kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua

by Emachichi | in Tenzi
Mp3

Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;
lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

# I will Know HimTop Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Kazi Yangu Ikiisha Nami Nikiokoka - Nitamjua:

2 Comments/Reviews

  • Waziri

    Mungu akubariki mtumishi was mungu 1 year ago

  • Roseline

    Que Dieu vous bénisse mon frere , pouvez vous m'envoyer cette chanson en français s'il vous plaît que Dieu vous bénisse 1 year ago