Godwin Ombeni - Mwamba Wenye Imara Lyrics

Mwamba Wenye Imara Lyrics

Mwamba wenye imara, kwako nitajificha!
maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi

Kwa kazi zote pia , sitimizi sheria.
nijapofanya bidii, nikilia nakudhii,
hayaishi makosa: Ndiwe wa kuokoa.

Sina cha mkononi, Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.

Nikungojapo chini, nakwenda kaburini;
nipaapo Mbinguni, na kukwona enzini;
roho yangu na iwe rahani mwako wewe.

Swahili version of Rock of Ages cleft for me






Mwamba Wenye Imara Video

Godwin Ombeni Songs

Related Songs