Nehemia 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 13 (Swahili) Nehemiah 13 (English)

Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele; Nehemia 13:1

On that day they read in the book of Moses in the audience of the people; and therein was found written, that an Ammonite and a Moabite should not enter into the assembly of God forever,

kwa sababu hawakuwalaki wana wa Israeli kwa chakula na maji, bali walimwajiri Balaamu juu yao ili awalaani; lakini Mungu aliigeuza ile laana kuwa baraka. Nehemia 13:2

because they didn't meet the children of Israel with bread and with water, but hired Balaam against them, to curse them: however our God turned the curse into a blessing.

Ikawa walipoisikia torati, wakawatenga Israeli na umati wa watu waliochanganyika nao. Nehemia 13:3

It came to pass, when they had heard the law, that they separated from Israel all the mixed multitude.

Na kabla ya hayo, Eliashibu, kuhani, aliyewekwa avisimamie vyumba vya nyumba ya Mungu wetu, kwa kuwa alikuwa karibu yake Tobia, Nehemia 13:4

Now before this, Eliashib the priest, who was appointed over the chambers of the house of our God, being allied to Tobiah,

alikuwa amemtengenezea chumba kikubwa, hapo walipoweka zamani sadaka za unga, na ubani, na vyombo, na zaka za nafaka, na divai, na mafuta, walivyoamriwa kuwapa Walawi, na waimbaji, na mabawabu; tena sadaka za kuinuliwa zilizokuwa za makuhani. Nehemia 13:5

had prepared for him a great chamber, where before they laid the meal-offerings, the frankincense, and the vessels, and the tithes of the grain, the new wine, and the oil, which were given by commandment to the Levites, and the singers, and the porters; and the heave-offerings for the priests.

Lakini wakati huo wote mimi sikuwako huko Yerusalemu; maana katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta, mfalme wa Babeli, nalimrudia mfalme; na baada ya siku kadha wa kadha nikaomba ruhusa tena kwa mfalme. Nehemia 13:6

But in all this [time] I was not at Jerusalem; for in the two and thirtieth year of Artaxerxes king of Babylon I went to the king: and after certain days asked I leave of the king,

Nami nikaja Yerusalemu, nikafahamu yale mabaya, ambayo Eliashibu ameyatenda kwa ajili ya Tobia, kwa kumtengenezea chumba katika nyua za nyumba ya Mungu. Nehemia 13:7

and I came to Jerusalem, and understood the evil that Eliashib had done for Tobiah, in preparing him a chamber in the courts of the house of God.

Nami nikasikitika sana; basi nikavitupa nje vyombo vyote vya Tobia vitoke humo chumbani. Nehemia 13:8

It grieved me sore: therefore I cast forth all the household stuff of Tobiah out of the chamber.

Kisha nikatoa amri, nao wakavisafisha vyumba; nami nikavirudisha humo vyombo vya nyumba ya Mungu, pamoja na sadaka za unga na ubani. Nehemia 13:9

Then I commanded, and they cleansed the chambers: and there brought I again the vessels of the house of God, with the meal-offerings and the frankincense.

Tena nikaona ya kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; basi wamekimbia Walawi na waimbaji, waliofanya kazi, kila mtu shambani kwake. Nehemia 13:10

I perceived that the portions of the Levites had not been given them; so that the Levites and the singers, who did the work, were fled everyone to his field.

Ndipo nikagombana na mashehe, nikasema, Mbona nyumba ya Mungu imeachwa? Kisha nikawakusanya, nikawaweka mahali pao. Nehemia 13:11

Then contended I with the rulers, and said, Why is the house of God forsaken? I gathered them together, and set them in their place.

Ndipo Yuda wote walipoleta zaka za nafaka, na mvinyo, na mafuta, kwenye hazina. Nehemia 13:12

Then brought all Judah the tithe of the grain and the new wine and the oil to the treasuries.

Nami nikawaweka watunza hazina juu ya hazina, yaani, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na wa Walawi, Pedaya; na wa pili wao alikuwa Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania; kwani walihesabiwa kuwa waaminifu, na ilikuwa juu yao kuwagawia ndugu zao. Nehemia 13:13

I made treasurers over the treasuries, Shelemiah the priest, and Zadok the scribe, and of the Levites, Pedaiah: and next to them was Hanan the son of Zaccur, the son of Mattaniah; for they were counted faithful, and their business was to distribute to their brothers.

Unikumbukie hayo, Ee Mungu wangu, wala usifute fadhili zangu nilizozitenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, na kwa taratibu zake. Nehemia 13:14

Remember me, my God, concerning this, and don't wipe out my good deeds that I have done for the house of my God, and for the observances of it.

