Sifa Lyrics

Mungu wa Ishara - Uinuliwe by Emma Omonge cover art

Emma Omonge - Mungu wa Ishara - Uinuliwe Lyrics

Artist:
Emma Omonge

Lyrics

Baada ya kilio furaha sasa aah
Mafuta ya shangwe ondoa kuomboleza aah
Pahala pa dhihaka leta heshima
Majira na nyakati zote unabaki mwaminifu
Juu ya neema yako nashangaa ntakulipa nini
Uu mwaminifu ee Bwana, eeh Bwana,
U mwaminifu, ee Bwana.


Usiyepuuza kilio cha yeyote, wakubwa kwa wadogo
Maskini hata tajiri, sikio lako halibagui
Ukifuta makosa wala hukumbuki tena
Juu ya neema yako nashangaa ntakulipa nini
Uu mwaminifu ee Bwana, eeh Bwana,
U mwaminifu, ee Bwana.


Uinuliwe Mungu wa Ishara
Uinuliwe Mungu wa ajabu
Uinuliwe Mungu wa uweza
Uinuliwe Mungu wa ushindi


Uinuliwe Mungu wa Ishara
Uinuliwe Mungu wa ajabu
Uinuliwe Mungu wa uweza
Uinuliwe Mungu wa ushindi
Uinuliwe,Uinuliwe


Video