Marko 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 4 (Swahili) Mark 4 (English)

Akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari. Marko 4:1

Again he began to teach by the seaside. A great multitude was gathered to him, so that he entered into a boat in the sea, and sat down. All the multitude were on the land by the sea.

Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake, Marko 4:2

He taught them many things in parables, and told them in his teaching,

Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda; Marko 4:3

"Listen! Behold, the farmer went out to sow,

ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. Marko 4:4

and it happened, as he sowed, some seed fell by the road, and the birds{TR adds "of the air"} came and devoured it.

Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na udongo haba; Marko 4:5

Others fell on the rocky ground, where it had little soil, and immediately it sprang up, because it had no depth of soil.

hata jua lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina mizizi ikanyauka. Marko 4:6

When the sun had risen, it was scorched; and because it had no root, it withered away.

Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda. Marko 4:7

Others fell among the thorns, and the thorns grew up, and choked it, and it yielded no fruit.

Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia. Marko 4:8

Others fell into the good ground, and yielded fruit, growing up and increasing. Some brought forth thirty times, some sixty times, and some one hundred times as much."

Akasema, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie. Marko 4:9

He said, "Whoever has ears to hear, let him hear."

Naye alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza habari za ile mifano. Marko 4:10

When he was alone, those who were around him with the twelve asked him about the parables.

Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano, Marko 4:11

He said to them, "To you is given the mystery of the Kingdom of God, but to those who are outside, all things are done in parables,

ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa. Marko 4:12

that 'seeing they may see, and not perceive; and hearing they may hear, and not understand; lest perhaps they should turn again, and their sins should be forgiven them.'"

Akawaambia, Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje? Marko 4:13

He said to them, "Don't you understand this parable? How will you understand all of the parables?

Mpanzi huyo hulipanda neno. Marko 4:14

The farmer sows the word.

Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. Marko 4:15

These are the ones by the road, where the word is sown; and when they have heard, immediately Satan comes, and takes away the word which has been sown in them.

Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha; Marko 4:16

These in like manner are those who are sown on the rocky places, who, when they have heard the word, immediately receive it with joy.

ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa. Marko 4:17

They have no root in themselves, but are short-lived. When oppression or persecution arises because of the word, immediately they stumble.

Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, Marko 4:18

Others are those who are sown among the thorns. These are those who have heard the word,

na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai. Marko 4:19

and the cares of this age, and the deceitfulness of riches, and the lusts of other things entering in choke the word, and it becomes unfruitful.

Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia. Marko 4:20

These are those which were sown on the good ground: such as hear the word, and accept it, and bear fruit, some thirty times, some sixty times, and some one hundred times."

Akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango? Marko 4:21

He said to them, "Is the lamp brought to be put under a basket{Literally, a modion, a dry measuring basket containing about a peck (about 9 litres)} or under a bed? Isn't it put on a lampstand?

Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi. Marko 4:22

For there is nothing hidden, except that it should be made known; neither was anything made secret, but that it should come to light.

Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. Marko 4:23

If any man has ears to hear, let him hear."

Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa. Marko 4:24

He said to them, "Take heed what you hear. With whatever measure you measure, it will be measured to you, and more will be given to you who hear.

Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. Marko 4:25

For whoever has, to him will more be given, and he who doesn't have, from him will be taken away even that which he has."

Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; Marko 4:26

He said, "The Kingdom of God is as if a man should cast seed on the earth,

akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Marko 4:27

and should sleep and rise night and day, and the seed should spring up and grow, he doesn't know how.

Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Marko 4:28

For the earth bears fruit: first the blade, then the ear, then the full grain in the ear.

Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika. Marko 4:29

But when the fruit is ripe, immediately he puts forth the sickle, because the harvest has come."

Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? Marko 4:30

He said, "How will we liken the Kingdom of God? Or with what parable will we illustrate it?

Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi, Marko 4:31

It's like a grain of mustard seed, which, when it is sown in the earth, though it is less than all the seeds that are on the earth,

lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake. Marko 4:32

yet when it is sown, grows up, and becomes greater than all the herbs, and puts out great branches, so that the birds of the sky can lodge under its shadow."

Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia; Marko 4:33

With many such parables he spoke the word to them, as they were able to hear it.

wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha. Marko 4:34

Without a parable he didn't speak to them; but privately to his own disciples he explained all things.

Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. Marko 4:35

On that day, when evening had come, he said to them, "Let's go over to the other side."

Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. Marko 4:36

Leaving the multitude, they took him with them, even as he was, in the boat. Other small boats were also with him.

Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Marko 4:37

There arose a great wind storm, and the waves beat into the boat, so much that the boat was already filled.

Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Marko 4:38

He himself was in the stern, asleep on the cushion, and they woke him up, and told him, "Teacher, don't you care that we are dying?"

Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Marko 4:39

He awoke, and rebuked the wind, and said to the sea, "Peace! Be still!" The wind ceased, and there was a great calm.

Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? Marko 4:40

He said to them, "Why are you so afraid? How is it that you have no faith?"

Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii? Marko 4:41

They were greatly afraid, and said to one another, "Who then is this, that even the wind and the sea obey him?"