Nehemia 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 3 (Swahili) Nehemiah 3 (English)

Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli. Nehemia 3:1

Then Eliashib the high priest rose up with his brothers the priests, and they built the sheep gate; they sanctified it, and set up the doors of it; even to the tower of Hammeah they sanctified it, to the tower of Hananel.

Na baada yao wakajenga watu wa Yeriko. Na baada yao akajenga Zakuri, mwana wa Imri. Nehemia 3:2

Next to him built the men of Jericho. Next to them built Zaccur the son of Imri.

Na lango la samaki wakalijenga wana wa Senaa; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. Nehemia 3:3

The fish gate did the sons of Hassenaah build; they laid the beams of it, and set up the doors of it, the bolts of it, and the bars of it.

Na baada yao akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi. Na baada yao akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli. Na baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Baana. Nehemia 3:4

Next to them repaired Meremoth the son of Uriah, the son of Hakkoz. Next to them repaired Meshullam the son of Berechiah, the son of Meshezabel. Next to them repaired Zadok the son of Baana.

Na baada yao wakafanyiza Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao. Nehemia 3:5

Next to them the Tekoites repaired; but their nobles didn't put their necks to the work of their lord.

Na lango la kale wakalifanyiza Yoyada, mwana wa Pasea, na Meshulamu, mwana wa Besodeya; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. Nehemia 3:6

The old gate repaired Joiada the son of Paseah and Meshullam the son of Besodeiah; they laid the beams of it, and set up the doors of it, and the bolts of it, and the bars of it.

Na baada yao wakafanyiza Melatia, Mgibeoni, na Yadoni, Mmeronothi, watu wa Gibeoni, na wa Mispa, raia wa kiti cha enzi cha liwali wa ng'ambo ya Mto. Nehemia 3:7

Next to them repaired Melatiah the Gibeonite, and Jadon the Meronothite, the men of Gibeon, and of Mizpah, [that appertained] to the throne of the governor beyond the River.

Na baada yao akafanyiza Uzieli, mwana wa Harhaya, mmoja wa mafundi wa dhahabu. Na baada yake akafanyiza Hanania, mmoja wa mafundi wa manukato, nao wakaujengea Yerusalemu buruji mpaka ule ukuta mpana. Nehemia 3:8

Next to him repaired Uzziel the son of Harhaiah, goldsmiths. Next to him repaired Hananiah one of the perfumers, and they fortified Jerusalem even to the broad wall.

Na baada yao akafanyiza Refaya, mwana wa Huri, akida wa nusu ya Yerusalemu. Nehemia 3:9

Next to them repaired Rephaiah the son of Hur, the ruler of half the district of Jerusalem.

Na baada yao akafanyiza Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akafanyiza Hatushi, mwana wa Hashabneya. Nehemia 3:10

Next to them repaired Jedaiah the son of Harumaph, over against his house. Next to him repaired Hattush the son of Hashabneiah.

Malkiya, mwana wa Harimu, na Hashubu, mwana wa Pahath-moabu, wakafanyiza sehemu nyingine, na mnara wa tanuu. Nehemia 3:11

Malchijah the son of Harim, and Hasshub the son of Pahath-moab, repaired another portion, and the tower of the furnaces.

Na baada yake akafanyiza Shalumu, mwana wa Haloheshi, akida wa nusu ya Yerusalemu, yeye na binti zake. Nehemia 3:12

Next to him repaired Shallum the son of Hallohesh, the ruler of half the district of Jerusalem, he and his daughters.

Lango la bondeni wakalifanyiza Hanuni, nao wakaao Zanoa; wakalijenga, wakaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuta wa dhiraa elfu mpaka lango la jaa. Nehemia 3:13

The valley gate repaired Hanun, and the inhabitants of Zanoah; they built it, and set up the doors of it, the bolts of it, and the bars of it, and one thousand cubits of the wall to the dung gate.

Na lango la jaa akalifanyiza Malkiya, mwana wa Rekabu, akida wa mtaa wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake. Nehemia 3:14

The dung gate repaired Malchijah the son of Rechab, the ruler of the district of Beth Haccherem; he built it, and set up the doors of it, the bolts of it, and the bars of it.

Na lango la chemchemi akalifanyiza Shalumu, mwana wa Kolhoze, akida wa mtaa wa Mispa; akalijenga na kulifunika, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi. Nehemia 3:15

The spring gate repaired Shallun the son of Colhozeh, the ruler of the district of Mizpah; he built it, and covered it, and set up the doors of it, the bolts of it, and the bars of it, and the wall of the pool of Shelah by the king's garden, even to the stairs that go down from the city of David.

Baada yake akafanyiza Nehemia, mwana wa Azbuki, akida wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya mashujaa. Nehemia 3:16

After him repaired Nehemiah the son of Azbuk, the ruler of half the district of Beth Zur, to the place over against the tombs of David, and to the pool that was made, and to the house of the mighty men.

