Yohana 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 11 (Swahili) John 11 (English)

Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Yohana 11:1

Now a certain man was sick, Lazarus from Bethany, of the village of Mary and her sister, Martha.

Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. Yohana 11:2

It was that Mary who had anointed the Lord with ointment, and wiped his feet with her hair, whose brother, Lazarus, was sick.

Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. Yohana 11:3

The sisters therefore sent to him, saying, "Lord, behold, he for whom you have great affection is sick."

Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Yohana 11:4

But when Jesus heard it, he said, "This sickness is not to death, but for the glory of God, that God's Son may be glorified by it."

Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. Yohana 11:5

Now Jesus loved Martha, and her sister, and Lazarus.

Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Yohana 11:6

When therefore he heard that he was sick, he stayed two days in the place where he was.

Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. Yohana 11:7

Then after this he said to the disciples, "Let's go into Judea again."

Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? Yohana 11:8

The disciples told him, "Rabbi, the Jews were just trying to stone you, and are you going there again?"

Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Yohana 11:9

Jesus answered, "Aren't there twelve hours of daylight? If a man walks in the day, he doesn't stumble, because he sees the light of this world.

Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. Yohana 11:10

But if a man walks in the night, he stumbles, because the light isn't in him."

Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Yohana 11:11

He said these things, and after that, he said to them, "Our friend, Lazarus, has fallen asleep, but I am going so that I may awake him out of sleep."

Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. Yohana 11:12

The disciples therefore said, "Lord, if he has fallen asleep, he will recover."

Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. Yohana 11:13

Now Jesus had spoken of his death, but they thought that he spoke of taking rest in sleep.

Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. Yohana 11:14

So Jesus said to them plainly then, "Lazarus is dead.

Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. Yohana 11:15

I am glad for your sakes that I was not there, so that you may believe. Nevertheless, let's go to him."

Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye. Yohana 11:16

Thomas therefore, who is called Didymus,{"Didymus" means "Twin"} said to his fellow disciples, "Let's go also, that we may die with him."

Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Yohana 11:17

So when Jesus came, he found that he had been in the tomb four days already.

Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; Yohana 11:18

Now Bethany was near Jerusalem, about fifteen stadia{15 stadia is about 2.8 kilometers or 1.7 miles} away.

na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Yohana 11:19

Many of the Jews had joined the women around Martha and Mary, to console them concerning their brother.

Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Yohana 11:20

Then when Martha heard that Jesus was coming, she went and met him, but Mary stayed in the house.

Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Yohana 11:21

Therefore Martha said to Jesus, "Lord, if you would have been here, my brother wouldn't have died.

Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yohana 11:22

Even now I know that, whatever you ask of God, God will give you."

Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Yohana 11:23

Jesus said to her, "Your brother will rise again."

Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yohana 11:24

Martha said to him, "I know that he will rise again in the resurrection at the last day."

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; Yohana 11:25

Jesus said to her, "I am the resurrection and the life. He who believes in me, though he die, yet will he live.

naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? Yohana 11:26

Whoever lives and believes in me will never die. Do you believe this?"

Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni. Yohana 11:27

She said to him, "Yes, Lord. I have come to believe that you are the Christ, God's Son, he who comes into the world."

Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. Yohana 11:28

When she had said this, she went away, and called Mary, her sister, secretly, saying, "The Teacher is here, and is calling you."

Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. Yohana 11:29

When she heard this, she arose quickly, and went to him.

Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. Yohana 11:30

Now Jesus had not yet come into the village, but was in the place where Martha met him.

Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. Yohana 11:31

Then the Jews who were with her in the house, and were consoling her, when they saw Mary, that she rose up quickly and went out, followed her, saying, "She is going to the tomb to weep there."

Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Yohana 11:32

Therefore when Mary came to where Jesus was, and saw him, she fell down at his feet, saying to him, "Lord, if you would have been here, my brother wouldn't have died."

Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, Yohana 11:33

When Jesus therefore saw her weeping, and the Jews weeping who came with her, he groaned in the spirit, and was troubled,

akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yohana 11:34

and said, "Where have you laid him?" They told him, "Lord, come and see."

Yesu akalia machozi. Yohana 11:35

Jesus wept.

Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. Yohana 11:36

The Jews therefore said, "See how much affection he had for him!"

Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Yohana 11:37

Some of them said, "Couldn't this man, who opened the eyes of him who was blind, have also kept this man from dying?"

Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yohana 11:38

Jesus therefore, again groaning in himself, came to the tomb. Now it was a cave, and a stone lay against it.

Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yohana 11:39

Jesus said, "Take away the stone." Martha, the sister of him who was dead, said to him, "Lord, by this time there is a stench, for he has been dead four days."

Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Yohana 11:40

Jesus said to her, "Didn't I tell you that if you believed, you would see God's glory?"

Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Yohana 11:41

So they took away the stone from the place where the dead man was lying. Jesus lifted up his eyes, and said, "Father, I thank you that you listened to me.

Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Yohana 11:42

I know that you always listen to me, but because of the multitude that stands around I said this, that they may believe that you sent me."

Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Yohana 11:43

When he had said this, he cried with a loud voice, "Lazarus, come out!"

Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake. Yohana 11:44

He who was dead came out, bound hand and foot with wrappings, and his face was wrapped around with a cloth. Jesus said to them, "Free him, and let him go."

Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. Yohana 11:45

Therefore many of the Jews, who came to Mary and saw what Jesus did, believed in him.

Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. Yohana 11:46

But some of them went away to the Pharisees, and told them the things which Jesus had done.

Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. Yohana 11:47

The chief priests therefore and the Pharisees gathered a council, and said, "What are we doing? For this man does many signs.

Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. Yohana 11:48

If we leave him alone like this, everyone will believe in him, and the Romans will come and take away both our place and our nation."

Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; Yohana 11:49

But a certain one of them, Caiaphas, being high priest that year, said to them, "You know nothing at all,

wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. Yohana 11:50

nor do you consider that it is advantageous for us that one man should die for the people, and that the whole nation not perish."

Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. Yohana 11:51

Now he didn't say this of himself, but being high priest that year, he prophesied that Jesus would die for the nation,

Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja. Yohana 11:52

and not for the nation only, but that he might also gather together into one the children of God who are scattered abroad.

Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. Yohana 11:53

So from that day forward they took counsel that they might put him to death.

Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. Yohana 11:54

Jesus therefore walked no more openly among the Jews, but departed from there into the country near the wilderness, to a city called Ephraim. He stayed there with his disciples.

Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. Yohana 11:55

Now the Passover of the Jews was at hand. Many went up from the country to Jerusalem before the Passover, to purify themselves.

Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? Yohana 11:56

Then they sought for Jesus and spoke one with another, as they stood in the temple, "What do you think--that he isn't coming to the feast at all?"

Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata. Yohana 11:57

Now the chief priests and the Pharisees had commanded that if anyone knew where he was, he should report it, that they might seize him.