Yohana 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 3 (Swahili) John 3 (English)

Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Yohana 3:1

Now there was a man of the Pharisees named Nicodemus, a ruler of the Jews.

Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yohana 3:2

The same came to him by night, and said to him, "Rabbi, we know that you are a teacher come from God, for no one can do these signs that you do, unless God is with him."

Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Yohana 3:3

Jesus answered him, "Most assuredly, I tell you, unless one is born anew,{The word translated "anew" here and in John 3:7 (anothen) also means "again" and "from above".} he can't see the Kingdom of God."

Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yohana 3:4

Nicodemus said to him, "How can a man be born when he is old? Can he enter a second time into his mother's womb, and be born?"

Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Yohana 3:5

Jesus answered, "Most assuredly I tell you, unless one is born of water and spirit, he can't enter into the Kingdom of God!

Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Yohana 3:6

That which is born of the flesh is flesh. That which is born of the Spirit is spirit.

Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Yohana 3:7

Don't marvel that I said to you, 'You must be born anew.'

Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. Yohana 3:8

The wind{The same Greek word (pneuma) means wind, breath, and spirit.} blows where it wants to, and you hear its sound, but don't know where it comes from and where it is going. So is everyone who is born of the Spirit."

Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya? Yohana 3:9

Nicodemus answered him, "How can these things be?"

Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? Yohana 3:10

Jesus answered him, "Are you the teacher of Israel, and don't understand these things?

Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. Yohana 3:11

Most assuredly I tell you, we speak that which we know, and testify of that which we have seen, and you don't receive our witness.

Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? Yohana 3:12

If I told you earthly things and you don't believe, how will you believe if I tell you heavenly things?

Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. Yohana 3:13

No one has ascended into heaven, but he who descended out of heaven, the Son of Man, who is in heaven.

Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; Yohana 3:14

As Moses lifted up the serpent in the wilderness, even so must the Son of Man be lifted up,

ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Yohana 3:15

that whoever believes in him should not perish, but have eternal life.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16

For God so loved the world, that he gave his one and only Son, that whoever believes in him should not perish, but have eternal life.

Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Yohana 3:17

For God didn't send his Son into the world to judge the world, but that the world should be saved through him.

Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Yohana 3:18

He who believes in him is not judged. He who doesn't believe has been judged already, because he has not believed in the name of the one and only Son of God.

Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Yohana 3:19

This is the judgment, that the light has come into the world, and men loved the darkness rather than the light; for their works were evil.

Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Yohana 3:20

For everyone who does evil hates the light, and doesn't come to the light, lest his works would be exposed.

Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu. Yohana 3:21

But he who does the truth comes to the light, that his works may be revealed, that they have been done in God."

Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. Yohana 3:22

After these things, Jesus came with his disciples into the land of Judea. He stayed there with them, and baptized.

Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. Yohana 3:23

John also was baptizing in Enon near Salim, because there was much water there. They came, and were baptized.

Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani. Yohana 3:24

For John was not yet thrown into prison.

Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso. Yohana 3:25

There arose therefore a questioning on the part of John's disciples with some Jews about purification.

Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. Yohana 3:26

They came to John, and said to him, "Rabbi, he who was with you beyond the Jordan, to whom you have testified, behold, the same baptizes, and everyone is coming to him."

Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. Yohana 3:27

John answered, "A man can receive nothing, unless it has been given him from heaven.

Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Yohana 3:28

You yourselves testify that I said, 'I am not the Christ,' but, 'I have been sent before him.'

Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Yohana 3:29

He who has the bride is the bridegroom; but the friend of the bridegroom, who stands and hears him, rejoices greatly because of the bridegroom's voice. This, my joy, therefore is made full.

Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua. Yohana 3:30

He must increase, but I must decrease.

Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote. Yohana 3:31

He who comes from above is above all. He who is from the Earth belongs to the Earth, and speaks of the Earth. He who comes from heaven is above all.

Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake. Yohana 3:32

What he has seen and heard, of that he testifies; and no one receives his witness.

Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. Yohana 3:33

He who has received his witness has set his seal to this, that God is true.

Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. Yohana 3:34

For he whom God has sent speaks the words of God; for God gives the Spirit without measure.

Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. Yohana 3:35

The Father loves the Son, and has given all things into his hand.

Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Yohana 3:36

One who believes in the Son has eternal life, but one who disobeys{The same word can be translated "disobeys" or "disbelieves" in this context.} the Son won't see life, but the wrath of God remains on him."