Nehemia 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Nehemia 2 (Swahili) Nehemiah 2 (English)

Ikawa katika mwezi wa Nisani, mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wo wote. Nehemia 2:1

It happened in the month Nisan, in the twentieth year of Artaxerxes the king, when wine was before him, that I took up the wine, and gave it to the king. Now I had not been [before] sad in his presence.

Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana. Nehemia 2:2

The king said to me, Why is your face sad, seeing you are not sick? this is nothing else but sorrow of heart. Then I was very sore afraid.

Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto? Nehemia 2:3

I said to the king, Let the king live forever: why should not my face be sad, when the city, the place of my fathers' tombs, lies waste, and the gates of it are consumed with fire?

Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. Nehemia 2:4

Then the king said to me, For what do you make request? So I prayed to the God of heaven.

Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. Nehemia 2:5

I said to the king, If it please the king, and if your servant have found favor in your sight, that you would send me to Judah, to the city of my fathers' tombs, that I may build it.

Mfalme akaniuliza, (malkia naye ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunipeleka; nami nikampa muda. Nehemia 2:6

The king said to me (the queen also sitting by him), For how long shall your journey be? and when will you return? So it pleased the king to send me; and I set him a time.

Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, ili waniache kupita mpaka nifike Yuda; Nehemia 2:7

Moreover I said to the king, If it please the king, let letters be given me to the governors beyond the River, that they may let me pass through until I come to Judah;

nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza mwitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanyizia boriti kwa malango ya ngome ya nyumba, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakayoingia mimi. Naye mfalme akanipa, kama mkono mwema wa Mungu wangu ulivyokuwa juu yangu. Nehemia 2:8

and a letter to Asaph the keeper of the king's forest, that he may give me timber to make beams for the gates of the castle which appertains to the house, and for the wall of the city, and for the house that I shall enter into. The king granted me, according to the good hand of my God on me.

Ndipo nikafika kwa maliwali walio ng'ambo ya Mto, nikawapa hizo nyaraka za mfalme. Naye mfalme alikuwa amepeleka maakida wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami. Nehemia 2:9

Then I came to the governors beyond the River, and gave them the king's letters. Now the king had sent with me captains of the army and horsemen.

Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli. Nehemia 2:10

When Sanballat the Horonite, and Tobiah the servant, the Ammonite, heard of it, it grieved them exceedingly, because a man had come to seek the welfare of the children of Israel.

Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu. Nehemia 2:11

So I came to Jerusalem, and was there three days.

Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe. Nehemia 2:12

I arose in the night, I and some few men with me; neither told I any man what my God put into my heart to do for Jerusalem; neither was there any animal with me, except the animal that I rode on.

Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. Nehemia 2:13

I went out by night by the valley gate, even toward the jackal's well, and to the dung gate, and viewed the walls of Jerusalem, which were broken down, and the gates of it were consumed with fire.

Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama aliyekuwa chini yangu. Nehemia 2:14

Then I went on to the spring gate and to the king's pool: but there was no place for the animal that was under me to pass.

Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo. Nehemia 2:15

Then went I up in the night by the brook, and viewed the wall; and I turned back, and entered by the valley gate, and so returned.

Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo. Nehemia 2:16

The rulers didn't know where I went, or what I did; neither had I as yet told it to the Jews, nor to the priests, nor to the nobles, nor to the rulers, nor to the rest who did the work.

Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena. Nehemia 2:17

Then said I to them, You see the evil case that we are in, how Jerusalem lies waste, and the gates of it are burned with fire: come, and let us build up the wall of Jerusalem, that we be no more a reproach.

Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema. Nehemia 2:18

I told them of the hand of my God which was good on me, as also of the king's words that he had spoken to me. They said, Let us rise up and build. So they strengthened their hands for the good [work].

Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme? Nehemia 2:19

But when Sanballat the Horonite, and Tobiah the servant, the Ammonite, and Geshem the Arabian, heard it, they ridiculed us, and despised us, and said, What is this thing that you do? will you rebel against the king?

Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.

Nehemia 2:20

Then answered I them, and said to them, The God of heaven, he will prosper us; therefore we his servants will arise and build: but you have no portion, nor right, nor memorial, in Jerusalem.