Unaniona

Unaniona Lyrics

Kama Mungu angechagua watu wake 
Mimi singekuwepo duniani 
Kama Mungu angechagua watakatifu 
Mimi singekuwepo duniani  .

Mimi binadamu wala si malaika 
Mengi ninakosea na kukuchukiza 
Ninafanya mambo yasiyostahili 
Nimevuruga-vuruga mipango yako 
Wanihurumia,  .

Mbele ya macho ya wanadamu 
Nilikuwa nikijificha 
Kumbe wewe waniona 
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu) 
Nilikuwa (mnyenyekevu tena mpole sana) 
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu) 
Kwenye ibada (mnyenyekevu tena mpole sana) .

Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama 
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah 
Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama 
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah  .

Sasa nimetambua mbivu na mbichi ni zipi 
Sasa ninaelewa njia salama ni wapi 
Na nimejua bila ya wewe sifiki 
Hata nikila pasipo neno lako sishibi 
Neema yako (ila kwa neema yako) 
Upendo wako (ila kwa upendo wako) 
Na rehema zako zimenihimarisha tena  .

Mbele ya macho ya wanadamu 
Nilikuwa nikijificha 
Kumbe wewe waniona 
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu) 
Nilikuwa (mnyenyekevu tena mpole sana) 
Kwa Kujifanya (mtakatifu) tena (mkarimu) 
Kwenye ibada (mnyenyekevu tena mpole sana)  .

Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama 
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah 
Kumbe Mungu aniona, macho yako yanitazama 
Sikio lako lanisikia, siwezi jificha aah 

Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Unaniona:

0 Comments/Reviews

Bible Verses for Unaniona

Psalms 139 : 7

Where may I go from your spirit? how may I go in flight from you?

Hebrews 4 : 13

And there is nothing made which is not completely clear to him; there is nothing covered, but all things are open to the eyes of him with whom we have to do.

Proverbs 15 : 3

The eyes of the Lord are in every place, keeping watch on the evil and the good.