Sifa Lyrics

Unastahili by Ali Mukhwana cover art

Ali Mukhwana - Unastahili Lyrics

Artist:
Ali Mukhwana
Album:
Unastahili - Single
Official Release:
24 Dec 2024

Lyrics

Mwenye Enzi Ni weeh ni Wewe ×2
Unaetawala Duniani ni weeh ni Wewe 
Muumba Mbingu na inchi Ni weeh ni Wewe 


Unastahili Bwana Eeeh Unastahili Yesu Unastahili kuabudiwa Unastahili ×2


Kwa mapigo yako Yesu nimeona Mwanga kwa mateso yako Yesu Mimi nimepona ulifanyika maskini ili niwe tajiri Ulidhihakiwa mbele ya watu ili nione Mbingu mikuki Bwana ukachomwa ili nikombolewee Mwishoe Baba haukuhukumu yeyote uliwasamehe wote Unastahili Bwana eeeh 


Unastahili Bwana eeeh 
Unastahili Yesu 
Unastahili kuabudiwa Unastahili ×2


Nikitazama Duniani wengi wamekufa nami niko hai Hilo nidhitisho tosha wanipenda matendo yako Bwana yapita ufahamu Wangu Bwana wangu weeeh Unastahili eeeh 


Usikiye na kuomba kwangu kilio changu kikufikie nchi imeshiba mazao ya kazi zako Bwana Unastahili eeeh 


Unastahili Bwana eeeh 
Unastahili Yesu 
Unastahili kuabudiwa
Unastahili ×2
 
WEWE NDIWE MUNGU MKUU MUUMBA MBINGU NA NCHI UNAISHI NDANI YANGU 


Unaishi ndani yangu Bwana ×4 


Video