kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua

kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua Lyrics

Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka
Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele;
lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

# I will Know HimShare:

Write a review/comment of Kazi Yangu Ikiisha Nami Nikiokoka - Nitamjua:

2 Comments/Reviews

 • Waziri

  Mungu akubariki mtumishi was mungu 4 months ago

 • Roseline

  Que Dieu vous bénisse mon frere , pouvez vous m'envoyer cette chanson en français s'il vous plaît que Dieu vous bénisse 8 months ago

 • Emachichi

  @emachichi

  Bio

  View all songs, albums & biography of Emachichi

  View Profile

  Bible Verses for kazi yangu ikiisha nami nikiokoka - Nitamjua

  No verses added for this song, suggest a verse to be included in the comments section

  Mp3 Songs & Download from iTunes

  • listen on Itunes Music