Marko 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 10 (Swahili) Mark 10 (English)

Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea. Marko 10:1

He arose from there and came into the borders of Judea and beyond the Jordan. Multitudes came together to him again. As he usually did, he was again teaching them.

Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu. Marko 10:2

Pharisees came to him testing him, and asked him, "Is it lawful for a man to divorce his wife?"

Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini? Marko 10:3

He answered, "What did Moses command you?"

Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha. Marko 10:4

They said, "Moses allowed a certificate of divorce to be written, and to divorce her."

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Marko 10:5

But Jesus said to them, "For your hardness of heart, he wrote you this commandment.

Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Marko 10:6

But from the beginning of the creation, 'God made them male and female.

Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; Marko 10:7

For this cause a man will leave his father and mother, and will join to his wife,

na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Marko 10:8

and the two will become one flesh,' so that they are no longer two, but one flesh.

Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Marko 10:9

What therefore God has joined together, let no man separate."

Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo. Marko 10:10

In the house, his disciples asked him again about the same matter.

Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake; Marko 10:11

He said to them, "Whoever divorces his wife, and marries another, commits adultery against her.

na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini. Marko 10:12

If a woman herself divorces her husband, and marries another, she commits adultery."

Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Marko 10:13

They were bringing to him little children, that he should touch them, but the disciples rebuked those who were bringing them.

Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Marko 10:14

But when Jesus saw it, he was moved with indignation, and said to them, "Allow the little children to come to me! Don't forbid them, for the Kingdom of God belongs to such as these.

Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. Marko 10:15

Most assuredly I tell you, whoever will not receive the Kingdom of God like a little child, he will in no way enter into it."

Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia. Marko 10:16

He took them in his arms, and blessed them, laying his hands on them.

Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Marko 10:17

As he was going out into the way, one ran to him, knelt before him, and asked him, "Good Teacher, what shall I do that I may inherit eternal life?"

Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Marko 10:18

Jesus said to him, "Why do you call me good? No one is good except one-- God.

Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Marko 10:19

You know the commandments: 'Do not murder,' 'Do not commit adultery,' 'Do not steal,' 'Do not give false testimony,' 'Do not defraud,' 'Honor your father and mother.'"

Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Marko 10:20

He said to him, "Teacher, I have observed all these things from my youth."

Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Marko 10:21

Jesus looking at him loved him, and said to him, "One thing you lack. Go, sell whatever you have, and give to the poor, and you will have treasure in heaven; and come, follow me, taking up the cross."

Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Marko 10:22

But his face fell at that saying, and he went away sorrowful, for he was one who had great possessions.

Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Marko 10:23

Jesus looked around, and said to his disciples, "How difficult it is for those who have riches to enter into the Kingdom of God!"

Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Marko 10:24

The disciples were amazed at his words. But Jesus answered again, "Children, how hard is it for those who trust in riches to enter into the Kingdom of God!

Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Marko 10:25

It is easier for a camel to go through a{or, the} needle's eye than for a rich man to enter into the Kingdom of God."

Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka? Marko 10:26

They were exceedingly astonished, saying to him, "Then who can be saved?"

Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. Marko 10:27

Jesus, looking at them, said, "With men it is impossible, but not with God, for all things are possible with God."

Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Marko 10:28

Peter began to tell him, "Behold, we have left all, and have followed you."

Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, Marko 10:29

Jesus said, "Most assuredly I tell you, there is no one who has left house, or brothers, or sisters, or father, or mother, or wife, or children, or land, for my sake, and for the Gospel's sake,

ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Marko 10:30

but he will receive one hundred times more now in this time, houses, brothers, sisters, mothers, children, and land, with persecutions; and in the age to come eternal life.

Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza. Marko 10:31

But many who are first will be last; and the last first."

Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Thenashara, akaanza kuwaambia habari za mambo yatakayompata, Marko 10:32

They were on the way, going up to Jerusalem; and Jesus was going in front of them, and they were amazed; and those who followed were afraid. He again took the twelve, and began to tell them the things that were going to happen to him.

akisema, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa Mataifa, Marko 10:33

"Behold, we are going up to Jerusalem. The Son of Man will be delivered to the chief priests and the scribes. They will condemn him to death, and will deliver him to the Gentiles.

nao watamdhihaki, na kumtemea mate, na kumpiga mijeledi, na kumwua; na baada ya siku tatu atafufuka. Marko 10:34

They will mock him, spit on him, scourge him, and kill him. On the third day he will rise again."

Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba. Marko 10:35

James and John, the sons of Zebedee, came near to him, saying, "Teacher, we want you to do for us whatever we will ask."

Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini? Marko 10:36

He said to them, "What do you want me to do for you?"

Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako. Marko 10:37

They said to him, "Grant to us that we may sit, one at your right hand, and one at your left hand, in your glory."

Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Marko 10:38

But Jesus said to them, "You don't know what you are asking. Are you able to drink the cup that I drink, and to be baptized with the baptism that I am baptized with?"

Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa; Marko 10:39

They said to him, "We are able." Jesus said to them, "You shall indeed drink the cup that I drink, and you shall be baptized with the baptism that I am baptized with;

lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari. Marko 10:40

but to sit at my right hand and at my left hand is not mine to give, but for whom it has been prepared."

Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana. Marko 10:41

When the ten heard it, they began to be indignant towards James and John.

Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Marko 10:42

Jesus summoned them, and said to them, "You know that they who are recognized as rulers over the Gentiles lord it over them, and their great ones exercise authority over them.

Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, Marko 10:43

But it shall not be so among you, but whoever wants to become great among you shall be your servant.

na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. Marko 10:44

Whoever of you wants to become first among you, shall be bondservant of all.

Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Marko 10:45

For the Son of Man also came not to be served, but to serve, and to give his life as a ransom for many."

Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia. Marko 10:46

They came to Jericho. As he went out from Jericho, with his disciples and a great multitude, the son of Timaeus, Bartimaeus, a blind beggar, was sitting by the road.

Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu. Marko 10:47

When he heard that it was Jesus the Nazarene, he began to cry out, and say, "Jesus, you son of David, have mercy on me!"

Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu. Marko 10:48

Many rebuked him, that he should be quiet, but he cried out much more, "You son of David, have mercy on me!"

Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita. Marko 10:49

Jesus stood still, and said, "Call him." They called the blind man, saying to him, "Cheer up! Get up. He is calling you!"

Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu. Marko 10:50

He, casting away his cloak, sprang up, and came to Jesus.

Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. Marko 10:51

Jesus asked him, "What do you want me to do for you?" The blind man said to him, "Rhabboni,{Rhabboni is a transliteration of the Hebrew word for "great teacher."} that I may see again."

Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani. Marko 10:52

Jesus said to him, "Go your way. Your faith has made you well." Immediately he received his sight, and followed Jesus in the way.