Marko 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 16 (Swahili) Mark 16 (English)

Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Marko 16:1

When the Sabbath was past, Mary Magdalene, and Mary the mother of James, and Salome, bought spices, that they might come and anoint him.

Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza; Marko 16:2

Very early on the first day of the week, they came to the tomb when the sun had risen.

wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Marko 16:3

They were saying among themselves, "Who will roll away the stone from the door of the tomb for us?"

Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno. Marko 16:4

for it was very big. Looking up, they saw that the stone was rolled back.

Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Marko 16:5

Entering into the tomb, they saw a young man sitting on the right side, dressed in a white robe, and they were amazed.

Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka. Marko 16:6

He said to them, "Don't be amazed. You seek Jesus, the Nazarene, who has been crucified. He has risen. He is not here. Behold, the place where they laid him!

Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia. Marko 16:7

But go, tell his disciples and Peter, 'He goes before you into Galilee. There you will see him, as he said to you.'"

Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [ Marko 16:8

They went out,{TR adds "quickly"} and fled from the tomb, for trembling and astonishment had come on them. They said nothing to anyone; for they were afraid.

Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. Marko 16:9

Now when he had risen early on the first day of the week, he appeared first to Mary Magdalene, from whom he had cast out seven demons.

Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia. Marko 16:10

She went and told those who had been with him, as they mourned and wept.

Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki. Marko 16:11

When they heard that he was alive, and had been seen by her, they disbelieved.

Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. Marko 16:12

After these things he was revealed in another form to two of them, as they walked, on their way into the country.

Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki. Marko 16:13

They went away and told it to the rest. They didn't believe them, either.

Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Marko 16:14

Afterward he was revealed to the eleven themselves as they sat at the table, and he rebuked them for their unbelief and hardness of heart, because they didn't believe those who had seen him after he had risen.

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Marko 16:15

He said to them, "Go into all the world, and preach the Gospel to the whole creation.

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Marko 16:16

He who believes and is baptized will be saved; but he who disbelieves will be condemned.

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; Marko 16:17

These signs will accompany those who believe: in my name they will cast out demons; they will speak with new languages;

watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Marko 16:18

they will take up serpents; and if they drink any deadly thing, it will in no way hurt them; they will lay hands on the sick, and they will recover."

Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Marko 16:19

So then the Lord Jesus, after he had spoken to them, was received up into heaven, and sat down at the right hand of God.

Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.] Marko 16:20

They went out, and preached everywhere, the Lord working with them, and confirming the word by the signs that followed. Amen.