Narudisha

'Audio Mp3 Preview Courtesy of iTunes listen on Itunes Music View on amazon

Abudiwa bwana,tukuka bwana
heshimika bwana,tukuka milele
wewe ni mungu hakuna kama wewe
bwana ,unayotenda hakuna mwingine
awezaye tenda,

unarudishia watu miaka yao,waliopoteza
unarudishia watu miaka yao iliyoliwa na nzige
ulimrudishia ayubu miaka yote aliopoteza
mali yake watoto wote bwana ulirudisha
tena mara dufu,
bwana ulirudisha,nami najua nitarudishiwa
miaka yangu nitarudishiwa,
iliyoliwa na nzige,nitarudisha
eeeeieee miaka yangu,
iliyoliwa na nzige,

narudisha narudisha
miaka yangu,iliyoliwa na nzige,
narudisha kwa jina la yesu
miaka yangu,iliyoliwa na nzige,
narudisha kwa jina la yesu

Nzige wamekula amani ya wengi
nzige wameharibu afya ya wengi mno
angalia imebaki mifupa mikavu
tazama imebaki mifupa mikavu
lakini kuna tumaini bwana atarudisha,
amani itarudishwa,afya itarudishwa
biashara itarudishwa,furaha inarudishwa
waliopakwa matope,bwana anasafisha
walioshushwa chini,bwana anainua
ata mti ukikatwa,utachipuka tena
waliopoteza maono yao,jipe moyo
bwana anarudisha,kwa jina la yesu

Narudisha narudisha
miaka yangu,iliyoliwa na nzige,
narudisha kwa jina la yesu
miaka yangu,iliyoliwa na nzige,
narudisha kwa jina la yesu

@ Gloria Muliro - NarudishaShare:
0 Comments

Comments / Song Reviews

Share your understanding & meaning of this song


Gloria Muliro

@gloria-muliro

Bio

View all songs, albums & biography of Gloria Muliro

View Profile

Bible Verses for Narudisha

Deuteronomy 30 : 3

ndipo Bwana, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia Bwana, Mungu wako.

Job 42 : 12

Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda wake elfu.

Jeremiah 24 : 7

Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni Bwana; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

Joel 2 : 25

Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

Mp3 Songs & Download from iTunes

listen on Itunes Music

Sifa Lyrics

Social Links