Baada yake wakafanyiza Walawi, Rehumi, mwana wa Bani. Baada yake akafanyiza Hashabia, akida wa nusu ya mtaa wa Keila, kwa mtaa wake. Nehemia 3:17

After him repaired the Levites, Rehum the son of Bani. Next to him repaired Hashabiah, the ruler of half the district of Keilah, for his district.

Baada yake wakafanyiza ndugu zao, Binui, mwana wa Henadadi, akida wa nusu ya mtaa wa Keila. Nehemia 3:18

After him repaired their brothers, Bavvai the son of Henadad, the ruler of half the district of Keilah.

Na baada yake akafanyiza Ezeri, mwana wa Yeshua, akida wa Mispa, sehemu nyingine, kupaelekea penye kupanda kwa ghala ya silaha, ukuta ugeukapo. Nehemia 3:19

Next to him repaired Ezer the son of Jeshua, the ruler of Mizpah, another portion, over against the ascent to the armory at the turning [of the wall].

Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akafanyiza kwa bidii sehemu nyingine, toka ugeukapo ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu. Nehemia 3:20

After him Baruch the son of Zabbai earnestly repaired another portion, from the turning [of the wall] to the door of the house of Eliashib the high priest.

Baada yake akafanyiza Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu. Nehemia 3:21

After him repaired Meremoth the son of Uriah the son of Hakkoz another portion, from the door of the house of Eliashib even to the end of the house of Eliashib.

Na baada yake wakafanyiza makuhani, watu wa Uwandani. Nehemia 3:22

After him repaired the priests, the men of the Plain.

Baada yao wakafanyiza Benyamini na Hashubu, kuielekea nyumba yao. Baada yao akafanyiza Azaria, mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, kando ya nyumba yake. Nehemia 3:23

After them repaired Benjamin and Hasshub over against their house. After them repaired Azariah the son of Maaseiah the son of Ananiah beside his own house.

Baada yake akafanyiza Binui, mwana wa Henadadi, sehemu nyingine, toka nyumba ya Azaria mpaka ugeukapo ukuu, na mpaka pembeni. Nehemia 3:24

After him repaired Binnui the son of Henadad another portion, from the house of Azariah to the turning [of the wall], and to the corner.

Baada yake akafanyiza Palali, mwana wa Uzai, kuelekea ugeukapo ukuta, nao mnara utokezao penye nyumba ya juu ya kifalme, iliyopo karibu na uwanda wa walinzi. Baada yake akafanyiza Pedaya, mwana wa Paroshi, Nehemia 3:25

Palal the son of Uzai [repaired] over against the turning [of the wall], and the tower that stands out from the upper house of the king, which is by the court of the guard. After him Pedaiah the son of Parosh [repaired].

(basi Wanethini hukaa Ofeli), mpaka mahali paelekeapo lango la maji kukabili mashariki, nao mnara utokezao. Nehemia 3:26

(Now the Nethinim lived in Ophel, to the place over against the water gate toward the east, and the tower that stands out.)

Baada yake wakafanyiza Watekoi sehemu nyingine, kuuelekea mnara mkubwa utokezao, na mpaka ukuta wa Ofeli. Nehemia 3:27

After him the Tekoites repaired another portion, over against the great tower that stands out, and to the wall of Ophel.

Juu ya lango la farasi wakafanyiza makuhani, kila mtu kuielekea nyumba yake. Baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Imeri, kuielekea nyumba yake. Nehemia 3:28

Above the horse gate repaired the priests, everyone over against his own house.

Na baada yake akafanyiza Shemaya, mwana wa Shekania, mlinzi wa lango la mashariki. Nehemia 3:29

After them repaired Zadok the son of Immer over against his own house. After him repaired Shemaiah the son of Shecaniah, the keeper of the east gate.

Baada yake wakafanyiza Hanania, mwana wa Shelemia, na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, sehemu nyingine. Baada yake akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, sehemu nyingine kuelekea chumba chake. Nehemia 3:30

After him repaired Hananiah the son of Shelemiah, and Hanun the sixth son of Zalaph, another portion. After him repaired Meshullam the son of Berechiah over against his chamber.

Baada yake akafanyiza Malkiya, mmoja wa mafundi wa dhahabu, mpaka nyumba ya Wanethini, na ya wafanya biashara, kulielekea lango la gereza, na mpaka chumba cha juu cha pembeni. Nehemia 3:31

After him repaired Malchijah one of the goldsmiths to the house of the Nethinim, and of the merchants, over against the gate of Hammiphkad, and to the ascent of the corner.

Na kati ya chumba cha juu cha pembeni na lango la kondoo wakafanyiza mafundi wa dhahabu na wafanya biashara.

Nehemia 3:32

Between the ascent of the corner and the sheep gate repaired the goldsmiths and the merchants.