Jinsi Nilivyo Bwana Lyrics

Ali Mukhwana Tumaini kuabudu

Jinsi nilivyo Bwana 
Jinsi nilivyo 
Jinsi nilivyo Bwana 
Naja Kwako 
Jinsi nilivyo nipokee  .

Baba nikikumbuka ulikonitoa 
Ulinitoa mbali Baba eh 
Nikulinganishe na nani Baba haulinganishwi 
Siwezi siwezi bila wewe 
Ndiposa nasema jinsi nilivyo naja kwako
Wewe ni mchungaji wangu 
Wewe ni njia yangu ya uzima 
Jinsi nilivyo Bwana nipokee 
Bila wewe nitakuongee* na nani 
Bila wewe siyawezi eeh 
Jinsi nilivyo Bwana nipokee  .

Jinsi nilivyo Bwana 
Jinsi nilivyo 
Jinsi nilivyo Bwana 
Naja Kwako 
Jinsi nilivyo 
Jinsi nilivyo nipokee  .

Kila mwenye pumzi akuhitaji wewe 
Kila ana uhai Mungu ana haja nawe 
Kila mwenye pumzi akuhitaji wewe 
Kila ana uhai Mungu ana haja nawe 
Nami nina haja nawe Yesu 
Jinsi nilivyo nakuhitaji tu 
Nina haja nawee jinsi niliyo .

Jinsi nilivyo Bwana 
Jinsi nilivyo 
Jinsi nilivyo Bwana 
Jinsi nilivyo
Jinsi nilivyo nipokee  .

Tunaungana na maserafi na makerubi 
Jinsi nilivyo naja kwako 
Nimejaribu Bwana wanadamu Baba 
Wanadamu eeh wana mambo yao 
Wananihukumu na kusema Baba 
Mimi si wa haki eeh 
Toka nikujue Mungu wangu 
Umebadilisha maisha yangu 
Tangu nikujue mwokozi wangu 
Sijawai jutia 
Nilipokupokea mwokozi Yesu 
Sijawai juta hata siku moja 
Kumbe kwako kuna faida 
Kukujua ni muhimu sana 
Naja mbele zako Baba  .

Jinsi nilivyo Bwana 
Jinsi nilivyo 
Jinsi nilivyo Bwana 
nipokee  .Jinsi Nilivyo Bwana Video