Nehemia Mlango 11 Nehemiah

Nehemia 11:1

Basi, wakuu wa watu walikuwa wakikaa Yerusalemu; nao watu waliosalia wakapiga kura, ili katika watu kumi kumleta mmoja akae ndani ya Yerusalemu mji mtakatifu, na wale kenda wakae mijini.

Nehemia 11:2

Na hao watu wakawabariki wote waliojitoa kwa hiari wakae Yerusalemu.

Nehemia 11:3

Basi hawa ndio wakuu wa jimbo waliokaa Yerusalemu; ila mijini mwa Yuda wakakaa kila mtu katika milki yake mijini mwao, yaani, Israeli, makuhani, na Walawi, na Wanethini, na akina watumwa wa Sulemani.

Nehemia 11:4

Tena wakakaa Yerusalemu wengine wa wana wa Yuda, na wengine wa wana wa Benyamini. Wa wana wa Yuda; Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, wa wana wa Peresi;

Nehemia 11:5

na Maaseya, mwana wa Baruki, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, Mshelani.

Nehemia 11:6

Wana wa Peresi wote waliokaa Yerusalemu walikuwa watu mia nne sitini na wanane, mashujaa.

Nehemia 11:7

Na wana wa Benyamini ndio hawa; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseva, mwana wa Ithieli, mwana wa Yeshaya.

Nehemia 11:8

Na baada yake Gabai, Salai, watu mia kenda ishirini na wanane.

Nehemia 11:9

Na Yoeli, mwana wa Zikri, alikuwa msimamizi wao; na Yuda, mwana wa Hasenua, alikuwa wa pili juu ya mji.

Nehemia 11:10

Wa makuhani; Yedaya, Yoyaribu, Yakini,

Nehemia 11:11

na Seraya, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, msimamizi wa nyumba ya Mungu,

Nehemia 11:12

na ndugu zao waliofanya kazi ya nyumbani, watu mia nane ishirini na wawili; na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amzi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya,

Nehemia 11:13

na ndugu zake, wakuu wa mbari za mababa, watu mia mbili arobaini na wawili; na Maasai, mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri,

Nehemia 11:14

na ndugu zao, waume mashujaa, watu mia na ishirini na wanane; na msimamizi wao alikuwa Zabdieli, mmojawapo wa hao wakuu.

Nehemia 11:15

Na wa Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni;

Nehemia 11:16

na Shabethai na Yozabadi, wa wakuu wa Walawi, walioisimamia kazi ya nje ya nyumba ya Mungu;

Nehemia 11:17

na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu mwenye kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.

Nehemia 11:18

Walawi wote waliokaa katika mji mtakatifu walikuwa watu mia mbili themanini na wanne.

Nehemia 11:19

Pamoja na hao, mabawabu; Akubu, Talmoni, na ndugu zao waliolinda malangoni, walikuwa watu mia na sabini na wawili.

Nehemia 11:20

Na Israeli waliosalia, katika hao makuhani, na Walawi, walikuwamo mijini mwote mwa Yuda, kila mtu katika milki yake.

Nehemia 11:21

Lakini Wanethini walikuwa wakikaa Ofeli; na juu ya Wanethini walikuwa Siha na Gishpa.

Nehemia 11:22

Naye msimamizi wa Walawi huko Yerusalemu, ni Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika, wa wana wa Asafu, hao waimbaji, alikuwa juu ya kazi ya nyumba ya Mungu.

Nehemia 11:23

Kwa kuwa palikuwa na amri ya mfalme juu yao, na agizo la hakika walilowekewa waimbaji, kama ilivyohusika na kila siku.

Nehemia 11:24

Na Pethahia, mwana wa Meshezabeli, wa wana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa wakili wa mfalme kwa habari ya mambo yote ya watu.

Nehemia 11:25

Na katika habari za vijiji na mashamba yake; wengine wa wana wa Yuda walikuwa wakikaa Kiriath-arba na vijiji vyake, na katika Diboni na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake;

Nehemia 11:26

na katika Yeshua, na Molada, na Beth-peleti;

Nehemia 11:27

na Hazar-shuali, na Beer-sheba na vijiji vyake;

Nehemia 11:28

na katika Siklagi, na Mekona na vijiji vyake;

Nehemia 11:29

na katika Enrimoni, na Sora, na Yarmuthi;

Nehemia 11:30

Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, Lakishi na mashamba yake, Azeka na vijiji vyake. Hivyo wakatua toka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.

Nehemia 11:31

Wana wa Benyamini nao walikuwa wakikaa Geba, na Mikmashi, na Aiya, na Beth-eli na vijiji vyake;

Nehemia 11:32

Anathothi, Nobu, Anania;

Nehemia 11:33

Hazori, Rama, Gitaimu;

Nehemia 11:34

Hadidi, Seboimu, Nebalati;

Nehemia 11:35

Lodi, na Ono, bonde la Wakarashi.

Nehemia 11:36

Na wa Walawi, wengine walikaa katika Yuda na wengine katika Benyamini.