Nehemia 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 5 (Swahili) Nehemiah 5 (English)

Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi. Nehemia 5:1

Then there arose a great cry of the people and of their wives against their brothers the Jews.

Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi. Nehemia 5:2

For there were that said, We, our sons and our daughters, are many: let us get grain, that we may eat and live.

Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa. Nehemia 5:3

Some also there were that said, We are mortgaging our fields, and our vineyards, and our houses: let us get grain, because of the dearth.

Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu. Nehemia 5:4

There were also that said, We have borrowed money for the king's tribute [on] our fields and our vineyards.

Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu. Nehemia 5:5

Yet now our flesh is as the flesh of our brothers, our children as their children: and, behold, we bring into bondage our sons and our daughters to be servants, and some of our daughters are brought into bondage [already]: neither is it in our power to help it; for other men have our fields and our vineyards.

Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. Nehemia 5:6

I was very angry when I heard their cry and these words.

Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na mashehe, nikawaambia, Mnatoza watu riba, kila mtu ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kushindana nao. Nehemia 5:7

Then I consulted with myself, and contended with the nobles and the rulers, and said to them, You exact usury, everyone of his brother. I held a great assembly against them.

Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lo lote. Nehemia 5:8

I said to them, We after our ability have redeemed our brothers the Jews, that were sold to the nations; and would you even sell your brothers, and should they be sold to us? Then held they their peace, and found never a word.

Tena nalisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu? Nehemia 5:9

Also I said, The thing that you do is not good: ought you not to walk in the fear of our God, because of the reproach of the nations our enemies?

Na mimi pia, na ndugu zangu, na watumishi wangu, twawakopesha fedha na ngano ili kupata faida? Tafadhali na tuliache jambo hili la riba. Nehemia 5:10

I likewise, my brothers and my servants, do lend them money and grain. Please let us leave off this usury.

Naomba, warudishieni leo hivi mashamba yao, na mashamba yao ya mizabibu, na mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao, na lile fungu la mia la fedha, na la ngano, na la divai, na la mafuta, mnalowatoza. Nehemia 5:11

Please restore to them, even this day, their fields, their vineyards, their olive groves, and their houses, also the hundredth part of the money, and of the grain, the new wine, and the oil, that you exact of them.

Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama ahadi hiyo. Nehemia 5:12

Then said they, We will restore them, and will require nothing of them; so will we do, even as you say. Then I called the priests, and took an oath of them, that they would do according to this promise.

Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana. Nao watu wakafanya kama ahadi hiyo. Nehemia 5:13

Also I shook out my lap, and said, So God shake out every man from his house, and from his labor, that doesn't perform this promise; even thus be he shaken out, and emptied. All the assembly said, Amen, and praised Yahweh. The people did according to this promise.

Tena tangu wakati huo nilipowekwa kuwa liwali wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini hata mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme, yaani, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula cha liwali. Nehemia 5:14

Moreover from the time that I was appointed to be their governor in the land of Judah, from the twentieth year even to the two and thirtieth year of Artaxerxes the king, [that is], twelve years, I and my brothers have not eaten the bread of the governor.

Lakini maliwali wa kwanza walionitangulia, wakawalemea watu, wakawatwalia chakula na mvinyo, zaidi ya shekeli arobaini za fedha; tena watumwa wao nao wakatawala juu ya watu; lakini mimi sikufanya hivyo, kwa kuwa nalimcha Mungu. Nehemia 5:15

But the former governors who were before me were chargeable to the people, and took of them bread and wine, besides forty shekels of silver; yes, even their servants bore rule over the people: but I didn't do so, because of the fear of God.

Naam, hata kazi ya ukuta huu tena nikaishika sana, wala hatukununua mashamba; na watumishi wangu wote wakakusanyika huko kazini. Nehemia 5:16

Yes, also I continued in the work of this wall, neither bought we any land: and all my servants were gathered there to the work.

Pamoja na hayo wakawako mezani pangu, katika Wayahudi na mashehe, watu mia na hamsini, zaidi ya wale waliotujia kutoka kwa makafiri waliotuzunguka. Nehemia 5:17

Moreover there were at my table, of the Jews and the rulers, one hundred fifty men, besides those who came to us from among the nations that were round about us.

Basi, maandalio yaliyoandaliwa kwa siku moja yalikuwa ng'ombe mmoja, na kondoo wazuri sita; tena nikaandaliwa kuku, na mara moja katika siku kumi akiba ya mvinyo ya namna zote; wala kwa hayo yote sikukidai chakula cha liwali, kwa kuwa utumwa ulikuwa mzito juu ya watu hao. Nehemia 5:18

Now that which was prepared for one day was one ox and six choice sheep; also fowls were prepared for me, and once in ten days store of all sorts of wine: yet for all this I didn't demand the bread of the governor, because the bondage was heavy on this people.

Unikumbukie, Ee Mungu wangu, kwa mema, yote niliyowafanyia watu hawa. Nehemia 5:19

Remember to me, my God, for good, all that I have done for this people.