Wagalatia 5 Swahili & English
Wagalatia 5 (Swahili) | Galatians 5 (English) |
---|---|
Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Wagalatia 5:1 |
Stand firm therefore in the liberty by which Christ has made us free, and don't be entangled again with a yoke of bondage. |
Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Wagalatia 5:2 |
Behold, I, Paul, tell you that if you receive circumcision, Christ will profit you nothing. |
Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Wagalatia 5:3 |
Yes, I testify again to every man who receives circumcision, that he is a debtor to do the whole law. |
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Wagalatia 5:4 |
You are alienated from Christ, you who desire to be justified by the law. You have fallen away from grace. |
Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Wagalatia 5:5 |
For we, through the Spirit, by faith wait for the hope of righteousness. |
Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo. Wagalatia 5:6 |
For in Christ Jesus neither circumcision amounts to anything, nor uncircumcision, but faith working through love. |
Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? Wagalatia 5:7 |
You were running well! Who interfered with you that you should not obey the truth? |
Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. Wagalatia 5:8 |
This persuasion is not from him who calls you. |
Chachu kidogo huchachua donge zima. Wagalatia 5:9 |
A little yeast grows through the whole lump. |
Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote. Wagalatia 5:10 |
I have confidence toward you in the Lord that you will think no other way. But he who troubles you will bear his judgment, whoever he is. |
Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika! Wagalatia 5:11 |
But I, brothers, if I still preach circumcision, why am I still persecuted? Then the stumbling-block of the cross has been removed. |
Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao! Wagalatia 5:12 |
I wish that those who disturb you would cut themselves off. |
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Wagalatia 5:13 |
For you, brothers, were called for freedom. Only don't use your freedom for gain to the flesh, but through love be servants to one another. |
Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Wagalatia 5:14 |
For the whole law is fulfilled in one word, in this: "You shall love your neighbor as yourself." |
Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana. Wagalatia 5:15 |
But if you bite and devour one another, be careful that you don't consume one another. |
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Wagalatia 5:16 |
But I say, walk by the Spirit, and you won't fulfill the lust of the flesh. |
Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Wagalatia 5:17 |
For the flesh lusts against the Spirit, and the Spirit against the flesh; and these are contrary to one other, that you may not do the things that you desire. |
Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Wagalatia 5:18 |
But if you are led by the Spirit, you are not under the law. |
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, Wagalatia 5:19 |
Now the works of the flesh are obvious, which are: adultery, sexual immorality, uncleanness, lustfulness, |
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, Wagalatia 5:20 |
idolatry, sorcery, hatred, strife, jealousies, outbursts of anger, rivalries, divisions, heresies, |
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:21 |
envyings, murders, drunkenness, orgies, and things like these; of which I forewarn you, even as I also forewarned you, that those who practice such things will not inherit the Kingdom of God. |
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, Wagalatia 5:22 |
But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faithfulness, |
upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Wagalatia 5:23 |
gentleness, and self-control. Against such things there is no law. |
Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Wagalatia 5:24 |
Those who belong to Christ have crucified the flesh with its passions and lusts. |
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Wagalatia 5:25 |
If we live by the Spirit, let's also walk by the Spirit. |
Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana. Wagalatia 5:26 |
Let's not become conceited, provoking one another, and envying one another. |