Goodluck Gozbert

Kama Si Wewe Lyrics

Na wala sio sababu ya jina langu 
Wala sio sababu nina-vaa 
Najua sio sababu ya sadaka zangu 
Oh, maana ndio ninashangaa 
Nilijua kwamba nimeshapoteza nafasi 
Mimi ni nani kwani? Nakosa neno kusema 
Unisamehe, sikujua unanipenda hivi 
Umefanya bure, sawa upendavyo 
Umeruhusu niwe, vile upendavyo 

Refrain:
Nitakushukuru tu, kwa neema 
Asante tu, kwa wema 
Nitakushukuru tu, kwa neema 
Asante tu, kwa wema 
Maana kama si wewe 
Kama si wewe ningekuwa wapi? 
Wacha machozi yanitirike tu 
Wacha kilio nikulilie Mungu 

Natafuta cha kunitenga nawe, bado sijaona 
Nilishakatwakatwa moyo na kupondwa na wanadamu 
Wao wataniambia nini, nikiwa nawe? 
Leo wataniambia nini, nikiwa nawe? 
Pesa huitwa sabuni, ila maji ni wewe 
Unioshe Bwana, nitakase  

Nitakushukuru tu, kwa neema 
Asante tu, kwa wema 
Maana kama si wewe 
Kama si wewe ningekuwa wapi? 
Wacha machozi yanitirike tu 
Wacha kilio nikulilie Mungu 


Kama Si Wewe Video