Sifa Lyrics

Niliye Msafiri by PaPi Clever & Dorcas cover art

PaPi Clever & Dorcas - Niliye Msafiri Lyrics

Artist:
PaPi Clever & Dorcas
Album:
Ninakumbuka Sayuni
Official Release:
14 Nov 2023

Lyrics

Niliye msafiri, mgeni duniani
Sioni kwangu hapa, ni huko ju’ mbinguni
Ninatamani nami kukaa siku zote
Pamoja naye Baba katika utukufu


Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku


Mwokozi yuko huko, rafiki yangu mwema
Aliyenikomboa na ku’chukua dhambi
Na hata nikiona furaha siku zote
Ningali natamani makao ya mbinguni


Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku


Na nikipewa huku vipawa vya thamani
Na wakiimba nyimbo za kunifurahisha
Rafiki wangu wote wakipendeza mimi
Ningali natamani makao ya mbinguni
Ningali natamani makao ya mbinguni
Ningali natamani makao ya mbinguni


Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku


Upesi nitaona kifiko cha mbinguni
Mwokozi wangu Yesu atanikaribisha
Na huko nitaona nilivyotumaini
Kinubi nita’piga kumshukuru Yesu
Na huko nitaona nilivyotumaini
Kinubi nita’piga kumshukuru Yesu
Kinubi nita’piga kumshukuru Yesu


Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku
Kwangu mbinguni, kwangu, uzuri
Wa binguni wapita yote huku


Video