Sifa Lyrics

Najivunia by Walter Chilambo cover art

Walter Chilambo - Najivunia Lyrics

Artist:
Walter Chilambo
Album:
Thank You Lord
Official Release:
30 Jan 2021

Lyrics

Ningekuwa na mali
Magari ya kifari 
Bila amani 
Ninajivunia nini ? yeah


Pesa nyingi 
Nyumba na biashara 
Bila amani, yeah yeah 


Si mali kitu kama unaishi unalia ndani yako
Kwa maumivu tena umeshikilia imani zako 
Wamsahau mungu eti unajivuna ni nguvu zako
na shule umesoma tena unajidanganya ni akili zako 
Polee 


Duniani sipakujivunia jina
Wala mavazi ya heshima
Bali neno la uzima
litatuongoza vyemaaa


Chorus:
Mwezenu mimi jamanii
Najivunia kuwa na yesu
Vya dunia nimeviacha mbali
Najivunia kuwa na Yeye


Yesuu 
Pekee yake anasimama
Najivunia kuwa na Yesu
Mfalme wa wafalme
Najivunia kuwa na yeye


Yeye ni mwalimu wa walimu 
Ananifundisha vyema
Yeye ni tabibu wa karibu
Napata tiba njema 


Yeye ni dereva 
Anazijua njia zangu baba wo
yeye ndie Shujaa 
Anishindia vita yangu baba wo 


Si mali kitu kama unaishi unalia ndani yako 
Kwa maumivutena umeshikilia imani zako
Wamsahau mungu eti unajivuna ni nguvu zako 
Na shule umesoma tena unajidanganya ni akili zako
Polee


Duniani si pakujivunia jina 
Wala mavazi ya heshima 
Bali neno la uzima litatuongoza vyema 


[Chorus] 
Mwenzenu mimi jamani 
Najivunia kuwa na yesu 
Vya dunia nimeviacha mbali 
Najivunia kuwa na yeye 


Yesu pekee yake anasimama 
Najivunia kuwa na Yesu 
Mfalme wa wafalme 
Najivunia kuwa na Yesu 


Kwa mara hii mungu
Aliupenda ulimwengu 
Akamtoa mwanae wa pekee 
Ili kila mtu a mwaminie asipotee 
Bali awe na uzima wa milele 


Najivunia kuwa nae


Mwenzenu mimi jamani najivunia kuwa na Yesu
Vya dunia nimeviacha mbali 
Najivunia kuwa na yeye 


Yesu peke yake anasimama 
Najivunia kuwa na yesu 
Ninatembea kwa maringo
Najivunia kuwa na yeye


Video