Wagalatia 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wagalatia 2 (Swahili) Galatians 2 (English)

Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nalipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami. Wagalatia 2:1

Then after a period of fourteen years I went up again to Jerusalem with Barnabas, taking Titus also with me.

Nami nalikwenda kwa kuwa nalifunuliwa, nikawaeleza injili ile niihubiriyo katika Mataifa, lakini kwa faragha kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio bure, au nalipiga mbio bure. Wagalatia 2:2

I went up by revelation, and I laid before them the Gospel which I preach among the Gentiles, but privately before those who were respected, for fear that I might be running, or had run, in vain.

Lakini Tito aliyekuwa pamoja nami, naye ni Myunani, hakulazimishwa kutahiriwa. Wagalatia 2:3

But not even Titus, who was with me, being a Greek, was compelled to be circumcised.

Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri; ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani; Wagalatia 2:4

This was because of the false brothers secretly brought in, who stole in to spy out our liberty which we have in Christ Jesus, that they might bring us into bondage;

ambao hata saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae pamoja nanyi. Wagalatia 2:5

to whom we gave no place in the way of subjection, not for an hour, that the truth of the Gospel might continue with you.

Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; Wagalatia 2:6

But from those who were reputed to be important (whatever they were, it makes no difference to me; God doesn't show partiality to man)--they, I say, who were respected imparted nothing to me,

bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa; Wagalatia 2:7

but to the contrary, when they saw that I had been entrusted with the Gospel for the uncircumcision, even as Peter with the Gospel for the circumcision

(maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa); Wagalatia 2:8

(for he who appointed Peter to the apostleship of the circumcision appointed me also to the Gentiles);

tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara; Wagalatia 2:9

and when they perceived the grace that was given to me, James and Cephas and John, they who were reputed to be pillars, gave to me and Barnabas the right hand of fellowship, that we should go to the Gentiles, and they to the circumcision.

ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya. Wagalatia 2:10

They only asked us to remember the poor--which very thing I was also zealous to do.

Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu. Wagalatia 2:11

But when Peter came to Antioch, I resisted him to the face, because he stood condemned.

Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa. Wagalatia 2:12

For before some people came from James, he ate with the Gentiles. But when they came, he drew back and separated himself, fearing those who were of the circumcision.

Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. Wagalatia 2:13

And the rest of the Jews joined him in his hypocrisy; so that even Barnabas was carried away with their hypocrisy.

Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi? Wagalatia 2:14

But when I saw that they didn't walk uprightly according to the truth of the Gospel, I said to Peter before them all, "If you, being a Jew, live as the Gentiles do, and not as the Jews do, why do you compel the Gentiles to live as the Jews do?

Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wakosaji wa Mataifa, Wagalatia 2:15

"We, being Jews by nature, and not Gentile sinners,

hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. Wagalatia 2:16

yet knowing that a man is not justified by the works of the law but through the faith of Jesus Christ, even we believed in Christ Jesus, that we might be justified by faith in Christ, and not by the works of the law, because no flesh will be justified by the works of the law.

Lakini ikiwa sisi wenyewe, kwa kutafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, tulionekana kuwa wenye dhambi, je! Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? Hasha! Wagalatia 2:17

But if, while we sought to be justified in Christ, we ourselves also were found sinners, is Christ a servant of sin? Certainly not!

Maana nikiyajenga tena yale niliyoyabomoa, naonyesha ya kuwa mimi mwenyewe ni mkosaji. Wagalatia 2:18

For if I build up again those things which I destroyed, I prove myself a law-breaker.

Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie Mungu. Wagalatia 2:19

For I, through the law, died to the law, that I might live to God.

Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. Wagalatia 2:20

I have been crucified with Christ, and it is no longer I that live, but Christ living in me. That life which I now live in the flesh, I live by faith in the Son of God, who loved me, and gave himself up for me.

Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure. Wagalatia 2:21

I don't make void the grace of God. For if righteousness is through the law, then Christ died for nothing!"