resurrection of the dead?

Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 1 Wakorintho 15:13

But if there is no resurrection of the dead, neither has Christ been raised.

tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 1 Wakorintho 15:14

If Christ has not been raised, then our preaching is in vain, and your faith also is in vain.

Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 1 Wakorintho 15:15

Yes, we are found false witnesses of God, because we testified about God that he raised up Christ, whom he didn't raise up, if it is so that the dead are not raised.

Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 1 Wakorintho 15:16

For if the dead aren't raised, neither has Christ been raised.

Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 1 Wakorintho 15:17

If Christ has not been raised, your faith is vain; you are still in your sins.

Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 1 Wakorintho 15:18

Then they also who are fallen asleep in Christ have perished.

Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. 1 Wakorintho 15:19

If we have only hoped in Christ in this life, we are of all men most pitiable.

Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 1 Wakorintho 15:20

But now Christ has been raised from the dead. He became the first fruits of those who are asleep.

Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 1 Wakorintho 15:21

For since death came by man, the resurrection of the dead also came by man.

Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 1 Wakorintho 15:22

For as in Adam all die, so also in Christ all will be made alive.

Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 1 Wakorintho 15:23

But each in his own order: Christ the first fruits, then those who are Christ's, at his coming.

Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 1 Wakorintho 15:24

Then the end comes, when he will deliver up the Kingdom to God, even the Father; when he will have abolished all rule and all authority and power.

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 1 Wakorintho 15:25

For he must reign until he has put all his enemies under his feet.

Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 1 Wakorintho 15:26

The last enemy that will be abolished is death.

Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 1 Wakorintho 15:27

For, "He put all things in subjection under his feet." But when he says, "All things are put in subjection," it is evident that he is excepted who subjected all things to him.

Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote. 1 Wakorintho 15:28

When all things have been subjected to him, then the Son will also himself be subjected to him who subjected all things to him, that God may be all in all.

Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao? 1 Wakorintho 15:29

Or else what will they do who are baptized for the dead? If the dead aren't raised at all, why then are they baptized for the dead?

Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? 1 Wakorintho 15:30

Why do we also stand in jeopardy every hour?

Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku. 1 Wakorintho 15:31

I affirm, by the boasting in you which I have in Christ Jesus our Lord, I die daily.

Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa. 1 Wakorintho 15:32

If I fought with animals at Ephesus for human purposes, what does it profit me? If the dead are not raised, then "let us eat and drink, for tomorrow we die."

Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. 1 Wakorintho 15:33

Don't be deceived! "Evil companionships corrupt good morals."

Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe. 1 Wakorintho 15:34

Wake up righteously, and don't sin, for some have no knowledge of God. I say this to your shame.

Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? 1 Wakorintho 15:35

But someone will say, "How are the dead raised?" and, "With what kind of body do they come?"

Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; 1 Wakorintho 15:36

You foolish one, that which you yourself sow is not made alive unless it dies.

nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo; 1 Wakorintho 15:37

That which you sow, you don't sow the body that will be, but a bare grain, maybe of wheat, or of some other kind.

lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake. 1 Wakorintho 15:38

But God gives it a body even as it pleased him, and to each seed a body of its own.

Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki. 1 Wakorintho 15:39

All flesh is not the same flesh, but there is one flesh of men, another flesh of animals, another of fish, and another of birds.

Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. 1 Wakorintho 15:40

There are also celestial bodies, and terrestrial bodies; but the glory of the celestial differs from that of the terrestrial.

Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 1 Wakorintho 15:41

There is one glory of the sun, another glory of the moon, and another glory of the stars; for one star differs from another star in glory.

Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 1 Wakorintho 15:42

So also is the resurrection of the dead. It is sown in corruption; it is raised in incorruption.

hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 1 Wakorintho 15:43

It is sown in dishonor; it is raised in glory. It is sown in weakness; it is raised in power.

hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 1 Wakorintho 15:44

It is sown a natural body; it is raised a spiritual body. There is a natural body and there is also a spiritual body.

Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 1 Wakorintho 15:45

So also it is written, "The first man, Adam, became a living soul." The last Adam became a life-giving spirit.

Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 1 Wakorintho 15:46

However that which is spiritual isn't first, but that which is natural, then that which is spiritual.

Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 1 Wakorintho 15:47

The first man is of the earth, made of dust. The second man is the Lord from heaven.

Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 1 Wakorintho 15:48

As is the one made of dust, such are those who are also made of dust; and as is the heavenly, such are they also that are heavenly.

Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 1 Wakorintho 15:49

As we have borne the image of those made of dust, let's{NU, TR read "we will" instead of "let's"} also bear the image of the heavenly.

Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 1 Wakorintho 15:50

Now I say this, brothers,{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} that flesh and blood can't inherit the Kingdom of God; neither does corruption inherit incorruption.

Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 1 Wakorintho 15:51

Behold, I tell you a mystery. We will not all sleep, but we will all be changed,

kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 1 Wakorintho 15:52

in a moment, in the twinkling of an eye, at the last trumpet. For the trumpet will sound, and the dead will be raised incorruptible, and we will be changed.

Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 1 Wakorintho 15:53

For this corruptible must put on incorruption, and this mortal must put on immortality.

Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. 1 Wakorintho 15:54

But when this corruptible will have put on incorruption, and this mortal will have put on immortality, then what is written will happen: "Death is swallowed up in victory."

Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 1 Wakorintho 15:55

"Death, where is your sting? Hades, where is your victory?"

Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 1 Wakorintho 15:56

The sting of death is sin, and the power of sin is the law.

Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 1 Wakorintho 15:57

But thanks be to God, who gives us the victory through our Lord Jesus Christ.

Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana. 1 Wakorintho 15:58

Therefore, my beloved brothers, be steadfast, immovable, always abounding in the Lord's work, because you know that your labor is not in vain in the Lord.