Walter Chilambo - Busara Lyrics
Lyrics
Jawabu la upole huigeuza hasira bali neno liumizalo huchochea ghadhabu Midomo ya mwenye hekima hueleza hueneza Maarifa bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo Mmh bwana bwana bwana nakuita bwana Uliye mwama bwana nakwitaji bwana Unaye badilisha nakutu tengeneza Nanyenyekea kwako nanyenyekea kwako
Mimi nikama gari bovu wajua pakugusa ni wapi ni wake Mi nikama kinda la ndege baba oh ukiniacha nitaliwa na mwewe Ooh mimi nikama jumba bovu sijaezekwa na mkandarasi wangu ni wewe Maana tunaangamia kwa kukosa maarifa Nipe nipe nipe (busara) Ooh nipe (busara) Baba nipe maarifa na (busara nifanane nawe) Nifanane nawe bwana ninaomba (busara) Hekima yako na (busara) Domo langu nalijua mwenyewe (busara nifanane nawe)
Macho yako bwana yako kila mahali yakichunguza mbaya na mwema Mmh unitoe katika boma la miba maana ina choma Na unifanye zao lenya faida nisiwe hasara tena Unyenyekevu wako bwana (wako bwana) wakufanana (hakuna) Nami unifanye vivyo hivyo (ooh bwana) unifinyange (sawa sawa)
Mimi nikama gari bovu wajua pakugusa ni wapi ni wake Mi nikama kinda la ndege baba oh ukiniacha nitaliwa na mwewe Ooh mimi nikama jumba bovu sijaezekwa na mkandarasi wangu ni wewe Maana tunaangamia kwa kukosa maarifa Nipe nipe nipe (busara) Ooh nipe (busara) Baba nipe maarifa na (busara nifanane nawe) Nifanane nawe bwana ninaomba (busara) Hekima yako na (busara) Domo langu nalijua mwenyewe (busara nifanane nawe) Nipe nipe nipe (busara) Yesu nipe (busara) Niondolee kiburi baba nipe (busara nifanane nawe) Uuh sikunibeba kwa mbeleko hivo (busara) Bali nitualize kwa neno lako (busara) Bwana ninaomba hekima na (busara nifanane nawe)
Video
Walter Chilambo - Busara (Official Lyric Video)