Atafanya Kitu Lyrics - Zabron Singers
Zabron Singers sifa
Atafanya Kitu Lyrics
Ukihesabu utachoka kuna ya juzi jana na leo
Ya kesho Mungu kafanya
Huku kwetu hakunanga hofu, mashaka, wasiwasi
Twajiamini tuko na Mungu
Mimi si yule wa zamani wa kulialia
Mungu kanitoa huko namfurahia
Sasa nimehama kitengo cha kulialia
Nimehamia level zingine za kufurahia
Aliumba mchana, usiku
Lipi ngumu la kumishinda Mungu
Huyu Mungu hufanya zaidi ya mtu na mahitaji
Ametenda mengi kwangu
(Hebu subiri na wewe, Mungu atafanya kitu)
Usichoke ndugu yangu
(Subiri subiri na wewe, Huyu Yesu atafanya kitu)
Subiri, Subiri
Eeh Subiri
Huku kwa Yesu tupata shida mateso
Na Yesu anatatua
Twashukuru na kuimba sifa zake
Ni Yeye astahili kuinuliwa
Mungu katufanya tuimbe na kumtukuza
Tuvae tun'ngae tuishi na kufurahia
Siwezi hesabu mangapi kanisimamia
Mipaka nivuke na jina nikamtukuze
Kwa tiketi ya jina la Yesu
Hakuna jambo gumu kutushinda
Sifa zake zipande asante
Bwana umetuinua
Ametenda mengi kwangu
(Hebu subiri na wewe, Mungu atafanya kitu)
Usichoke ndugu yangu
(Subiri subiri na wewe, Huyu Yesu atafanya kitu)