Yohana 18 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 18 (Swahili) John 18 (English)

Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake. Yohana 18:1

When Jesus had spoken these words, he went out with his disciples over the brook Kidron, where was a garden, into which he and his disciples entered.

Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. Yohana 18:2

Now Judas, who betrayed him, also knew the place, for Jesus often resorted there with his disciples.

Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha. Yohana 18:3

Judas then, having taken a detachment of soldiers and officers from the chief priests and the Pharisees, came there with lanterns, torches, and weapons.

Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? Yohana 18:4

Jesus therefore, knowing all the things that were happening to him, went forth, and said to them, "Who are you looking for?"

Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. Yohana 18:5

They answered him, "Jesus of Nazareth." Jesus said to them, "I AM." Judas also, who betrayed him, was standing with them.

Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. Yohana 18:6

When therefore he said to them, "I AM," they went backward, and fell to the ground.

Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. Yohana 18:7

Again therefore he asked them, "Who are you looking for?" They said, "Jesus of Nazareth."

Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao. Yohana 18:8

Jesus answered, "I told you that I AM. If therefore you seek me, let these go their way,"

Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. Yohana 18:9

that the word might be fulfilled which he spoke, "Of those whom you have given me, I have lost none."

Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. Yohana 18:10

Simon Peter therefore, having a sword, drew it, and struck the high priest's servant, and cut off his right ear. The servant's name was Malchus.

Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee? Yohana 18:11

Jesus therefore said to Peter, "Put the sword into its sheath. The cup which the Father has given me, shall I not surely drink it?"

Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga. Yohana 18:12

So the detachment, the commanding officer, and the officers of the Jews, seized Jesus and bound him,

Wakamchukua kwa Anasi kwanza; maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. Yohana 18:13

and led him to Annas first, for he was father-in-law to Caiaphas, who was high priest that year.

Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. Yohana 18:14

Now it was Caiaphas who advised the Jews that it was expedient that one man should perish for the people.

Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu. Yohana 18:15

Simon Peter followed Jesus, as did another disciple. Now that disciple was known to the high priest, and entered in with Jesus into the court of the high priest;

Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani. Yohana 18:16

but Peter was standing at the door outside. So the other disciple, who was known to the high priest, went out and spoke to her who kept the door, and brought in Peter.

Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi. Yohana 18:17

Then the maid who kept the door said to Peter, "Are you also one of this man's disciples?" He said, "I am not."

Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi; wakawa wakikota moto. Petro naye alikuwapo pamoja nao, anakota moto. Yohana 18:18

Now the servants and the officers were standing there, having made a fire of coals, for it was cold. They were warming themselves. Peter was with them, standing and warming himself.

Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu habari za wanafunzi wake, na habari za mafundisho yake. Yohana 18:19

The high priest therefore asked Jesus about his disciples, and about his teaching.

Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lo lote. Yohana 18:20

Jesus answered him, "I spoke openly to the world. I always taught in synagogues, and in the temple, where the Jews always meet. I said nothing in secret.

Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale waliosikia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyoyanena. Yohana 18:21

Why do you ask me? Ask those who have heard me what I said to them. Behold, these know the things which I said."

Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu? Yohana 18:22

When he had said this, one of the officers standing by slapped Jesus with his hand, saying, "Do you answer the high priest like that?"

Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini? Yohana 18:23

Jesus answered him, "If I have spoken evil, testify of the evil; but if well, why do you beat me?"

Basi Anasi akampeleka hali amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu. Yohana 18:24

Annas sent him bound to Caiaphas, the high priest.

Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi. Yohana 18:25

Now Simon Peter was standing and warming himself. They said therefore to him, "You aren't also one of his disciples, are you?" He denied it, and said, "I am not."

Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye? Yohana 18:26

One of the servants of the high priest, being a relative of him whose ear Peter had cut off, said, "Didn't I see you in the garden with him?"

Basi Petro akakana tena, na mara akawika jimbi. Yohana 18:27

Peter therefore denied it again, and immediately the rooster crowed.

Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri;lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile praitorio,wasije wakanajisika,bali wapate kuila Pasaka. Yohana 18:28

They led Jesus therefore from Caiaphas into the Praetorium. It was early, and they themselves didn't enter into the Praetorium, that they might not be defiled, but might eat the Passover.

Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? Yohana 18:29

Pilate therefore went out to them, and said, "What accusation do you bring against this man?"

Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. Yohana 18:30

They answered him, "If this man weren't an evildoer, we wouldn't have delivered him up to you."

Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. Yohana 18:31

Pilate therefore said to them, "Take him yourselves, and judge him according to your law." Therefore the Jews said to him, "It is not lawful for us to put anyone to death,"

Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa. Yohana 18:32

that the word of Jesus might be fulfilled, which he spoke, signifying by what kind of death he should die.

Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? Yohana 18:33

Pilate therefore entered again into the Praetorium, called Jesus, and said to him, "Are you the King of the Jews?"

Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? Yohana 18:34

Jesus answered him, "Do you say this by yourself, or did others tell you about me?"

Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? Yohana 18:35

Pilate answered, "I'm not a Jew, am I? Your own nation and the chief priests delivered you to me. What have you done?"

Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. Yohana 18:36

Jesus answered, "My Kingdom is not of this world. If my Kingdom were of this world, then my servants would fight, that I wouldn't be delivered to the Jews. But now my Kingdom is not from here."

Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. Yohana 18:37

Pilate therefore said to him, "Are you a king then?" Jesus answered, "You say that I am a king. For this reason I have been born, and for this reason I have come into the world, that I should testify to the truth. Everyone who is of the truth listens to my voice."

Pilato akamwambia, Kweli ni nini? Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yo yote kwake. Yohana 18:38

Pilate said to him, "What is truth?" When he had said this, he went out again to the Jews, and said to them, "I find no basis for a charge against him.

Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi, mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi? Yohana 18:39

But you have a custom, that I should release someone to you at the Passover. Therefore do you want me to release to you the King of the Jews?"

Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi. Yohana 18:40

Then they all shouted again, saying, "Not this man, but Barabbas!" Now Barabbas was a robber.