Yohana 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 1 (Swahili) John 1 (English)

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Yohana 1:1

In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.

Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Yohana 1:2

The same was in the beginning with God.

Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Yohana 1:3

All things were made through him. Without him was not anything made that has been made.

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Yohana 1:4

In him was life, and the life was the light of men.

Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza. Yohana 1:5

The light shines in the darkness, and the darkness hasn't overcome{The word translated "overcome" (katelaben) can also be translated "comprehended." It refers to getting a grip on an enemy to defeat him.} it.

Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Yohana 1:6

There came a man, sent from God, whose name was John.

Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Yohana 1:7

The same came as a witness, that he might testify about the light, that all might believe through him.

Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Yohana 1:8

He was not the light, but was sent that he might testify about the light.

Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Yohana 1:9

The true light that enlightens everyone was coming into the world.

Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Yohana 1:10

He was in the world, and the world was made through him, and the world didn't recognize him.

Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Yohana 1:11

He came to his own, and those who were his own didn't receive him.

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; Yohana 1:12

But as many as received him, to them he gave the right to become God's children, to those who believe in his name:

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Yohana 1:13

who were born not of blood, nor of the will of the flesh, nor of the will of man, but of God.

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Yohana 1:14

The Word became flesh, and lived among us. We saw his glory, such glory as of the one and only Son of the Father, full of grace and truth.

Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Yohana 1:15

John testified about him. He cried out, saying, "This was he of whom I said, 'He who comes after me has surpassed me, for he was before me.'"

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Yohana 1:16

From his fullness we all received grace upon grace.

Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Yohana 1:17

For the law was given through Moses. Grace and truth came through Jesus Christ.

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Yohana 1:18

No one has seen God at any time. The one and only Son, who is in the bosom of the Father, he has declared him.

Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Yohana 1:19

This is John's testimony, when the Jews sent priests and Levites from Jerusalem to ask him, "Who are you?"

Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Yohana 1:20

He confessed, and didn't deny, but he confessed, "I am not the Christ."

Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Yohana 1:21

They asked him, "What then? Are you Elijah?" He said, "I am not." "Are you the Prophet?" He answered, "No."

Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Yohana 1:22

They said therefore to him, "Who are you? Give us an answer to take back to those who sent us. What do you say about yourself?"

Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. Yohana 1:23

He said, "I am the voice of one crying in the wilderness, 'Make straight the way of the Lord,' as Isaiah the prophet said."

Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. Yohana 1:24

The ones who had been sent were from the Pharisees.

Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? Yohana 1:25

They asked him, "Why then do you baptize, if you are not the Christ, nor Elijah, nor the Prophet?"

Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. Yohana 1:26

John answered them, "I baptize in water, but among you stands one whom you don't know.

Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. Yohana 1:27

He is the one who comes after me, who is preferred before me, whose sandal strap I'm not worthy to loosen."

Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza. Yohana 1:28

These things were done in Bethany beyond the Jordan, where John was baptizing.

Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Yohana 1:29

The next day, he saw Jesus coming to him, and said, "Behold, the Lamb of God, who takes away the sin of the world!

Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Yohana 1:30

This is he of whom I said, 'After me comes a man who is preferred before me, for he was before me.'

Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Yohana 1:31

I didn't know him, but for this reason I came baptizing in water: that he would be revealed to Israel."

Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Yohana 1:32

John testified, saying, "I have seen the Spirit descending like a dove out of heaven, and it remained on him.

Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Yohana 1:33

I didn't recognize him, but he who sent me to baptize in water, he said to me, 'On whomever you will see the Spirit descending, and remaining on him, the same is he who baptizes in the Holy Spirit.'

Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. Yohana 1:34

I have seen, and have testified that this is the Son of God."

Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Yohana 1:35

Again, the next day, John was standing with two of his disciples,

Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! Yohana 1:36

and he looked at Jesus as he walked, and said, "Behold, the Lamb of God!"

Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yohana 1:37

The two disciples heard him speak, and they followed Jesus.

Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? Yohana 1:38

Jesus turned, and saw them following, and said to them, "What are you looking for?" They said to him, "Rabbi" (which is to say, being interpreted, Teacher), "where are you staying?"

Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. Yohana 1:39

He said to them, "Come, and see." They came and saw where he was staying, and they stayed with him that day. It was about the tenth hour.{4:00 PM.}

Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. Yohana 1:40

One of the two who heard John, and followed him, was Andrew, Simon Peter's brother.

Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Yohana 1:41

He first found his own brother, Simon, and said to him, "We have found the Messiah!" (which is, being interpreted, Christ{"Messiah" (Hebrew) and "Christ" (Greek) both mean "Anointed One".}).

Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe). Yohana 1:42

He brought him to Jesus. Jesus looked at him, and said, "You are Simon the son of Jonah. You shall be called Cephas" (which is by interpretation, Peter).

Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. Yohana 1:43

On the next day, he was determined to go out into Galilee, and he found Philip. Jesus said to him, "Follow me."

Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. Yohana 1:44

Now Philip was from Bethsaida, of the city of Andrew and Peter.

Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Yohana 1:45

Philip found Nathanael, and said to him, "We have found him, of whom Moses in the law, and the prophets, wrote: Jesus of Nazareth, the son of Joseph."

Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Yohana 1:46

Nathanael said to him, "Can any good thing come out of Nazareth?" Philip said to him, "Come and see."

Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Yohana 1:47

Jesus saw Nathanael coming to him, and said about him, "Behold, an Israelite indeed, in whom is no deceit!"

Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Yohana 1:48

Nathanael said to him, "How do you know me?" Jesus answered him, "Before Philip called you, when you were under the fig tree, I saw you."

Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yohana 1:49

Nathanael answered him, "Rabbi, you are the Son of God! You are King of Israel!"

Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Yohana 1:50

Jesus answered him, "Because I told you, 'I saw you underneath the fig tree,' do you believe? You will see greater things than these!"

Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu. Yohana 1:51

He said to him, "Most assuredly, I tell you, hereafter you will see heaven opened, and the angels of God ascending and descending on the Son of Man."