Sifa Lyrics

Nitaingia Lango Lake  by Msanii Music Group cover art

Msanii Music Group - Nitaingia Lango Lake Lyrics

Artist:
Msanii Music Group

Lyrics

Wakati nitajikuta, mbinguni kwa baba,
Nitajua ya ulimwengu nimeshayaacha,
Halleluya nitasifu, kufika mbinguni,
Hossana nitaingia kwa shangwe


Nitaingia lango lake na sifa moyoni,
Nitaingia kwa shangwe kuu,
Nitasema ni siku njema bwana ameifanya,
Nitafurahi kufika mbinguni


Nchi nzuri nchi safi, kwa baba yangu,
Kuna amani kuna furaha, uko ni kusifu,
Tutakaa na mungu wetu, nchi ya amani,
Hossana nitaingia kwa shangwe,


Nitaingia lango lake na sifa moyoni,
Nitaingia kwa shangwe kuu,
Nitasema ni siku njema bwana ameifanya,
Nitafurahi kufika mbinguni


Nitawaona watakatifu, manabii wote
Hata mitume nchi hiyo, nitawaona,
Tutakula meza moja, nchi ya amani,
Hossana nitaingia kwa shangwe


Nitaingia lango lake na sifa moyoni,
Nitaingia kwa shangwe kuu,
Nitasema ni siku njema bwana ameifanya,
Nitafurahi kufika mbinguni


Video