Marko 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 11 (Swahili) Mark 11 (English)

Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake, Marko 11:1

When they drew near to Jerusalem, to Bethsphage{TR reads "Bethphage" instead of "Bethsphage"} and Bethany, at the Mount of Olives, he sent two of his disciples,

akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. Marko 11:2

and said to them, "Go your way into the village that is opposite you. Immediately as you enter into it, you will find a young donkey tied, on which no one has sat. Untie him, and bring him.

Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa. Marko 11:3

If anyone asks you, 'Why are you doing this?' say, 'The Lord needs him;' and immediately he will send him back here."

Wakaenda zao, wakamwona mwana-punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. Marko 11:4

They went away, and found a young donkey tied at the door outside in the open street, and they untied him.

Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda? Marko 11:5

Some of those who stood there asked them, "What are you doing, untying the young donkey?"

Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza, nao wakawaruhusu. Marko 11:6

They said to them just as Jesus had said, and they let them go.

Wakamletea Yesu yule mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake. Marko 11:7

They brought the young donkey to Jesus, and threw their garments on it, and Jesus sat on it.

Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani. Marko 11:8

Many spread their garments on the way, and others were cutting down branches from the trees, and spreading them on the road.

Nao watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana; Marko 11:9

Those who went in front, and those who followed, cried out, "Hosanna! Blessed is he who comes in the name of the Lord!

umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni. Marko 11:10

Blessed is the kingdom of our father David that is coming in the name of the Lord! Hosanna in the highest!"

Naye akaingia Yerusalemu hata ndani ya hekalu; na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka, akaenda Bethania pamoja na wale Thenashara. Marko 11:11

Jesus entered into the temple in Jerusalem. When he had looked around at everything, it being now evening, he went out to Bethany with the twelve.

Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Marko 11:12

The next day, when they had come out from Bethany, he was hungry.

Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Marko 11:13

Seeing a fig tree afar off having leaves, he came to see if perhaps he might find anything on it. When he came to it, he found nothing but leaves, for it was not the season for figs.

Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. Marko 11:14

Jesus told it, "May no one ever eat fruit from you again!" and his disciples heard it.

Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa; Marko 11:15

They came to Jerusalem, and Jesus entered into the temple, and began to throw out those who sold and those who bought in the temple, and overthrew the tables of the money-changers, and the seats of those who sold the doves.

wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu. Marko 11:16

He would not allow anyone to carry a container through the temple.

Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. Marko 11:17

He taught, saying to them, "Isn't it written, 'My house will be called a house of prayer for all the nations?' But you have made it a den of robbers!"

Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangaa kwa mafundisho yake. Marko 11:18

The chief priests and the scribes heard it, and sought how they might destroy him. For they feared him, because all the multitude was astonished at his teaching.

Na kulipokuwa jioni alitoka mjini. Marko 11:19

When evening came, he went out of the city.

Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Marko 11:20

As they passed by in the morning, they saw the fig tree withered away from the roots.

Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. Marko 11:21

Peter, remembering, said to him, "Rabbi, look! The fig tree which you cursed has withered away."

Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Marko 11:22

Jesus answered them, "Have faith in God.

Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Marko 11:23

For most assuredly I tell you, whoever may tell this mountain, 'Be taken up and cast into the sea,' and doesn't doubt in his heart, but believes that what he says is happening; he shall have whatever he says.

Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Marko 11:24

Therefore I tell you, all things whatever you pray and ask for, believe that you receive them, and you shall have them.

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Marko 11:25

Whenever you stand praying, forgive, if you have anything against anyone; so that your Father, who is in heaven, may also forgive you your transgressions.

Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.] Marko 11:26

But if you do not forgive, neither will your Father in heaven forgive your transgressions."

Wakafika Yerusalemu tena; hata alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee, Marko 11:27

They came again to Jerusalem, and as he was walking in the temple, the chief priests, and the scribes, and the elders came to him,

wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya? Marko 11:28

and they began saying to him, "By what authority do you do these things? Or who gave you this authority to do these things?"

Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya. Marko 11:29

Jesus said to them, "I will ask you one question. Answer me, and I will tell you by what authority I do these things.

Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni. Marko 11:30

The baptism of John -- was it from heaven, or from men? Answer me."

Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini? Marko 11:31

They reasoned with themselves, saying, "If we should say, 'From heaven;' he will say, 'Why then did you not believe him?'

Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, -- waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi. Marko 11:32

If we should say, 'From men'"--they feared the people, for all held John to really be a prophet.

Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya. Marko 11:33

They answered Jesus, "We don't know." Jesus said to them, "Neither do I tell you by what authority I do these things."