Yohana 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 5 (Swahili) John 5 (English)

Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. Yohana 5:1

After these things, there was a feast of the Jews, and Jesus went up to Jerusalem.

Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. Yohana 5:2

Now in Jerusalem by the sheep gate, there is a pool, which is called in Hebrew, "Bethesda," having five porches.

Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Yohana 5:3

In these lay a great multitude of those who were sick, blind, lame, or paralyzed, waiting for the moving of the water;

Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] Yohana 5:4

for an angel of the Lord went down at certain times into the pool, and stirred up the water. Whoever stepped in first after the stirring of the water was made whole of whatever disease he had.

Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yohana 5:5

A certain man was there, who had been sick for thirty-eight years.

Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yohana 5:6

When Jesus saw him lying there, and knew that he had been sick for a long time, he asked him, "Do you want to be made well?"

Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yohana 5:7

The sick man answered him, "Sir, I have no one to put me into the pool when the water is stirred up, but while I'm coming, another steps down before me."

Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Yohana 5:8

Jesus said to him, "Arise, take up your mat, and walk."

Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. Yohana 5:9

Immediately, the man was made well, and took up his mat and walked. Now it was the Sabbath on that day.

Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro. Yohana 5:10

So the Jews said to him who was cured, "It is the Sabbath. It is not lawful for you to carry the mat."

Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende. Yohana 5:11

He answered them, "He who made me well, the same said to me, 'Take up your mat, and walk.'"

Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani? Yohana 5:12

Then they asked him, "Who is the man who said to you, 'Take up your mat, and walk'?"

Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale. Yohana 5:13

But he who was healed didn't know who it was, for Jesus had withdrawn, a crowd being in the place.

Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi. Yohana 5:14

Afterward Jesus found him in the temple, and said to him, "Behold, you are made well. Sin no more, so that nothing worse happens to you."

Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima. Yohana 5:15

The man went away, and told the Jews that it was Jesus who had made him well.

Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato. Yohana 5:16

For this cause the Jews persecuted Jesus, and sought to kill him, because he did these things on the Sabbath.

Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Yohana 5:17

But Jesus answered them, "My Father is still working, so I am working, too."

Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yohana 5:18

For this cause therefore the Jews sought all the more to kill him, because he not only broke the Sabbath, but also called God his own Father, making himself equal with God.

Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. Yohana 5:19

Jesus therefore answered them, "Most assuredly, I tell you, the Son can do nothing of himself, but what he sees the Father doing. For whatever things he does, these the Son also does likewise.

Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu. Yohana 5:20

For the Father has affection for the Son, and shows him all things that he himself does. He will show him greater works than these, that you may marvel.

Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao. Yohana 5:21

For as the Father raises the dead and gives them life, even so the Son also gives life to whom he desires.

Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; Yohana 5:22

For the Father judges no one, but he has given all judgment to the Son,

ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka. Yohana 5:23

that all may honor the Son, even as they honor the Father. He who doesn't honor the Son doesn't honor the Father who sent him.

Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Yohana 5:24

"Most assuredly I tell you, he who hears my word, and believes him who sent me, has eternal life, and doesn't come into judgment, but has passed out of death into life.

Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. Yohana 5:25

Most assuredly, I tell you, the hour comes, and now is, when the dead will hear the Son of God's voice; and those who hear will live.

Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. Yohana 5:26

For as the Father has life in himself, even so he gave to the Son also to have life in himself.

Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. Yohana 5:27

He also gave him authority to execute judgment, because he is a son of man.

Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Yohana 5:28

Don't marvel at this, for the hour comes, in which all that are in the tombs will hear his voice,

Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. Yohana 5:29

and will come out; those who have done good, to the resurrection of life; and those who have done evil, to the resurrection of judgment.

Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Yohana 5:30

I can of myself do nothing. As I hear, I judge, and my judgment is righteous; because I don't seek my own will, but the will of my Father who sent me.

Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. Yohana 5:31

"If I testify about myself, my witness is not valid.

Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. Yohana 5:32

It is another who testifies about me. I know that the testimony which he testifies about me is true.

Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli. Yohana 5:33

You have sent to John, and he has testified to the truth.

Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka. Yohana 5:34

But the testimony which I receive is not from man. However, I say these things that you may be saved.

Yeye alikuwa taa iwakayo na kung'aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda. Yohana 5:35

He was the burning and shining lamp, and you were willing to rejoice for a while in his light.

Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma. Yohana 5:36

But the testimony which I have is greater than that of John, for the works which the Father gave me to accomplish, the very works that I do, testify about me, that the Father has sent me.

Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. Yohana 5:37

The Father himself, who sent me, has testified about me. You have neither heard his voice at any time, nor seen his form.

Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. Yohana 5:38

You don't have his word living in you; because you don't believe him whom he sent.

Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Yohana 5:39

"You search the Scriptures, because you think that in them you have eternal life; and these are they which testify about me.

Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. Yohana 5:40

Yet you will not come to me, that you may have life.

Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu. Yohana 5:41

I don't receive glory from men.

Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. Yohana 5:42

But I know you, that you don't have God's love in yourselves.

Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. Yohana 5:43

I have come in my Father's name, and you don't receive me. If another comes in his own name, you will receive him.

Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti? Yohana 5:44

How can you believe, who receive glory from one another, and you don't seek the glory that comes from the only God?

Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. Yohana 5:45

"Don't think that I will accuse you to the Father. There is one who accuses you, even Moses, on whom you have set your hope.

Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Yohana 5:46

For if you believed Moses, you would believe me; for he wrote about me.

Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

Yohana 5:47

But if you don't believe his writings, how will you believe my words?"