Yohana 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 7 (Swahili) John 7 (English)

Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Yohana 7:1

After these things, Jesus was walking in Galilee, for he wouldn't walk in Judea, because the Jews sought to kill him.

Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. Yohana 7:2

Now the feast of the Jews, the Feast of Booths, was at hand.

Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Yohana 7:3

His brothers therefore said to him, "Depart from here, and go into Judea, that your disciples also may see your works which you do.

Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Yohana 7:4

For no one does anything in secret, and himself seeks to be known openly. If you do these things, reveal yourself to the world."

Maana hata nduguze hawakumwamini. Yohana 7:5

For even his brothers didn't believe in him.

Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. Yohana 7:6

Jesus therefore said to them, "My time has not yet come, but your time is always ready.

Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Yohana 7:7

The world can't hate you, but it hates me, because I testify about it, that its works are evil.

Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. Yohana 7:8

You go up to the feast. I am not yet going up to this feast, because my time is not yet fulfilled."

Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya. Yohana 7:9

Having said these things to them, he stayed in Galilee.

Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri. Yohana 7:10

But when his brothers had gone up to the feast, then he also went up, not publicly, but as it were in secret.

Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule? Yohana 7:11

The Jews therefore sought him at the feast, and said, "Where is he?"

Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano. Yohana 7:12

There was much murmuring among the multitudes concerning him. Some said, "He is a good man." Others said, "Not so, but he leads the multitude astray."

Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. Yohana 7:13

Yet no one spoke openly of him for fear of the Jews.

Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. Yohana 7:14

But when it was now the midst of the feast, Jesus went up into the temple and taught.

Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? Yohana 7:15

The Jews therefore marveled, saying, "How does this man know letters, having never been educated?"

Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Yohana 7:16

Jesus therefore answered them, "My teaching is not mine, but his who sent me.

Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yohana 7:17

If anyone desires to do his will, he will know about the teaching, whether it is from God, or if I am speaking from myself.

Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu. Yohana 7:18

He who speaks from himself seeks his own glory, but he who seeks the glory of him who sent him, the same is true, and no unrighteousness is in him.

Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? Yohana 7:19

Didn't Moses give you the law, and yet none of you keeps the law? Why do you seek to kill me?"

Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? Yohana 7:20

The multitude answered, "You have a demon! Who seeks to kill you?"

Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. Yohana 7:21

Jesus answered them, "I did one work, and you all marvel because of it.

Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. Yohana 7:22

Moses has given you circumcision (not that it is of Moses, but of the fathers), and on the Sabbath you circumcise a boy.

Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? Yohana 7:23

If a boy receives circumcision on the Sabbath, that the law of Moses may not be broken, are you angry with me, because I made a man every bit whole on the Sabbath?

Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. Yohana 7:24

Don't judge according to appearance, but judge righteous judgment."

Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? Yohana 7:25

Therefore some of them of Jerusalem said, "Isn't this he whom they seek to kill?

Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? Yohana 7:26

Behold, he speaks openly, and they say nothing to him. Can it be that the rulers indeed know that this is truly the Christ?

Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako. Yohana 7:27

However we know where this man comes from, but when the Christ comes, no one will know where he comes from."

Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Yohana 7:28

Jesus therefore cried out in the temple, teaching and saying, "You both know me, and know where I am from. I have not come of myself, but he who sent me is true, whom you don't know.

Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. Yohana 7:29

I know him, because I am from him, and he sent me."

Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado. Yohana 7:30

They sought therefore to take him; but no one laid a hand on him, because his hour had not yet come.

Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? Yohana 7:31

But of the multitude, many believed in him. They said, "When the Christ comes, he won't do more signs than those which this man has done, will he?"

Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate. Yohana 7:32

The Pharisees heard the multitude murmuring these things concerning him, and the chief priests and the Pharisees sent officers to arrest him.

Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. Yohana 7:33

Then Jesus said, "I will be with you a little while longer, then I go to him who sent me.

Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. Yohana 7:34

You will seek me, and won't find me; and where I am, you can't come."

Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? Yohana 7:35

The Jews therefore said among themselves, "Where will this man go that we won't find him? Will he go to the Dispersion among the Greeks, and teach the Greeks?

Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja? Yohana 7:36

What is this word that he said, 'You will seek me, and won't find me; and where I am, you can't come?'"

Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Yohana 7:37

Now on the last and greatest day of the feast, Jesus stood and cried out, "If anyone is thirsty, let him come to me and drink!

Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:38

He who believes in me, as the Scripture has said, from within him will flow rivers of living water."

Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa. Yohana 7:39

But he said this about the Spirit, which those believing in him were to receive. For the Holy Spirit was not yet given, because Jesus wasn't yet glorified.

Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule. Yohana 7:40

Many of the multitude therefore, when they heard these words, said, "This is truly the prophet."

Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya? Yohana 7:41

Others said, "This is the Christ." But some said, "What, does the Christ come out of Galilee?

Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi? Yohana 7:42

Hasn't the Scripture said that the Christ comes of the seed of David, and from Bethlehem, the village where David was?"

Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. Yohana 7:43

So there arose a division in the multitude because of him.

Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika. Yohana 7:44

Some of them would have arrested him, but no one laid hands on him.

Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? Yohana 7:45

The officers therefore came to the chief priests and Pharisees, and they said to them, "Why didn't you bring him?"

Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena. Yohana 7:46

The officers answered, "No man ever spoke like this man!"

Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika? Yohana 7:47

The Pharisees therefore answered them, "You aren't also led astray, are you?

Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? Yohana 7:48

Have any of the rulers believed in him, or of the Pharisees?

Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. Yohana 7:49

But this multitude that doesn't know the law is accursed."

Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), Yohana 7:50

Nicodemus (he who came to him by night, being one of them) said to them,

Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? Yohana 7:51

"Does our law judge a man, unless it first hears from him personally and knows what he does?"

Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya! Yohana 7:52

They answered him, "Are you also from Galilee? Search, and see that no prophet has arisen out of Galilee."

Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii. Yohana 7:53

Everyone went to his own house,