Siku hizo naliona katika Yuda watu wengine waliokanyaga mashinikizo ya mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu, na tini, na namna zote za mizigo, waliyoileta Yerusalemu, siku ya sabato; nami nikashuhudia juu yao siku ile waliyouza vyakula. Nehemia 13:15

In those days saw I in Judah some men treading wine-presses on the Sabbath, and bringing in sheaves, and lading donkeys [therewith]; as also wine, grapes, and figs, and all manner of burdens, which they brought into Jerusalem on the Sabbath day: and I testified [against them] in the day in which they sold food.

Tena wakakaa humo watu wa Tiro, walioleta samaki, na biashara za kila namna, wakawauzia wana wa Yuda siku ya sabato, na mumo humo Yerusalemu. Nehemia 13:16

There lived men of Tyre also therein, who brought in fish, and all manner of wares, and sold on the Sabbath to the children of Judah, and in Jerusalem.

Ndipo nikagombana na wakuu wa Yuda, nikawaambia, Ni neno baya gani hili mnalofanya ninyi, na kuinajisi siku ya sabato? Nehemia 13:17

Then I contended with the nobles of Judah, and said to them, What evil thing is this that you do, and profane the Sabbath day?

Je! Sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! Hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mwazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi sabato! Nehemia 13:18

Didn't your fathers do thus, and did not our God bring all this evil on us, and on this city? yet you bring more wrath on Israel by profaning the Sabbath.

Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, naliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wo wote siku ya sabato. Nehemia 13:19

It came to pass that, when the gates of Jerusalem began to be dark before the Sabbath, I commanded that the doors should be shut, and commanded that they should not be opened until after the Sabbath: and some of my servants set I over the gates, that there should no burden be brought in on the Sabbath day.

Basi wenye biashara na wachuuzi wa bidhaa za kila namna wakalala nje ya Yerusalemu mara mbili tatu. Nehemia 13:20

So the merchants and sellers of all kind of wares lodged outside of Jerusalem once or twice.

Ndipo nikawashuhudia, nikawaambia, Mbona mwalala mbele ya ukuta? Mkitenda hivi tena, nitawakamata. Tangu wakati ule hawakuja tena siku ya sabato. Nehemia 13:21

Then I testified against them, and said to them, Why lodge you about the wall? if you do so again, I will lay hands on you. From that time forth came they no more on the Sabbath.

Kisha nikawaamuru Walawi wajitakase, nao waje kuyalinda malango, ili kuitakasa siku ya sabato. Unikumbukie hayo nayo, Ee Mungu wangu, ukaniachilie sawasawa na wingi wa rehema zako. Nehemia 13:22

I commanded the Levites that they should purify themselves, and that they should come and keep the gates, to sanctify the Sabbath day. Remember to me, my God, this also, and spare me according to the greatness of your loving kindness.

Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; Nehemia 13:23

In those days also saw I the Jews who had married women of Ashdod, of Ammon, [and] of Moab:

na watoto wao wakanena nusu kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kunena kwa Kiyahudi, bali kwa lugha ya watu hao mojawapo. Nehemia 13:24

and their children spoke half in the speech of Ashdod, and could not speak in the Jews' language, but according to the language of each people.

Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. Nehemia 13:25

I contended with them, and cursed them, and struck certain of them, and plucked off their hair, and made them swear by God, [saying], You shall not give your daughters to their sons, nor take their daughters for your sons, or for yourselves.

Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye. Nehemia 13:26

Did not Solomon king of Israel sin by these things? yet among many nations was there no king like him, and he was beloved of his God, and God made him king over all Israel: nevertheless even him did foreign women cause to sin.

Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumhalifu Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni? Nehemia 13:27

Shall we then listen to you to do all this great evil, to trespass against our God in marrying foreign women?

Na mwana mmoja wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe Sanbalati, Mhoroni, basi nikamfukuza kwangu. Nehemia 13:28

One of the sons of Joiada, the son of Eliashib the high priest, was son-in-law to Sanballat the Horonite: therefore I chased him from me.

Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi. Nehemia 13:29

Remember them, my God, because they have defiled the priesthood, and the covenant of the priesthood, and of the Levites.

Hivyo nikawatakasa na kila kitu kigeni, nami nikawaagizia zamu makuhani na Walawi, kila mtu kazini mwake; Nehemia 13:30

Thus cleansed I them from all foreigners, and appointed charges for the priests and for the Levites, everyone in his work;

na matoleo ya kuni nyakati zilizoamriwa, na malimbuko. Nikumbuke, Ee Mungu wangu, ili unitendee mema. Nehemia 13:31

and for the wood-offering, at times appointed, and for the first fruits. Remember me, my God, for good.