Sifa Lyrics

Kampeni by Goodluck Gozbert cover art

Goodluck Gozbert - Kampeni Lyrics

Artist:
Goodluck Gozbert

Lyrics

Waliponikaribia na kuniaibisha eeh
Haukunyamaza ukanipigania eeh
Waliponivua utu na kulichana vazi langu
Na heshima ulinikumbatia nisiaibike


Waliposema mi mjinga, ujinga ninao
Sababu hekima haiezi bila upendo
Nilipoyafunika madhaifu yao
Na kumbe tafsiri ni mjinga kwao


Hata nilipokaa kimya wewe uliona yote
Uliponyamaza hukuacha nife
Ninakushukuru ooh, ooh Jire Dumo
Asante, ooh, oooh Igwe


Nitafanya kampeni za wema wako
Wajue Mungu ni mwema
Nitafanya kampeni za wema wako
Wajue Yesu ni mwema


Unaponibariki bariki adui zangu
Ili wasinisonge kutaka uhai wangu
Unapopiga mapigo samehe rafiki zangu
Wanaoning'ata alafu wanapuliza puu


Hata nilipokaa kimya wewe uliona yote
Uliponyamaza hukuacha nife
Ninakushukuru ooh, ooh Jire Dumo
Asante, ooh, oooh Igwe


Nitafanya kampeni za wema wako
Wajue Mungu ni mwema
Nitafanya kampeni za wema wako
Wajue Yesu ni mwema


Fadhili zako zadumu kila asubuhi
Wewe ni Mungu unayesimamisha mianga angani
Pendo lako lanitosha daima
Huruma yako imepita fahamu zangu
Ninakupenda Yesu, ninakupenda mwamba wangu


Video