Yohana 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 2 (Swahili) John 2 (English)

Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yohana 2:1

The third day, there was a marriage in Cana of Galilee. Jesus' mother was there.

Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Yohana 2:2

Jesus also was invited, with his disciples, to the marriage.

Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. Yohana 2:3

When the wine ran out, Jesus' mother said to him, "They have no wine."

Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Yohana 2:4

Jesus said to her, "Woman, what does that have to do with you and me? My hour has not yet come."

Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni. Yohana 2:5

His mother said to the servants, "Whatever he says to you, do it."

Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yohana 2:6

Now there were six water pots of stone set there after the Jews' manner of purifying, containing two or three metretes{2 to 3 metretes is about 20 to 30 U. S. Gallons, 16 to 25 imperial gallons, or 75 to 115 litres.} apiece.

Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Yohana 2:7

Jesus said to them, "Fill the water pots with water." They filled them up to the brim.

Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka. Yohana 2:8

He said to them, "Now draw some out, and take it to the ruler of the feast." So they took it.

Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, Yohana 2:9

When the ruler of the feast tasted the water now become wine, and didn't know where it came from (but the servants who had drawn the water knew), the ruler of the feast called the bridegroom,

akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. Yohana 2:10

and said to him, "Everyone serves the good wine first, and when the guests have drunk freely, then that which is worse. You have kept the good wine until now!"

Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Yohana 2:11

This beginning of his signs Jesus did in Cana of Galilee, and revealed his glory; and his disciples believed in him.

Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi. Yohana 2:12

After this, he went down to Capernaum, he, and his mother, his brothers, and his disciples; and they stayed there a few days.

Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. Yohana 2:13

The Passover of the Jews was at hand, and Jesus went up to Jerusalem.

Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Yohana 2:14

He found in the temple those who sold oxen, sheep, and doves, and the changers of money sitting.

Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; Yohana 2:15

He made a whip of cords, and threw all out of the temple, both the sheep and the oxen; and he poured out the changers' money, and overthrew their tables.

akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Yohana 2:16

To those who sold the doves, he said, "Take these things out of here! Don't make my Father's house a marketplace!"

Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. Yohana 2:17

His disciples remembered that it was written, "Zeal for your house will eat me up."

Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Yohana 2:18

The Jews therefore answered him, "What sign do you show us, seeing that you do these things?"

Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Yohana 2:19

Jesus answered them, "Destroy this temple, and in three days I will raise it up."

Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Yohana 2:20

The Jews therefore said, "Forty-six years was this temple in building, and will you raise it up in three days?"

Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Yohana 2:21

But he spoke of the temple of his body.

Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu. Yohana 2:22

When therefore he was raised from the dead, his disciples remembered that he said this, and they believed the Scripture, and the word which Jesus had said.

Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya. Yohana 2:23

Now when he was in Jerusalem at the Passover, during the feast, many believed in his name, observing his signs which he did.

Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; Yohana 2:24

But Jesus didn't trust himself to them, because he knew everyone,

na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu. Yohana 2:25

and because he didn't need for anyone to testify concerning man; for he himself knew what was in man.