Yohana 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 12 (Swahili) John 12 (English)

Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu. Yohana 12:1

Then six days before the Passover, Jesus came to Bethany, where Lazarus was, who had been dead, whom he raised from the dead.

Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye. Yohana 12:2

So they made him a supper there. Martha served, but Lazarus was one of those who sat at the table with him.

Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu. Yohana 12:3

Mary, therefore, took a pound{a Roman pound of 12 ounces, or about 340 grams} of ointment of pure nard, very precious, and anointed the feet of Jesus, and wiped his feet with her hair. The house was filled with the fragrance of the ointment.

Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, Yohana 12:4

Then Judas Iscariot, Simon's son, one of his disciples, who would betray him, said,

Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? Yohana 12:5

"Why wasn't this ointment sold for three hundred denarii,{300 denarii was about a year's wages for an agricultural laborer.} and given to the poor?"

Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo. Yohana 12:6

Now he said this, not because he cared for the poor, but because he was a thief, and having the money box, used to steal what was put into it.

Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu. Yohana 12:7

But Jesus said, "Leave her alone. She has kept this for the day of my burial.

Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote. Yohana 12:8

For you always have the poor with you, but you don't always have me."

Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. Yohana 12:9

A large crowd therefore of the Jews learned that he was there, and they came, not for Jesus' sake only, but that they might see Lazarus also, whom he had raised from the dead.

Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; Yohana 12:10

But the chief priests conspired to put Lazarus to death also,

maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu. Yohana 12:11

because on account of him many of the Jews went away and believed in Jesus.

Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; Yohana 12:12

On the next day a great multitude had come to the feast. When they heard that Jesus was coming to Jerusalem,

wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! Yohana 12:13

they took the branches of the palm trees, and went out to meet him, and cried out, "Hosanna! Blessed is he who comes in the name of the Lord, the King of Israel!"

Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, Yohana 12:14

Jesus, having found a young donkey, sat on it. As it is written,

Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. Yohana 12:15

"Don't be afraid, daughter of Zion. Behold, your King comes, sitting on a donkey's colt."

Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. Yohana 12:16

His disciples didn't understand these things at first, but when Jesus was glorified, then they remembered that these things were written about him, and that they had done these things to him.

Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. Yohana 12:17

The multitude therefore that was with him when he called Lazarus out of the tomb, and raised him from the dead, was testifying about it.

Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo. Yohana 12:18

For this cause also the multitude went and met him, because they heard that he had done this sign.

Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake. Yohana 12:19

The Pharisees therefore said among themselves, "See how you accomplish nothing. Behold, the world has gone after him."

Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu. Yohana 12:20

Now there were certain Greeks among those that went up to worship at the feast.

Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. Yohana 12:21

These, therefore, came to Philip, who was from Bethsaida of Galilee, and asked him, saying, "Sir, we want to see Jesus."

Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Yohana 12:22

Philip came and told Andrew, and in turn, Andrew came with Philip, and they told Jesus.

Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Yohana 12:23

Jesus answered them, "The time has come for the Son of Man to be glorified.

Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi. Yohana 12:24

Most assuredly I tell you, unless a grain of wheat falls into the earth and dies, it remains by itself alone. But if it dies, it bears much fruit.

Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. Yohana 12:25

He who loves his life will lose it. He who hates his life in this world will keep it to eternal life.

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. Yohana 12:26

If anyone serves me, let him follow me. Where I am, there will my servant also be. If anyone serves me, the Father will honor him.

Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii. Yohana 12:27

"Now my soul is troubled. What shall I say? 'Father, save me from this time?' But for this cause I came to this time.

Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. Yohana 12:28

Father, glorify your name!" Then there came a voice out of the sky, saying, "I have both glorified it, and will glorify it again."

Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye. Yohana 12:29

The multitude therefore, who stood by and heard it, said that it had thundered. Others said, "An angel has spoken to him."

Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu. Yohana 12:30

Jesus answered, "This voice hasn't come for my sake, but for your sakes.

Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. Yohana 12:31

Now is the judgment of this world. Now the prince of this world will be cast out.

Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. Yohana 12:32

And I, if I am lifted up from the earth, will draw all people to myself."

Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa. Yohana 12:33

But he said this, signifying by what kind of death he should die.

Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani? Yohana 12:34

The multitude answered him, "We have heard out of the law that the Christ remains forever. How do you say, 'The Son of Man must be lifted up?' Who is this Son of Man?"

Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako. Yohana 12:35

Jesus therefore said to them, "Yet a little while the light is with you. Walk while you have the light, that darkness doesn't overtake you. He who walks in the darkness doesn't know where he is going.

Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone. Yohana 12:36

While you have the light, believe in the light, that you may become children of light." Jesus said these things, and he departed and hid himself from them.

Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini; Yohana 12:37

But though he had done so many signs before them, yet they didn't believe in him,

ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Yohana 12:38

that the word of Isaiah the prophet might be fulfilled, which he spoke, "Lord, who has believed our report? To whom has the arm of the Lord been revealed?"

Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena, Yohana 12:39

For this cause they couldn't believe, for Isaiah said again,

Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. Yohana 12:40

"He has blinded their eyes and he hardened their heart, Lest they should see with their eyes, And perceive with their heart, And would turn, And I would heal them."

Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake. Yohana 12:41

Isaiah said these things when he saw his glory, and spoke of him.

Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Yohana 12:42

Nevertheless even of the rulers many believed in him, but because of the Pharisees they didn't confess it, so that they wouldn't be put out of the synagogue,

Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu. Yohana 12:43

for they loved men's praise more than God's praise.

Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka. Yohana 12:44

Jesus cried out and said, "Whoever believes in me, believes not in me, but in him who sent me.

Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka. Yohana 12:45

He who sees me sees him who sent me.

Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. Yohana 12:46

I have come as a light into the world, that whoever believes in me may not remain in the darkness.

Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. Yohana 12:47

If anyone listens to my sayings, and doesn't believe, I don't judge him. For I came not to judge the world, but to save the world.

Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Yohana 12:48

He who rejects me, and doesn't receive my sayings, has one who judges him. The word that I spoke, the same will judge him in the last day.

Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Yohana 12:49

For I spoke not from myself, but the Father who sent me, he gave me a commandment, what I should say, and what I should speak.

Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo. Yohana 12:50

I know that his commandment is eternal life. The things therefore which I speak, even as the Father has said to me, so I speak."