Marko 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 1 (Swahili) Mark 1 (English)

Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Marko 1:1

The beginning of the Gospel of Jesus Christ, the Son of God.

Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako. Marko 1:2

As it is written in the prophets, "Behold, I send my messenger before your face, Who will prepare your way before you.

Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Marko 1:3

The voice of one crying in the wilderness, 'Make ready the way of the Lord! Make his paths straight!'"

Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Marko 1:4

John came baptizing{To baptize means to immerse in (or wash with) water (or fire). This baptizm is not just to cleanse the body, but as an outward sign of an inward spiritual cleansing and commitment.} in the wilderness and preaching the baptism of repentance for forgiveness of sins.

Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. Marko 1:5

All the country of Judea and all those of Jerusalem went out to him. They were baptized by him in the Jordan river, confessing their sins.

Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwitu. Marko 1:6

John was clothed with camel's hair and a leather belt around his loins. He ate locusts and wild honey.

Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Marko 1:7

He preached, saying, "After me comes he who is mightier than I, the thong of whose sandals I am not worthy to stoop down and loosen.

Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu. Marko 1:8

I baptized you in{The Greek word (en) translated here as "in" could also be translated as "with" in some contexts.} water, but he will baptize you in the Holy Spirit."

Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. Marko 1:9

It happened in those days, that Jesus came from Nazareth of Galilee, and was baptized by John in the Jordan.

Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; Marko 1:10

Immediately coming up from the water, he saw the heavens parting, and the Spirit descending on him like a dove.

na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. Marko 1:11

A voice came out of the sky, "You are my beloved Son, in whom I am well pleased."

Mara Roho akamtoa aende nyikani. Marko 1:12

Immediately the Spirit drove him out into the wilderness.

Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia. Marko 1:13

He was there in the wilderness forty days tempted by Satan. He was with the wild animals; and the angels were ministering to him.

Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, Marko 1:14

Now after John was taken into custody, Jesus came into Galilee, preaching the Gospel of the Kingdom of God,

akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Marko 1:15

and saying, "The time is fulfilled, and the Kingdom of God is at hand! Repent, and believe in the Gospel."

Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Marko 1:16

Passing along by the sea of Galilee, he saw Simon and Andrew the brother of Simon casting a net in the sea, for they were fishermen.

Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Marko 1:17

Jesus said to them, "Come after me, and I will make you into fishers for men."

Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Marko 1:18

Immediately they left their nets, and followed him.

Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa chomboni, wakizitengeneza nyavu zao. Marko 1:19

Going on a little further from there, he saw James the son of Zebedee, and John, his brother, who were also in the boat mending the nets.

Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya chombo pamoja na watu wa mshahara, wakaenda, wakamfuata. Marko 1:20

Immediately he called them, and they left their father, Zebedee, in the boat with the hired servants, and went after him.

Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Marko 1:21

They went into Capernaum, and immediately on the Sabbath day he entered into the synagogue and taught.

Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi. Marko 1:22

They were astonished at his teaching, for he taught them as having authority, and not as the scribes.

Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, Marko 1:23

Immediately there was in their synagogue a man with an unclean spirit, and he cried out,

akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Marko 1:24

saying, "Ha! What do we have to do with you, Jesus, you Nazarene? Have you come to destroy us? I know you who you are: the Holy One of God!"

Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Marko 1:25

Jesus rebuked him, saying, "Be quiet, and come out of him!"

Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Marko 1:26

The unclean spirit, convulsing him and crying with a loud voice, came out of him.

Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii! Marko 1:27

They were all amazed, so that they questioned among themselves, saying, "What is this? A new teaching? For with authority he commands even the unclean spirits, and they obey him!"

Habari zake zikaenea mara kotekote katika nchi zote kandokando ya Galilaya. Marko 1:28

The report of him went out immediately everywhere into all the region of Galilee and its surrounding area.

Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. Marko 1:29

Immediately, when they had come out of the synagogue, they came into the house of Simon and Andrew, with James and John.

Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. Marko 1:30

Now Simon's wife's mother lay sick with a fever, and immediately they told him about her.

Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia. Marko 1:31

He came and took her by the hand, and raised her up. The fever left her, and she served them.

Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo. Marko 1:32

At evening, when the sun had set, they brought to him all who were sick, and those who were possessed by demons.

Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Marko 1:33

All the city was gathered together at the door.

Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. Marko 1:34

He healed many who were sick with various diseases, and cast out many demons. He didn't allow the demons to speak, because they knew him.

Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. Marko 1:35

Early in the night, he rose up and went out, and departed into a deserted place, and prayed there.

Simoni na wenziwe wakamfuata; Marko 1:36

Simon and those who were with him followed after him;

nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. Marko 1:37

and they found him, and told him, "Everyone is looking for you."

Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea. Marko 1:38

He said to them, "Let's go elsewhere into the next towns, that I may preach there also, because for this reason I came forth."

Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo. Marko 1:39

He went into their synagogues throughout all Galilee, preaching and casting out demons.

Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. Marko 1:40

There came to him a leper, begging him, kneeling down to him, and saying to him, "If you want to, you can make me clean."

Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. Marko 1:41

Being moved with compassion, he stretched out his hand, and touched him, and said to him, "I want to. Be made clean."

Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Marko 1:42

When he had said this, immediately the leprosy departed from him, and he was made clean.

Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, Marko 1:43

He strictly warned him, and immediately sent him out,

akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao. Marko 1:44

and said to him, "See you say nothing to anybody, but go show yourself to the priest, and offer for your cleansing the things which Moses commanded, for a testimony to them."

Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwako nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila mahali. Marko 1:45

But he went out, and began to proclaim it much, and to spread about the matter, so that Jesus could no more openly enter into a city, but was outside in desert places: and they came to him from everywhere.