AIC Chang'ombe - Moyo Lyrics

Lyrics

Kama machozi yangeweza kusimulia 
namna gani moyo unatunza mengi

Kama machozi yangeweza kusimulia
 namna gani moyo unavumilia

Moyo umebeba jeraha zangu
Eeh Moyo umebeba huzuni zangu

Moyo umebeba furaha yangu
Eeh Moyo umebeba ushindi wangu

Kuna muda kinywa kinatabasamu lakini Moyo unalia 
Kuna muda macho yanafurahi lakini Moyo unalia

Nitaulinda moyo wangu kuliko yote niyalindayo , niyalindayo,
 Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima , Za uzima, za uzima

Nitaulinda moyo wangu kuliko yote niyalindayo niyalindayo,
 Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima , Za uzima, za uzima

Kama machozi yangeweza kusimulia
 namna gani Moyo unatunza mengi

Kama machozi yangeweza kusimulia
 namna gani Moyo unavumilia

Linda Moyo wako kuliko yote uyalindayo
 Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima

MUNGU BABA nifute machozi yangu mimi
Waujua Moyo wangu nigange jeraha zangu nibaki

MUNGU BABA nifute machozi yangu mimi
Waujua moyo wangu nigange jeraha zangu nibaki

Video

AIC Chang'ombe Choir (CVC) - MOYO (Official Live Video)

Thumbnail for Moyo video
Loading...
In Queue
View Lyrics