Lyrics
[Verse 1]
Eh Baba tumekuja kwako
Tunaomba uturehemu
Watoto wako tuko miguuni pako
Tunalilia kwa ajili ya mateso
Tunayaona tunayopitia dunia hii
[Verse 2]
Majirani wametugeuka sisi
Hata ndugu wamekuwa maadui
Wanatutesa kila usiku, kila kuchao
[Chorus]
Kimbilio letu ni wewe
Kimbilio pekee ni wewe (Lord)
Mwenye uwezo sisi twakutambua
Tukilemewa tunajificha kwako
Wewe ni mwamba na sisi tuchini yako
Ukitamka jambo linatendeka
Hata mapepo yote hutawanyika
Nyoosha mkono, Mtuliza Bahari
[Verse 3]
Kuna wengi wamepoteza wapendwa wao
Kwa sababu ya chuki
Wapo wengi wamepoteza mali yao
Kwa sababu ya wivu
Kuna wengi wamepoteza mifugo
Wamepoteza mimea yao shambani
Na biashara zao zimeangushwa
[Chorus]
Kimbilio letu ni wewe
Kimbilio pekee ni wewe
Mwenye uwezo sisi twakutambua
Tukilemewa tunajificha kwako
Wewe ni mwamba na sisi tuchini yako
Ukitamka jambo linatendeka
Hata mapepo yote hutawanyika
Nyoosha mkono, Mtuliza Bahari
[Bridge]
Siku ya kiama inarejea
Maswali mengi yataulizwa pale
Nilikupa jirani umtunze
Mbona ukamtenda?
Miti na mawe ndio mashahidi
Paala nyumba yako litakukana
Likishuhudia uliyotenda
[Chorus]
Mwenye uwezo sisi twakutambua
Tukilemewa tunajificha kwako
Wewe ni mwamba na sisi tuchini yako
Ukitamka jambo linatendeka
Hata mapepo yote hutawanyika
Nyoosha mkono, Mtuliza Bahari
[Outro]
Mwenye uwezo sisi twakutambua
Tukilemewa tunajificha kwako
Wewe ni mwamba na sisi tuchini yako
Ukitamka jambo linatendeka
Hata mapepo yote hutawanyika
Nyoosha mkono, Mtuliza Bahari